Sultan Tamba na Mussa Banzi Chukueni maua yenu japo bado tunawadai muendelezo wa baadhi ya filamu. Kanumba alichangia kuua soko la filamu

Andiko zuri sana lakini usibeze mchango na jitihada za Kanumba kwenye tasnia ya filamu Tanzania.

Sijui nini kilikuja kuharibu hapo kati kati, lakini zamani pamoja na uduni wa vifaa vya kisasa ila unaangalia movie unaridhika kabisa.

Muziki umekuwa wa hovyo, filamu ndio usiseme hadi Mwijaku na Chris Mitindo wanaigiza, miaka iko mbio sana kweli kweli.
Mwijaku alianzia huko
 
Sultan Tamba na kundi lake la Tamba Arts group ambapo humo ndani unakutana na waigizaji kama Riyama Ally, Mwajabu Kazimili (Bi Nyamisi),Rehema Msangule (Doreen Nsyuka),Sanjo,Ringo,Chilisosi, nk

Mussa Banzi na kundi lake la White Elephant waigizaji wake kama vile Ramadhan Ally (Main character kwenye sijui la kufa, My Darling nk,Evans Moshi (Mack wa shumileta),Jenifer Kyaka (Odama), Jenifer Mwaipaja (Shumileta) ,mganga ndele nk.

Japo kuna waigizaji walikuwa wanaigiza huku na huku yani kwa Sultan Tamba na kwa Mussa Banzi na kuna wale ambao wapo either kwa Sultan Tamba au kwa Mussa Banzi.

Tuendelee,

Kifupi hawa jamaa ndio walioleta mapinduzi kwenye suala zima la filamu na filamu zao kwa kiasi kikubwa yaliakisi maisha halisi ya mtanzania .

Sultan Tamba alikuwa bingwa zaidi kwenye filamu za kutisha kuliko filamu za kawaida ,mfn filamu kama Nsyuka, Roho mbili, Mama Yangu anakula nyama za watu, Mzee wa busara, Chite Ukae,Sanda nyeusi ,Tabana, Jinamizi , Mume bwege,Girlfriend Nk

  1. Mussa Banzi alikuwa yupo vizuri zaidi kwenye filamu za mapenzi kuliko filamu za kutisha mfano Cindy na Candy, Dear Doctor,Shenaiza, Sikio la kufa ,My Darling,The game of love, Odama, Veronica, Zogo kisiwa Cha mauti, Kihongwe, Kinyamkela,Karibu paradiso,Joanita nk

Filamu tunazowadai muendelezo wake kwa hamu

1)Chite Ukae -Iliishia part one na walituahidi kuleta muendelezo wake ila mpaka leo kimya.

Hii ni miongoni mwa filamu zenye uchawi wa hali ya juu , tunamuona mwanadada Doreen nsyuka(Rehema Msangule) akipitia misukosuko mingi ya kichawi na akawa ametembea vilinge vingi ila jibu alilopewa ni Moja tu inabidi afariki kwa muda wa siku 3 kisha atafufuka upya kwa njia za kichawi/kiganga.

Misukosuko huu aliupata pia kwenye filamu ya Nsyuka part 2,Doreen alifariki ili Nsyuka atulizwe akaja kufufuka siku ya tatu wakati gari lipo njiani linaelekea makaburini.

2)Kihongwe (Nguvu za Giza)- Hii filamu ilikuwa nayo inasisimua sana, tunamuona muigizaji Ibrahimu Mbwana (bad boy fighter)(Desmond) kama mtu tajiri sana,sasa rafiki wa mke wake anaitwa Nolinda akaingilia penzini ili amtapeli Desmond Mali zake na hizo Mali Nolinda akatumie na mwanaume mwengine anayempenda kwa dhati.

Kwa njia za kawaida Nolinda alifanikiwa tu kumchuma pesa za kawaida ila akawa haridhiki anataka apate mpaka nyumba na magari ila ikashindikana ndipo akahamia kwenye upande wa nguvu za giza ,huko napo akakwama mara mbili kwa kukosea masharti ya mganga ndele, njia ya mwisho aliyopewa ni kuchukua kivuli Cha Desmond kifukiwe makaburini kwa siku 7 kisha kifukuliwe na kutunzwa kwenye jeneza ambalo atakuwa anakaa nalo Nolinda siku zote ,akitaka chochote anaenda kwenye huo mawili anauongelesha na Desmond mzima anatimiza.

Kwa hiyo kilichofanyika, ilichukuliwa bastola ikafanyiwa mambo ya kishirikina kisha Nolinda akaenda kumuulia nayo Desmond ,ikapatikana miili miwili (mmoja kama kivuli) , huo mawili kivuli ndio uliozikwa kwa siku saba na kufufuliwa .

Nolinda alifanikiwa kumtapeli parefu Desmond kishirikina alijengewa nyumba, na mpenzi wake naye akajengewa nyumba na Desmond akimdanganya ni kaka yake amepata matatizo ya kudhulumiwa nyumba na hana pa kuishi hivyo akamuomba amnunulie nyumba Desmond akafanya hivyo.

Mwisho wa filamu tunaona Desmond anapata ajali ya kweli na anakufa kifo cha kweli baada ya kupewa laana na mama yake baada ya kumfukuza mama yake mzazi na mkewe wa ndoa.

Lakini tuliambiwa kutakuwa na muendelezo wa Kihongwe sehemu ya 2 mpaka leo kimya.

3)Shumileta sehemu ya 3.

Tunaona Evance Mushi (Mack) anafanikiwa kurudi duniani baada ya kutokea vita kubwa huko ujinini kati ya Shumileta na mdogo wake wakimgambania Mack.

Tunataka tuone muendelezo utakuaje baada ya hapo maana tuliahidiwa muendelezo, wale makini hawakufungwa na Mack haikuwa na Kinga yoyote ya kutoendelea kusumbuliwa na hao majini ,sasa je nini kitaendelea baada ya hapo na uzuri Main Characters wote wapo hai mpaka leo .

Filamu zingine zilizohitaji muendelezo ni Kinyamkela ,Tabana ,Zogo kisiwa Cha mauti nk.


Tuendelee.

Mbali na Musa na Sultan Tamba
, mwingine aliyejitahidi tahidi alikuwa Jumanne Kihangala(Tuesday Kihangala) na alipata umaarufu zaidi na tamthilia ya jumba la dhahabu, amewapika wengi kupitia kundi lake la fukuto,kama vile Miriam Jolwa(Jini Kabula),Jackline Pentzel,Baga Mteme,Kitale,Nikita,nk

Tuendelee

Baada ya hawa jamaa kutamba kwa muda mrefu ujio wa Steven Kanumba ukaja kuharibu filamu za bongo kwa kiasi kikubwa na akajitengenezea mazingira ya yeye peke yake kung'aa.

Makosa ya Kanumba yalikuwa ni haya .

  • Kutuletea waigizaji kwa kuangalia urafiki uliopo baina yao bila kujali kipaji alichonacho.Kanumba alikuwa mtu wa kuokota okota akikuona upo smart na kuna filamu anataka kutoa anakuita ukaigize hata kama huna kipaji anakwambia utajulia huko huko .Na hili baadhi ya waigizaji waliwahi kulisema mfano Jackline Wolper ,Wema Sepetu,Kenny,Hao akina Hemed ,Mlela nk.
  • Zamani waigizaji wengi walilelewa na kupikwa kwenye vikundi /makundi ya Sanaa lakini yeye kwa Kanumba ilikuwa tofauti anakubeba tu ukaigize ukiwa na muonekano mzuri automatically utapendwa tu hata usipojua kuigiza.
  • Kanumba ndiye muanzilishi wa filamu ambazo zinakosa uhalisia mfano white maria, magic house nk
  • Kanumba ndiye aliyeanza kuharibu filamu za bongo kwa kulazimisha kila filamu iwe na part one na part two hata kama ni filamu ya saa Moja kitu ambacho zamani hakikuwepo,Zamani ukiona filamu ina part one na two basi ujue ina deserve maana filamu nyingi za zamani zilikuwa zinachukua si chini ya saa moja na nusu kwa filamu moja.Na ukiona kuna muendelezo wa part two basi lazima muisubiri kwa hamu tofauti na kipindi cha Kanumba.
  • Kilichombeba Kanumba enzi zake ni kule kujipendekeza pendekeza kwa wanaigeria kuomba collabo kinyume na hapo kawaida tu nk.


Itaendelea

Umetukumbusha kitambo sanaaa
 
Tuesday Kihangala alikuja baada ya Kanumba. Jumba la dhahabu inachezwa tayari Kanumba ni staa mkubwa tangu 2002 kama sikosei. Kwamba Kanumba ndo aliharibu bongo Movie ni kauli ya kupuuzwa. Kanumba ndo alileta mapinduzi makubwa kwenye filamu hadi nje ya mipaka alishaanza kupenya. Akili zake zilikuwa kama Diamond kwenye muziki. Hao kina Musa Banzi huenda walikuwa wana vipaji ila hawakuwa na vipaji vya biashara.
Duh! Kanumba wa juzi tu hapa ambaye kamkuta kwenye game hata Lulu (Elizabeth Michael) ndiyo amtangulie Kihangala?

Sijui kama unafahamu kama Kihangala alianzia Kaole ya Chris Mhenga kabla ya kuanzisha kundi lake la Fukuto na akina Ndende.

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom