Kuna sababu nyingi zinazopelekea kuta zinazounda kona kupata nyufa katika maungio na ili ujue sababu ya kutokea hiyo nyufa ni vizuri mtaalam akafika eneo la site akakagua vizuri.View attachment 2977303
Hii kuchanika kwenye kona shida ni nini? ubora wa tofari au mvutano wa kuta?
Ni Njia nzuri sana hii ila aisee maji yakiwa mengi sana taratiiibu yanakula udongo unaoegemewa/shika hizo gabions na mwishowe taritiiibu zinaporomoka zenyewe dah nimeshuhudia hii sehemu nyingi sana. Kama mtu bado ana nguvu za fedha hata kama ni kidogo ni heri akatafuta eneo jingine zuri la kuishi.Wale ndugu zangu ambao makazi yenu yapo pembezoni mwa mto, njia pekee ya kukabiliana na hayo maji yasiweze kuathiri makazi yenu ambayo ni ya uhakika ni kutumia Gabions.
Gabions ni yale mawe meusi ambayo huwa yanapangwa pembezoni mwa mto, yanafungwa na wavu ambao haupati kutu (galvanized). Mawe meusi ni mazuri zaidi kwa sababu yenyewe hayafyonzi maji kama ilivyo kwa mawe mengine
Wanakosea namna ya kuziweka, mawe inatakiwa yapangwe katika namna ambayo mtu akitaka kuingia mtoni awe anashuka kama anavyochuka kwenye ngazi. Chunguza hata kwenye madaraja makubwa, utaona njia hii ndio inayotumika sana, kabla ya kupanga hayo mawe chini huwa inatangulia zege (nitawaletea picha baadae)Ni Njia nzuri sana hii ila aisee maji yakiwa mengi sana taratiiibu yanakula udongo unaoegemewa/shika hizo gabions na mwishowe taritiiibu zinaporomoka zenyewe dah nimeshuhudia hii sehemu nyingi sana. Kama mtu bado ana nguvu za fedha hata kama ni kidogo ni heri akatafuta eneo jingine zuri la kuishi.
ok sawa mtaalamu shukraniWanakosea namna ya kuziweka, mawe inatakiwa yapangwe katika namna ambayo mtu akitaka kuingia mtoni awe anashuka kama anavyochuka kwenye ngazi. Chunguza hata kwenye madaraja makubwa, utaona njia hii ndio inayotumika sana, kabla ya kupanga hayo mawe chini huwa inatangulia zege (nitawaletea picha baadae)
weka mawasiliano na gharama zako zipojePlaster nzuri ni ile ambayo ukimwagia ukuta maji, ukuta unakauka bila kuchora alama za matofali. Kiujumla michoro ya tofali katika ukuta uliopigwa plaster hutokea pale ratio ya udongo uliotumika kujengea tofali ni kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kupigia plaster
Kitaalam udongo wa kujengea tofali tunatumia ratio ya 1:6 na udongo wa kupigia plaster tunatumia ratio ya 1:4 na 1:5 (ratio ya 1:4 inatumika kwenye kuta upande wa nje, na 1:5 upande wa ndani)
Ratio ya plaster inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kujengea
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Kulaza ama kusimamisha tofali inategemea na jengo lilidesigniwa namna gani (framed structure ama load bearing structure). Mfano yale majengo ya mjini ambayo unaona wanajenga tu nguzo,mkanda,slab, nguzo,mkanda,slab mpaka juu (ghorofa ya mwisho) yale uzito wake unabebwa na lile lifrem la zege unaloliona na kupelekwa moja kwa moja ardhini (slab>beam>column>footing>soil) hivyo kuta zake zote hazihusiki katika ubebaji wa mzigo badala yake zinakuwa na kazi ya kuziba tu uwazi au kufanya partition na ndio maana utaona tofali zake zinasimamishwa kuanzia floor ya kwanza mpaka mwisho na huwa zinajengwa mwishoni baada ya hilo lifrem kukamilikaHechy Essy
Kuhusu kulaza au kusimamisha matofali kwenye ujenzi wa nyumba ya kawaida ghorofa 1 kipi ni sahihi?
Maana kuna wanaosema kuwa ukitumia nondo 4 za mm16 kwenye nguzo tofali unaweza kusimamisha na wala hamna shida.
Then kuna wanasema ukitumia nondo 6 za mm12 basi tofali ndo utazilaza, na wakati huohuo bado kuna wanaotumia nondo hizo 6 za mm 12 na bado tofali zinasimamishwa.
Nimeona ujenzi wa nyumba Uganda, Nigeria, Kenya mara nyingi tofali hawalazi tena basi za kwao ni hollow blocks, sasa najuliza kipi ni sahihi kiutaalamu.
Then kwa sasa kuna ujenzi ule wa pre casted slab ambapo unakuta kwenye slab wanapanga tu hollow blocks, then kuna mapande marefu ya zege wanayapanga, then kuna wire mesh inatandikwa au wanaweka tu kichanja cha nondo chache then wanamwaga zege, najiuliza ujenzi huo ni sahihi?
Niseme yoyote kwa yote binafsi naamini/nahisi ujenzi huo wooote nilioutaja hapo juu nia yao ni kupunguza gharama sasa je huo ujenzi kiutaalam ni sahihi au ndo baada ya miaka kadhaa kupita tutegemee majanga?
+255(0)624068809 tuwasiliane ndgweka mawasiliano na gharama zako zipoje
Shukrani Eng. kwa kushare utaalamu wako kwa hiyo inawezekana jengo let say residential G+1 kufanyiwa design kuwa nondo za 12mmm ndo zitumike kwenye nguzo badala ya 16mm?Kulaza ama kusimamisha tofali inategemea na jengo lilidesigniwa namna gani (framed structure ama load bearing structure). Mfano yale majengo ya mjini ambayo unaona wanajenga tu nguzo,mkanda,slab, nguzo,mkanda,slab mpaka juu (ghorofa ya mwisho) yale uzito wake unabebwa na lile lifrem la zege unaloliona na kupelekwa moja kwa moja ardhini (slab>beam>column>footing>soil) hivyo kuta zake zote hazihusiki katika ubebaji wa mzigo badala yake zinakuwa na kazi ya kuziba tu uwazi au kufanya partition na ndio maana utaona tofali zake zinasimamishwa kuanzia floor ya kwanza mpaka mwisho na huwa zinajengwa mwishoni baada ya hilo lifrem kukamilika
Kwa hizi ghorofa za kawaida, mfumo wake wa ujenzi unafanya kuta nazo zihusike katika ubebaji wa mzigo ndio maana tofali zake zinalazwa (zege ya beam inamwagwa juu ya ukuta tofauti na ilivyo kwenye framed structure ambapo zege inakuwa supported na formwork na baada ya kufikia ukomavu kiasi flan, formwork inatolewa)
Kama jengo litakuwa limefanyiwa design ambayo kuta zake zitakuwa hazihusiki katika ubebaji wa mzigo basi hata ukisimamisha tofali inakuwa haina shida, lakini kama design ilikusudia kuta ziwe zinabeba mzigo halafu wewe ukawa umesimamisha hizo tofali maana yake kuna uwezekano mkubwa hizo kuta zikashindwa kubeba huo mzigo uliokusudiwa.
Inategemea na kiasi cha uzito utakaobebwa na nguzo, lakini yote kwa yote nguzo ni vizuri minimum size ya nondo ikaanzia 16mm japo kuwa mahesabu yanaweza yakaifanya nondo ya 12mm nayo ikapass kutokana na ushirikiano wa kuta na nguzo katika ubebaji wa mzigoShukrani Eng. kwa kushare utaalamu wako kwa hiyo inawezekana jengo let say residential G+1 kufanyiwa design kuwa nondo za 12mmm ndo zitumike kwenye nguzo badala ya 16mm?
Tafadhali jibu swali la aliyekuuliza. Jibu lako litatusaidia hata sisi tunaotarajia kujenga karibuni.Mimi huwa namjibu mtu kulingana na namna alivyouliza...kwani wangapi huko juu wameuliza maswali kwa lengo la kutaka kujua na nimewajibu tu vizuri? Mtu anayeuliza kwa lengo la kutaka kujua anauliza namna hiyo? We umekuja kwa lengo la kubishana, kwamba uonekane we ni mjuzi zaidi kuliko wengine. Endelea tu na nyuzi zako bro, mimi nipo hapa kibiashara sijaja kubishana na watu, atakayeuliza kistaarabu nitamjibu kistaarabu pia (mimi ni mtu mmoja peace sana, sipendagi kujibizana na watu kwa sababu ambazo hazina msingi)