Rafiki mpenzi amenigeuka, amekuwa adui yangu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,687
12,030
Huyu rafiki tulipoteana kwa muda mrefu kidogo. Tulianza fahamiana chuo. Tukamaliza tukaja kutana tena mkoa flani kazini, tukaendelea kuwa marafiki. Baadaye tukatengana tena.

Tukaja kutana tena hapa town baada ya yeye kunitafuta. Kumbe alikuwa anakaribia kuolewa. So akawa anataka mchango wa send off. Bahati mbaya ilikuwa kipindi ambacho nina mgonjwa amelazwa miezi kadhaa namhudumia.

Nilimjulisha hilo kabla hata hajaniambia habari zake za send off. Nlichosikitika. Hakuwahi niuliza mgonjwa anaendeleaje, ila aliendelea tu kutuma msgs zake za kukumbusha mchango.

Baadaye akafanya sherehe zake. Akamaliza na since then hakuwahi nitafuta tena. Hakuwahi kutaka kujua mgonjwa ameendeleaje. Hata mgonjwa alipofariki hakuwahi niambia pole. I lost her like that
 
Kuna watu hukukumbuka wakati wa shida zao, hivyo lazima utambue Hilo na uwe makini usije ukatumika kwenye mambo Yao kamwe usikubali hili, uzuri ni kwamba hakuzidishii au kukupunguzia kitu.
 
Kma umetendewa yote hayo alafu Bado unakuja kulia lia humu hta Mimi ningekupunguza kwenye maisha yang mkuu
 
Sijaona uadui umeingiaje hapo, yeye malengo yake ilikuwa mchango na alikwambia..... wewe malengo yako ni yapi na ulimwambia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom