SoC04 Tunatakiwa kutatua matatizo au changamoto zilizokuwa tishio kwa maendeleo ya Tanzania na kuleta mikakati thabiti

Tanzania Tuitakayo competition threads

Wise_lady

New Member
May 2, 2024
3
8
Watanzania wengi tumekuwa na ndoto na malengo ya kutaka Tanzania yetu kuwa yenye maendeleo na vile tuitakayo, baada ya uhuru wa Tanzania mikakati mingi iliwekwa Ili kuletea maendeleo Kwa watanzania. Baba wa taifa mwalimu Julius K. Nyerere aliweka mikakati thabiti Ili kukuza maendeleo Kwa watu wote nchini na kutaka Kila mtanzania kufanya kazi Kwa bidii,kuwajibika na kujikomboa kiuchumi.

Tumekuwa tukijiuliza maswali mengi nini kifanyike Ili kufikia lengo?. Je utayari utakuwepo Kwa watanzania wote?. Ni mambo mengi yanahitajika kufanyika Kwa bidii na tuangalie njia zetu za awali tulizokosea na kuzirekebisha Kwa ufanisi zaidi.

Hivyo basi tunatakiwa kutatua matatizo au changamoto zilizokuwa tishio Kwa maendeleo ya Tanzania na kuleta mikakati thabiti pamoja na utekelezaji Ili kuhakikisha tunafika Kwa pamoja Tanzania tuitakayo. Haya ni matatizo na mipango kazi zitakazosaidia Kwa namna Moja au nyingne Ili kufikia malengo Kwa watanzania.

KUBORESHA MIFUMO YA ELIMU
Mifumo ya elimu ya zamani na ya Sasa imeboreshwa Kwa kiwango chake lakini haijafikia lengo thabiti kama nchi zingine. Hapa Si jambo tu la serikali hata wananchi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu Bora inapatikana Kwa watu wote. Miundombinu mashuleni inatakiwa kuboreshwa Ili isiwe vikwazo Kwa wanafunzi kupata elimu Bora na hata Kwa walimu itawajengea taswira nzuri katika kazi zao na kufanya utendaji wa kazi kuwa fanisihi na Kwa uweledi wa juu. Kingine ni kubadilisha mifumo ya zamani na kutengeneza mifumo mipya kutokana na mazingira ya nchi, hii itakuwa mgumu kueleweka.

Mfano; Katika mtaala wa historia imeenda Kwa upana zaidi jinsi ukoloni ulivyotawala katika miaka ya nyuma 1800's mpaka 1980's. Inabidi kubadilishwa na kuelezea ukoloni mambo Leo na vitu gani vya msingi vifanyike Ili kukuza historia ya Tanzania na kudumisha utamaduni wetu

Serikali inabidi kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba wanafunzi pamoja na walimu Kwa kuangalia kero na kupata ufumbuzi hata hivyo walimu wanatakiwa kulipwa vizuri kulingana na uchumi uliopo Sasa na sio kuwadidimiza chini hivyo italeta ufanisi zaidi katika kazi zao.

Kingine elimu ya Tanzania inatakiwa iwe ya vitendo sio ya kinadharia. Elimu inatakiwa kuhusisha nadhari zaidi Ili kufanya kueleweka Kwa urahisi zaidi. Mashuleni kumekuwa na changamoto nyingi haswa Kwa wanafunzi kuwa na uelewa mdogo kutokana na kufundishwa Kwa nadharia hivyo inaleta ufaulu mdogo haswa Kwa wanafunzi wanaosoma shule za kata.

Mfano; katika masomo ya kemia,fizikia na bailojia kumekuwa na uhaba wa vifaa ya maabara ambavyo vitakavyosaidia kukuza uelewa wa wanafunzi. Hata hivyo shule nyingi zinakuwa na uhaba wa maabara ya kujifunza unakuta maabara Moja inatumika Kwa masomo yote na pengine wingi wa wanafunzi na kuzuia wote kuelewa Kwa wakati.

KUKUZA NA KUTUMIA SAYANSI NA TEKNOLOGIA YA JUU
Nchi yetu ya Tanzania Bado hatujaendelea zaidi katika sayansi na teknologia tunapata changamoto Kwa Kasi sana hivyo inakwamisha maendeleo ya nchi. Katika nchi yoyote lazima iendelee teknologia yake,kupitia hivi kwanza tutakuza viwanda vyetu vya ndani mahitaji yetu Kwa ujumla na tutazalisha Kwa wingi hvo itapelekea kutengeneza bidhaa nyingi , kukuza soko letu la ndani na nje na kuanzisha viwanda vikubwa nchini na tutaacha kuwa tegemezi Kwa nchi za wenzetu.

Uwepo wa sayansi na teknologia itachangia Kwa Kasi zaidi maendeleo Kwa sababu watanzania tunataka kufikia nchi tuitakayo Kwa uwepo wa miundombinu mizuri na iliyoboreshwa kama barabara, reli za kisasa,hata viwanda vikubwa vya kisasa vitakavyoleta chachu ya uzalishaji mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo serikali ihamasishe zaidi Kwa wanafunzi kusomea masomo ya sayansi mashuleni.

UWEPO WA SIASA SAFI NCHINI
Ili kufikia lengo la Tanzania tuitakayo lazima kuboresha na uwepo wa siasa safi nchini. Siasa ni pana sana viongozi wa nchini wanatakiwa kuongoza Kwa uweledi na ufanisi zaidi na wakubali kujifunza Kila siku. Ningependa kufafanua zaidi kuhusu siasa kama ifuatavyo;

a) Tanzania kujikita zaidi katika kidemokrasia
Viongozi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao na kufuata misingi mizuri na kuongoza katika nguzo za kidemokrasia. Watanzania wanataka kueleza matatizo yao na zitatuliwe Kwa viongozi wa serikalini pia Ili kufikia nchi tuitakayo kuwepo na uhuru wa kuzungumza na kukosoa Yale yasiyo sahihi na kuleta mipango mizuri Ili kuboresha demokrasia. Viongozi inabidi wajue wao wamepewa talanta ya kuongoza katika njia iliyo sahihi na sio kudidimiza matakwa ya watanzania na waelewe wamechaguliwa na wananchi na kuitumikia nchi.

b) Uwajibikaji Kwa viongozi wa nchi
Viongozi wengi wamejisahau kuhusu wajibu wao kama viongozi nchini Kwa kutekeleza majukumu Yao Kwa kipindi wanachotawala. Hili ni lalamiko la watanzania wengi, wananchi wanataka mabadiliko na utekelezaji Kwa viongozi. Wengi wao wamejisahau kuhusu wajibu na majukumu Yao,kinachotakiwa kufanyika ni viongozi wa juu wanatakiwa kuhakikisha Kila kiongozi wa nchi anapaswa kutekeleza majukumu yake Kwa usahihi. Sheria inabidi itungwe na kufuatwa wa kiongozi yoyote kushindwa kufanya hivyo itambidi ajiudhulu au kushushwa cheo chake.

c)Kutungwa na kuboresha Katiba ya nchi
Watanzania wote tunahitaji kufika katika nchi tunayoitaka Kwa kuweka sheria Bora na madhubuti ya kuleta maendeleo na kuacha kushikilia sheria zenye kudidimisha wananchi. Siku zote nchi inaongozwa na katiba safi ambayo haididimizi watu wote Kwa ujumla. Inatakiwa kuwepo na misingi mizuri itakayoongoza nchi na hizo sheria zifuatwe bila ya kipingamizi Kwa wananchi na serikali Kwa pamoja. Hivo na ikumbukwe ya kuwa hakuna mtu yoyote aliye juu ya sheria iwe viongozi hakuna mwenye kuipinga Kwa sababu ya madaraka waliyokuwa nayo au kwa wananchi kuwadidimiza kupitia sheria. Tangu mwaka 1977 katiba ilitungwa na haijatungwa sheria nyngne zaidi ya sheria za mabadiliko za muda kwahiyo inabidi ipatikane sheria mpya ya kudumu katika nchi Ili kuleta maendeleo.

KUBORESHA MIUNDOMBINU NA KUTOA HUDUMA BORA ZA KIJAMII
Watanzania wanatarajia kuona maendeleo katika miundombinu bora mijini na vijijini Kwa kujenga barabara,reli za kisasa na zilizo bora Ili kurahisisha usafirishaji,pia kutengeneza na kuhakikisha Kila mtanzania anatumia miundombinu Kwa ubora bila kuharibu. Huduma bora za kijamii kama maji safi,umeme unapatikana vijijini na mijini, afya Bora na elimu Kwa Kila mtanzania. Serikali ihakikishe inasimamia ipasavyo huduma hizi zinatolewa Kwa watu wote nchini na kueleza changamoto zinazotokea kutowafikia haswa Kwa watu wa vijijini.

KUTOFUJA RASILIMALI ZA NCHI NA KUZITUMIA KWA WELEDI KWA MAENDELEO YA NCHI
Tanzania tumebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na za kuvutia ambazo zinakuza uchumi wa nchi Kwa kuingiza kipato kikubwa. Tumebarikiwa utajiri wa ardhi yenye rutuba,madini kama dhahabu,almasi na madini pekee yapatikanayo Tanzania ( Tanzanite), vivutio vya utalii, wanyamapori,gesi asilia. Hivyo basi rasilimali hizi zitumike vizuri Kwa uweledi na njia sahihi na kuhakikisha zinaleta mchango mkubwa Kwa kuleta maendeleo ya watanzania. Haitakiwi kufuja mali hizi na tuzuie nchi za ulaya zinachukua utajiri wetu Kwa manufaa Yao binafsi na sio ya watanzania. Yatupasa kutumia mbinu thabiti kama sheria Kali Kwa watu watakaoharibu rasilimali zetu na zitakazosaidia kulinda na kutunufaisha watanzania wote Ili kuleta maendeleo nchini.

Pia serikali inabidi kuweka mazingira mazuri ya biashara Kwa kuvutia wawekezaji nchini itachangia sana maendeleo Kwa kuongeza pato la nchi na watu watapata ajira Kwa wenye ujuzi na wasio nao. Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafika Tanzania tuitakayo Kwa kuungana Kwa pamoja na kuweka tofauti zetu kando na kuwa wazalendo Kwa kulipenda taifa letu. Kingine tusiruhusu wageni wachukue utajiri wa watanzania bali wawe chachu ya uwekezaji na pia tutatue changamoto zinazotukabili Kwa kupata njia sahihi ya utatuzi.

Tanzania tuitakayo tunaweza kuifikia tuungane Kwa pamoja na kushirikiana na kutimiza majukumu yetu kwaajili ya nchi yetu.

kilimanjaro-2.jpg

Chanzo Cha picha hii imepatikana Wikipedia
 
Tanzania tuitakayo tunaweza kuifikia tuungane Kwa pamoja na kushirikiana na kutimiza majukumu yetu kwaajili ya nchi yetu
Sawa sawa tupo pamoja.


. Baba wa taifa mwalimu Julius K. Nyerere aliweka mikakati thabiti Ili kukuza maendeleo Kwa watu wote nchini na kutaka Kila mtanzania kufanya kazi Kwa bidii,kuwajibika na kujikomboa kiuchumi.
Inaonekana umeielewa ki dhati nafasi ya kika mtu kujiletea maendeleo mmoja mmoja na kama Taifa.

Vizuri
 
Back
Top Bottom