Nataka kufuga mbuzi naomba ushauri wa yafuatayo

BARDIZBAH

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
4,814
8,594
Habari,

Kwasasa nipo mkoa X nafanya kazi pahala kwenye kampuni fulani. NAfikiria mwez wa 12 nitoe kama 500k ninunue mbuzi kama 5 huko Tabora kwa bibi yangu.

Namna ninayowaza ya kuwafuga ni kutafuta kijana wa hapo kijijini niwe namlipa 30k mwisho wa mwezi awe anawazingatia kwenye swala la machungo. Vipi hii imekaaje wazoefu?

Karibuni wanajamvi kwa ushauri na Changamoto za hapa na pale.

Natanguliza shukrani.
 
Acha kununua mbuzi kwa bibi yako.
Nenda kwenye taasisi za utafiti kule mabuki au Kondoa au tafuta wazoefu ununue mbuzi wenye tija. Wenye kuleta matokeo.
Labda kqma unataka kufuga ceremonial goat keeping.
Funguka zaidi kiongozi.
Asante
 
mbuzi 5 kuajiri mtu ni gharama, kama una mtu huko yuko kijijini na mnaendana unawaweka kwake kwanza, ili angalau waongezeke utakuwa unachangia kiasi fulani.

wakisha angalau kufika kama 20 hadi 50 ndio unaweza anza kuweka kijana
 
Acha kununua mbuzi kwa bibi yako.

Nenda kwenye taasisi za utafiti kule mabuki au Kondoa au tafuta wazoefu ununue mbuzi wenye tija. Wenye kuleta matokeo.

Labda kqma unataka kufuga ceremonial goat keeping.
Wazo zuri sana mkuu!

Unamaanisha Mabuki ya Misungwi Mwanza? Wanauza mbuzi wa kisasa?
 
Back
Top Bottom