Nataka kufungua Kiwanda cha Peanut Butter, naombeni uzoefu!

africatuni

Member
Nov 13, 2023
60
111
Habari zenu wana jamvi. Hope this thread finds you well.

Bila kupoteza muda, naomba niruke kwenye mada moja kwa moja.. ninaomba uzoefu katika nyanja tofauti tofauti za uendeshaji wa kiwanda cha peanut butter,
Kama vile upatikanaji wa Mashine bora na bei zake. Changamoto?? Masoko?? n.k

Nipo dodoma, bila shaka mnafahamu kua karanga ni zao kuu huku kwetu... Kwa hivyo mpango nilionao ni kulima karanga na kuziuza kwa final consumer kama peanut butter.

Nakaribisha maoni, ushauri, uzoefu.. feel free to crush me down!!
possible-g9c5c021f1_1920.jpg
 
Nina mashine nzuri sana heavy duty ya peanut butter,imetumika mwezi mmoja tu nilinunua milioni Moja nitakupa kwa laki sita
 
Habari zenu wana jamvi. Hope this thread finds you well.

Bila kupoteza muda, naomba niruke kwenye mada moja kwa moja.. ninaomba uzoefu katika nyanja tofauti tofauti za uendeshaji wa kiwanda cha peanut butter,
Kama vile upatikanaji wa Mashine bora na bei zake. Changamoto?? Masoko?? n.k

Nipo dodoma, bila shaka mnafahamu kua karanga ni zao kuu huku kwetu... Kwa hivyo mpango nilionao ni kulima karanga na kuziuza kwa final consumer kama peanut butter.

Nakaribisha maoni, ushauri, uzoefu.. feel free to crush me down!!View attachment 2988986
Ukitaka mashine ya kukaanga karanga, ya kusaga na mashine za packing ndogo niambie. Ya kukaanga sijawahi kuitumua, ya kusaga nimeitumua kidogo ina motor ya 1.5 horsepower na mengine. Nimefanya fanya hii kitu nilikuwa natengeneza peanut ya kawaida na yenye ladha ya chocolate. Sema kutokana na sababu kadhaa nilishindwa kutoboa kwenye soko nikaacha
 
Nina mashine nzuri sana heavy duty ya peanut butter,imetumika mwezi mmoja tu nilinunua milioni Moja nitakupa kwa laki sita
Nadhani mleta uzi ungeanza mazungumzo na huyu bwana. Sababu anayo mashine unayoitaka.
 
Ukitaka mashine ya kukaanga karanga, ya kusaka na mashine za packing ndogo niambie. Ya kukaanga sijawahi kuitumua, ya kusaka nimeitumua kidogo ina motor ya 1.5 horsepower na mengine. Nimefanya fanya hii kitu nilikuwa natengeneza peanut ya kawaida na yenye ladha ya chocolate. Sema kutokana na sababu kadhaa nilishindwa kutoboa kwenye soko nikaacha
Usingeacha shida ni nini sasa? Mimi napenda sana siagi ya karanga lakini product yako sijui kama nilishawahi kuitumia.

Kuna ndugu yangu kwake anatumia sana siagi ya karanga, kwenye kupikia mboga, uji wa mtoto, na yeye huwa anatia sana kwenye mikate na kuitumia kama siagi. Ukienda kwake vile vikopo vyeupe vya nusu lita vimejaa utadhani huwa anaviokota kumbe huwa ananunua na kutumia siagi ya karanga.
 
Nadhani muda pia mkuu. Maana nilichukua hadi tbs, nikawa na kakiwanda kadogo. Nikafanya branding. Shida inahitaji uwe na stock ya karanga maana msimu wa karanga karanga zinashuka ikifika msimu karanga zinakuwa adimu zinapanda lakini bei ya kopo la peanut inabaki kuwa vile vile hapo kama huna stock utatengeneza hasara. Sema throughout the journey nilijua kuwa si kila karanga inafaa kwa peanut kuna kaanga kwa ajili ya peanut na karanga ambazo hazifai.
Ningekomaa ningetoboa sema mambo yalikuwa mengi nikasitisha toka mwaka juzi. Mwaka jana nikanunua mashine ya kukaanga nikiwa na wazo la kuja kuendelea ila sijioni nikifanya hivyo. Nilikuwa na partner na rafk yangu naona naye kwa sasa ana mambo meng tulikuaw 50/50 share
 
Kati ya zile karanga nyekundu flani kubwa kubwa na hizi za kawaida za dodoma zipi zinafaa zaidi, nataka nijaribu kutengeneza kwa matumizi ya nyumbani tu lakini ziwe nzuri
 
Nadhani muda pia mkuu. Maana nilichukua hadi tbs, nikawa na kakiwanda kadogo. Nikafanya branding. Shida inahitaji uwe na stock ya karanga maana msimu wa karanga karanga zinashuka ikifika msimu karanga zinakuwa adimu zinapanda lakini bei ya kopo la peanut inabaki kuwa vile vile hapo kama huna stock utatengeneza hasara. Sema throughout the journey nilijua kuwa si kila karanga inafaa kwa peanut kuna kaanga kwa ajili ya peanut na karanga ambazo hazifai.
Ningekomaa ningetoboa sema mambo yalikuwa mengi nikasitisha toka mwaka juzi. Mwaka jana nikanunua mashine ya kukaanga nikiwa na wazo la kuja kuendelea ila sijioni nikifanya hivyo. Nilikuwa na partner na rafk yangu naona naye kwa sasa ana mambo meng tulikuaw 50/50 share
Hiyo mashine ya kukaanga karanga inapatikana wapi na kwa bei gani na inatumia nishati gani mkuu?
 
Nadhani muda pia mkuu. Maana nilichukua hadi tbs, nikawa na kakiwanda kadogo. Nikafanya branding. Shida inahitaji uwe na stock ya karanga maana msimu wa karanga karanga zinashuka ikifika msimu karanga zinakuwa adimu zinapanda lakini bei ya kopo la peanut inabaki kuwa vile vile hapo kama huna stock utatengeneza hasara. Sema throughout the journey nilijua kuwa si kila karanga inafaa kwa peanut kuna kaanga kwa ajili ya peanut na karanga ambazo hazifai.
Ningekomaa ningetoboa sema mambo yalikuwa mengi nikasitisha toka mwaka juzi. Mwaka jana nikanunua mashine ya kukaanga nikiwa na wazo la kuja kuendelea ila sijioni nikifanya hivyo. Nilikuwa na partner na rafk yangu naona naye kwa sasa ana mambo meng tulikuaw 50/50 share
Ulikata tamaa mapema ila ulikuwa ndio unaelekea kutoboa.
 
Habari zenu wana jamvi. Hope this thread finds you well.

Bila kupoteza muda, naomba niruke kwenye mada moja kwa moja.. ninaomba uzoefu katika nyanja tofauti tofauti za uendeshaji wa kiwanda cha peanut butter,
Kama vile upatikanaji wa Mashine bora na bei zake. Changamoto?? Masoko?? n.k

Nipo dodoma, bila shaka mnafahamu kua karanga ni zao kuu huku kwetu... Kwa hivyo mpango nilionao ni kulima karanga na kuziuza kwa final consumer kama peanut butter.

Nakaribisha maoni, ushauri, uzoefu.. feel free to crush me down!!View attachment 2988986
soko lipo kazana na branding
 
Nadhani muda pia mkuu. Maana nilichukua hadi tbs, nikawa na kakiwanda kadogo. Nikafanya branding. Shida inahitaji uwe na stock ya karanga maana msimu wa karanga karanga zinashuka ikifika msimu karanga zinakuwa adimu zinapanda lakini bei ya kopo la peanut inabaki kuwa vile vile hapo kama huna stock utatengeneza hasara. Sema throughout the journey nilijua kuwa si kila karanga inafaa kwa peanut kuna kaanga kwa ajili ya peanut na karanga ambazo hazifai.
Ningekomaa ningetoboa sema mambo yalikuwa mengi nikasitisha toka mwaka juzi. Mwaka jana nikanunua mashine ya kukaanga nikiwa na wazo la kuja kuendelea ila sijioni nikifanya hivyo. Nilikuwa na partner na rafk yangu naona naye kwa sasa ana mambo meng tulikuaw 50/50 share
Procedures za kuanzisha kiwanda kidogo zipoje,
Kwa maana ya usajili na vibali
 
Zisiwe na mchanga mchanga tu, ukiweza mix na tende alafu iite Mkuu. Kwenye branding weka picha ya mwanaume miraba minne alafu sasa Piga promo kuwa zinaongeza nguvu za kiume.

Hapo kuuzani 100%

Ukiona hiyo ni jau, izo karanga mix na flavour yoyote inayopendwa na wadada, alafu iite Mrembo. Branding weka picha ya mdada mwenye hips zake. Sasa promo sema inaongeza shepu na ni special kwa wanawake.

Utauuzakwa uhakika.

Ukiona sawa fanya vyote vyote si unajua tena mwaka wa ku force huu Mkuu.
 
Procedures za kuanzisha kiwanda kidogo zipoje,
Kwa maana ya usajili na vibali
Unaenda sido kuna ela unalipa na training ya uzalishajj baada ya hapo kipindi naanzisha ulikuwa unaenda tfda sasa hivi si imebadilishwa jina wale wanakuja kukukagua sehemu unapozalisha bidhaa zako. Kwa peanut ilikuwa lazima floor iwe na tiles wakidhika basi unapata usajili na unafuatilia pia na tbs kwa kuwapeleka bidhaa yako na kulipa fee. Barcode unapata gs1 maana bila hvyo supermarket kuuza hauzi
 
Asante nimepata mwanga japo pa kuanzia,
Ukiweza kipande uendeleze kiwanda mkuu
 
Nadhani muda pia mkuu. Maana nilichukua hadi tbs, nikawa na kakiwanda kadogo. Nikafanya branding. Shida inahitaji uwe na stock ya karanga maana msimu wa karanga karanga zinashuka ikifika msimu karanga zinakuwa adimu zinapanda lakini bei ya kopo la peanut inabaki kuwa vile vile hapo kama huna stock utatengeneza hasara. Sema throughout the journey nilijua kuwa si kila karanga inafaa kwa peanut kuna kaanga kwa ajili ya peanut na karanga ambazo hazifai.
Ningekomaa ningetoboa sema mambo yalikuwa mengi nikasitisha toka mwaka juzi. Mwaka jana nikanunua mashine ya kukaanga nikiwa na wazo la kuja kuendelea ila sijioni nikifanya hivyo. Nilikuwa na partner na rafk yangu naona naye kwa sasa ana mambo meng tulikuaw 50/50 share
Ili kuweza kuanzisha biashara hiyo kwa kiwango cha chini, inahitaji kianzio kama milioni ngapi kwa makisio?.
 
Ni ngumu kukujibu hili swali inategemea vifaa unavyotaka. Ila tuseme mimi nlinunua mashine ya kusaga karanga 1.4 mls, ya kukaanga 1.3 wanatengeneza veta pale, mashini ya kuweka seal kwenye makopo ikumbuki nilinunua bei gani maana ni blower tu inatoa upepo wenye joto ile seal inajifunga kwenye kopo unachana kama vile imetoka kwa kiwanda, makopo inategemea aina yanauzwa karoakoo. Sticker za kubandika karatasi moja ya A4 nlikuwa napront buku kariakoo. Shida ni kuwa na karanga mkuu. Pia nlikuwa na pkpk ya kusupply so mtaji ulikuwa mls kama 7 na kitu ila niliuweka kwa awamu coz haikuwa main business na ndio maana nadhan haikufanikiwa mkuu
 
Back
Top Bottom