TotalEnergies yaanza kuchimba Visima vya kuzalisha Mafuta ya Bomba la EACOP

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,482
8,334
Licha ya mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania kuendelea kupingwa na Watetezi wa Masuala ya Mazingira, uchimbaji wa Visima vya Mafuta Ghafi umeanza katika Hifadhi za Maporomoko ya Murchison.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU), Visima zaidi ya 400 vitachimbwa ili kupata Mafuta yanayohitajika. Pia, hadi sasa ni eneo moja tu la Mradi limefanyiwa kazi kati ya maeneo matatu yanayotarajiwa kukamilisha mradi.

Mradi huo unaojengwa kwa ushirikiano kati ya kampuni za Chinese National Offshore Oil Corporation (CNOOC) na TotalEnergies kwa takriban Tsh. Trilioni 24 katika eneo la Kilomita 1,445, unatarajiwa kuanza uzalishaji wa Mapipa 190,000 ya Mafuta kwa siku kuanzia mwaka 2025.


========

TotalEnergies begins drilling oil wells in Uganda's Murchison Falls National Park, despite pressure from rights and environmental organizations.

The $10 billion deal with the Chinese National Offshore Oil Corporation (CNOOC) aims to develop Ugandan oilfields and transport petroleum to Tanzania's port through a 1,445-kilometer pipeline.

Environmental groups raise concerns about the impact on the park and nearby communities, while TotalEnergies defends its use of sustainable technology and claims to have provided fair compensation to affected communities.

BUSINESS INSIDER
 
Back
Top Bottom