Namna nilivompata mke wangu wa ndoa

Wakulenga

Member
Jul 1, 2015
77
134
Habari zenu members,

Leo nimetumia muda mrefu saana kuongea na kucheka na mke wangu(huaga nafanyaga hivo siku moja moja) maana huyu mwanamke hana utofauti na wanawake wengine kwahiyo naishi nae kwa akili saana.

Hivyo baada ya furaha ya muda ikabidi akili inikumbushe namna nilivompata huyu mwanamke na kumuoa baadae.

Ilikuwa mwaka 2012 wakati niko advance shule flani hivi nakumbuka ilikuwa kipindi cha kupokea wanafunzi wa form 5.

Bahati mzuri nilimuona jamaa mmoja hivi ambae nilisoma nae o-level nilikuwa sijuani nae saana ila kwa vile alinikumbuka ikabidi nimpokee, nikaenda nae room akatulia wakati wachakula cha mchana nikaenda kuchukua chakula nikala nae.

Siku iliyofuata tukaingia darasani mi nikamwambia yule chalii akomae tu palepale kwakuwa kulikuwa na kitanda ambacho hakina mtu so atalala tu.

Kweli chalii akalala pale na siku zikasonga, tukawa tunashare vitu yaan kama kuna kitu anakihitaji alafu mi sipo anafungua tu tranka langu anacheki kama kipo anachukua nami pia nacheki kwake kama kipo najichukulia.

Sasa siku moja katika pekuapekua kwenye tranka lake nikakutana na karatasi ya majina na namba za simu za watu aliosoma nao, alafu kwenye yale majina nikaona jina na msichana ambae alikuwa mtulivu mno shuleni ila nilimtangulia darasa moja.

Dah sikufikiria mzee nikachukua ile namba nikaandika kwenye karatasi nikaweka kweny tranka langu, siku iliyofuata nikaenda kuazima simu nikamcheki bahati mzuri akapatikana.

Nikaanza kushusha mistari ya kitoto, akanijibu kuwa ana mtu nikasema basi sawa isiwe shida ila akaniambia tuwe tu tunawasiliana nikajisemea tu mwenyewe huu mtego huenda hana mtu.

Basi tukawa tunawasiliana miaka miwili baadae akaniambia amekubali, duh nami nikawa nimeshajikanyaga sehem huko nikasema isiwe kesi haina shida twende tuishi.

Nikaenda nae manzi ila mim moyo wangu ulikuwa umerudi flani hivi sio kama mwanzo.
baada ya muda tukazinguana tukamwagana nikawa naendelea na maisha yangu ya chuo, nikimpigia simu tunaongea kawaida tu.

Baada ya muda manzi akapata post ya ajira akaniambia, nikamwambia sawa hongera, ooh baadae akanicheki tena akaniambia anaomba tuendelee nikamwambia haina shida maana nilishaona nina sehem yakuegemea.

Haikupita muda tukaoana mpaka leo hii niko nae nina miaka 7 kwenye ndoa.
Mimi sina ajira ila yeye ameajiriwa.

Hii siri sijawahi mwambia yy wala yule mshikaji na naamin sitakuja kuwaambia.

Na wewe kama hutojali tuambie huyo uliyefunga nae ndoa ulimpataje mpaka mkafunga ndoa na mna mda gani kwenye ndoa?
 
Huna ajira mkuu unalelewa na mkeo au ?
 
Kwa Mwamposa...."ukiwela picha yake kwenye mtungi wa gesi! , Gesi haiishi".
huyo hapo
Screenshot_20240505-234611.jpg
 
Kwa maelezo yako ulioa mwanamke asiye bikra, basi Bwana wa majeshi awabariki na kuwalinda, awaangazie nuru ya uso wake
Mkuu nilishawahi kukutana na mwanamke ambae ni bikra, nilikutana nae mara Moja tu na wala sikutaka kukutana nae Tena, na huyu ningemkuta bikra ndoa isingekuwepo kwahyo huenda kutokamkta bikra kumepelekea yy kupata ndoa namim
 
Umesema huna ajira?
Kwa hiyo mkeo ndio anakutunza master?
Kiongozi hili halina shida kwangu si amenipenda? Maana ake Kuna kitu anakitaka kwangu ndo maana amekubali.
Ila in fact huyu dada aliingia mkenge mazee maana alinilazimisha nimuoe mi baada tu yakumaliza chuo si alijua tu nitapata ajira!! Ila mpaka Leo aiseee ndo ameishia kuduaa tu.
Ila kiongozi hapo nimemaanisha ajira ya serikal ila saiv mi nakamata mkwanja kumzid yy, kwahyo tunatunza kwa kifupi
 
Swali:

- Ujaajiriwa, je una kipato labda ambacho ajira kama Biashara? Maana kama huna ajira, na huna kipato, mwaka wa 7 na mnacheka na kufurahia na shemeji, walahi umeotea bonge la mke.
Kiongozi,
Huaga napiga tu vibarua vya kuungaunga, ila nashukuru maisha yanaenda.
Nimeotea ila Kuna wakati chamoto nakiona, Hawa wanawake hawatofautian saana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom