KERO Magari yagoma kufanya safari kutoka Tunduma kwenda Mbeya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mdau kutoka mkoa wa Songwe, halmashauri ya mji wa Tunduma, kata ya Mpemba tunaomba serikali itatue changamoto ya magari yanayotoka stendi kuu ya Tunduma kutia mgomo tangu asubuhi ya Leo mpaka Sasa, usumbufu huu unakwamisha shughuli za maendeleo.

IMG_20240511_131606_835.jpg



==============

Wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma tunasikitishwa na kitendo cha kukosa vituo vya kushusha na kupakia abiria katikati ya Mji badala yake wasafiri tunaotoka nje ya Mkoa kuingia Tunduma tunalazimika kuongeza umbali wa Kilometa 13 ili kupata huduma ya kuingia katikati ya mji.

Mfano ukitokea Mkoani Rukwa mabasi hayashushi wala kupakia Abiria kutokana na kukosekana kwa vituo jambo ambalo linaongeza gharama za maisha kwani tunalazimika kurudi mahali tulipopapita.

Hoja hii imekuwepo kwa muda mrefu lakini haijafanyiwa maamuzi yenye faida kwa waathirika.
 
Back
Top Bottom