Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Mkuu ninaomba kufahamu baadhi ya vitu kwako, ni kwamba una karasha then una mtaji wako je hyo miamba unayopima unachimba mwenyewe na je duara lako Lina urefu gani? Na je vip maduara ya jirani na wewe yanatoaje pia je unapiga tu na kumwaga rundo au Kuna Wakati huwa unachenjuwa kwa mercury? Kwenye upimaji wa ppm na kusoma juu halafu mwisho kusoma chini Kuna sababu nyingi lazima nijue je mawe yako unayatoa yote sehemu moja tu au unakuwa unachanganya changanya ? Pamoja na kwamba una pima ppm ila jitahid sana kufanya bottle test ama kupima black ya udongo wako itakusaidi pia kujua kama udongo wako unasoma juuu au chini, yaani usije kuridhika eti ppm inasoma 8 ukajua ndo Iko ivo kote , unaweza kufanya bottle test plant ukakuta uhalisia wa ppm ni 4 au 2, nipo tayari pia kusikia na kupokea mawazo mapya kutoka kwa wadau wengine
Duara ni langu pia, duara la jirani linatoa vizuri tu,
Ukitumia Mercury unapata kidogo pia, ila kuna wengine wanatoa vizuri tu
 
Wanajamvi

Leo nimekuja, mwenzenu yamenifika shingoni

Nina miaka mitatu tangu nimeingi kwenye uchimbaji wa madini huku chunya mbeya,

Nimamiliki karasha, nimeshapoteza zaidi ya milioni 40 katika shughuli hii.

Huwa nnajitahidi kupima miamba kila hatua kama inavyoshauriwa lkn matokeo mara zote huwa kinyume na matarajio,

Mfano unaweza kupima mwamba ukaambiwa ni wastani wa ppm 8 lkn unachokuja kukipata ni wastani wa ppm 1

Wadau wengi hawataki kutoa siri ya wapi wanapitia ili kuhakikisha kile wanachotakiwa kukipata wanakipata,

Tafadhali sana, mwenye kujua namna nnaweza kupata msaada wa kweli tafadhali msaada hapo PM
Badilisha biashara nitafute ni kupe biashara isiyopasua kichwa ni ukweli na uta re lux
 
Duara ni langu pia, duara la jirani linatoa vizuri tu,
Ukitumia Mercury unapata kidogo pia, ila kuna wengine wanatoa vizuri tu
Basi usikate tamaaa mkuu fanya kazi Mimi nilianza mwezi wa 7 mwaka Jana urefu wa duara ulikuwa ni kama futi 60 ila matunda ya kazi nimekuja kuyaona mwezi wa 3 mwaka huu hata Mimi ppm yangu ilikuwa inabadilika saana kila mara ila nlikuwa ninapima kweny lab zaidi ya 2 na Bado nafanya bottle test plant kujua mabadiliko ya mwamba ni vizuri pia ujue kama Kuna madini mengine eneo Hilo yanayoweza kukuletea matokeo tofauti Kwako jitahid saana usage main lifu tu, mkuu achana na felo za akina mama kbsa
 
Wanajamvi

Leo nimekuja, mwenzenu yamenifika shingoni

Nina miaka mitatu tangu nimeingi kwenye uchimbaji wa madini huku chunya mbeya,

Nimamiliki karasha, nimeshapoteza zaidi ya milioni 40 katika shughuli hii.

Huwa nnajitahidi kupima miamba kila hatua kama inavyoshauriwa lkn matokeo mara zote huwa kinyume na matarajio,

Mfano unaweza kupima mwamba ukaambiwa ni wastani wa ppm 8 lkn unachokuja kukipata ni wastani wa ppm 1

Wadau wengi hawataki kutoa siri ya wapi wanapitia ili kuhakikisha kile wanachotakiwa kukipata wanakipata,

Tafadhali sana, mwenye kujua namna nnaweza kupata msaada wa kweli tafadhali msaada hapo PM
Mkuu hapo chunya sehemu gani maana mm nipo huku saza, mkwajuni naona watu wana piga noti tu.
 
Sawa mkuu, wewe unajua zaidi
Hapana mkuu, wala haihitaji elimu ya chuo kikuu kutambua kuwa waganga wanatuibia Tu.

Cha msingi ilikuwa wachimbaji kuungana na kukusanya mtaji utakaowawezesha kununua vifaa vya kisasa na teknolojia nzuri ya namna ya Ku locate madini yalipo na kiwango , au kuiomba Serikali kuwawezesha wachimbaji wazawa mitambo ya kisasa ya uchimbaji, muache kuchimba kwa kubahatisha na kupelekea kupoteza pesa zenu na mitaji.

Hivi mnaona hao wawekezaji wanapokuja kuchimba madini huku kwetu wanategemea waganga wa kienyeji kwenye uwekezaji wao wa mabilioni?

Hakuna uchawi katika sekta ya madini, wekeza vifaa na mitambo muhimu, teknolojia na wataalamu. Period
 
Ungekomaa na Karasha au mobile compressor na kukodisha vifaa tu kwenye hayo maeneo ungepiga hela huku taratibu unaisoma game hasa kwa kuingia share ukitumia vifaa vyako na sio kuweka cash yako kutoka mfukoni.
Mfano - unachoronga mahala kwa share unasepa zako, unachukua share mahala wanaposuasua lakini ulishausoma mchezo hawako mbali na mwamba Bali mpunga tu umekata, we hapo unaingiza submisible na compressor nk.

Uchimbaji unataka watu wenye roho ngumu wasioogopa kuchanjwa hata chale matakoni, hapa nazungumzia kuendesha duara from scratch ukifukuzia mwamba, kama sio mwamba unaweza kupoteza hata billions kadhaa.
 
Basi usikate tamaaa mkuu fanya kazi Mimi nilianza mwezi wa 7 mwaka Jana urefu wa duara ulikuwa ni kama futi 60 ila matunda ya kazi nimekuja kuyaona mwezi wa 3 mwaka huu hata Mimi ppm yangu ilikuwa inabadilika saana kila mara ila nlikuwa ninapima kweny lab zaidi ya 2 na Bado nafanya bottle test plant kujua mabadiliko ya mwamba ni vizuri pia ujue kama Kuna madini mengine eneo Hilo yanayoweza kukuletea matokeo tofauti Kwako jitahid saana usage main lifu tu, mkuu achana na felo za akina mama kbsa
Ni kweli mkuu, kawaida huwa tunapeleka maabara kila baada ya koleo 3 au chini ya hapo kama pesa inakuwepo.

lkn je kuna namna nyingine unafanya tofauti na hiyo?
 
Ungekomaa na Karasha au mobile compressor na kukodisha vifaa tu kwenye hayo maeneo ungepiga hela huku taratibu unaisoma game hasa kwa kuingia share ukitumia vifaa vyako na sio kuweka cash yako kutoka mfukoni.
Mfano - unachoronga mahala kwa share unasepa zako, unachukua share mahala wanaposuasua lakini ulishausoma mchezo hawako mbali na mwamba Bali mpunga tu umekata, we hapo unaingiza submisible na compressor nk.

Uchimbaji unataka watu wenye roho ngumu wasioogopa kuchanjwa hata chale matakoni, hapa nazungumzia kuendesha duara from scratch ukifukuzia mwamba, kama sio mwamba unaweza kupoteza hata billions kadhaa.
Mkuu kuchoronga kwa elfu 50 si unapata hela ya kula tu, hizo njia zote utapata hela ya kula lakini kusema kwamba utapata hela ya maana ukirudi nyumbani watoto waseme baba karudi sio rahisi

Tupeni mbinu mnazotumia kutoboa na sisi tutoke
 
Hapana mkuu, wala haihitaji elimu ya chuo kikuu kutambua kuwa waganga wanatuibia Tu.

Cha msingi ilikuwa wachimbaji kuungana na kukusanya mtaji utakaowawezesha kununua vifaa vya kisasa na teknolojia nzuri ya namna ya Ku locate madini yalipo na kiwango , au kuiomba Serikali kuwawezesha wachimbaji wazawa mitambo ya kisasa ya uchimbaji, muache kuchimba kwa kubahatisha na kupelekea kupoteza pesa zenu na mitaji.

Hivi mnaona hao wawekezaji wanapokuja kuchimba madini huku kwetu wanategemea waganga wa kienyeji kwenye uwekezaji wao wa mabilioni?

Hakuna uchawi katika sekta ya madini, wekeza vifaa na mitambo muhimu, teknolojia na wataalamu. Period
Kuna mgodi mkubwa wa wachina uko Makongorosi , mara kwa mara huwa wanachinja mbuzi wanaweka kwenye vizimba vyao wanachoma na madawa madawa,

Anyway, idea yako ni nzuri unaonaje ukiifanyia kazi huoni kama utapiga hela?
 
Ni kweli mkuu, kawaida huwa tunapeleka maabara kila baada ya koleo 3 au chini ya hapo kama pesa inakuwepo.

lkn je kuna namna nyingine unafanya tofauti na hiyo?
Mkuu unachopeleka ni unga au jiwe yaani mwamba kama wamba cjui huko mnafanje maana nimeona pia geita watu wanafanya tofauti ila Mimi kama Mimi mara nyingi huwa sipendi kupima mwamba yaani jiwe ila lazima nizalishe mawe then niyasage yaani ile bila kusoti mizunguko miwili au mitatu then unga nitaugawa mmoja watapitisha kwenye ule mtambo halafu na mwingine mkavu ndo napima lab, yaani jumla nakuwa na sample nne ili niwe na uhakika zaidi sipendelei saana kupima tu jiwe yaani eti mwamba
 
Tunatumia sampla kabla ya kuosha na baada ya kuosha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom