Madereva wa mabasi ya abiria Tanzania hawana akili ya kuendesha usiku,tutakwisha

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,422
37,130
Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza
 
usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Kati ya yote haya ni nchi Gani madereva wao wanakosa hata Moja,,!???
Note! Sheria kutokufuatwa, uwajibikaji mbovu wa trafic police na miundombinu mibovu + ujinga wa abilia ndio sababu ya ajali na vifo,,dereva anatenga elfu hamsini dar to mwanza ili aende speed ya 120 road , trafic wote wanakula elfu tanotano, wakiingia ndani ya basi utasikia vipi mwendo, abilia sasa walivo mazuzu utasikia kwa kweli ni mzuri baba!!subiri wapate ajali Sasa, utasikia Ile mwendo nilijua tu tutaanguka,. !!!!
 
Mrema alizifutilia mbali kwa sababu hakuwa na mabasi. Sasa watunga sheria ndiyo wenye mabasi unategemea nini? Huoni hata nauli zinavyopanda hovyo hovyo bila justification yo yote ya kiuchumi?

Mabasi yanaendeshwa kama vile hakuna sheria na hata abiria mkilalamika, trafiki anapigwa afutano tu na libeneke linaendelea. Ajali ikitokea wanatoa salamu za pole na maisha yanaendelea!
 
Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza
Augustino Mrema alifuta safari za usiku ilikuwa ni kutokana na sababu za kiusalama, mabasi yalikuwa yanavamiwa na majambazi wenye silaha, kutekwa na abiria wote kuvuliwa nguo zote walizovaa mwilini na kisha abiria kubaki uchi wa mnyama. Nguo zote za abiria pamoja na mizigo yao yote ilikuwa inaporwa na majambazi na kutokomea nayo kusikojulikana.
 
Kuna ukweli hapa
Nilipanda basi kutoka lusaka mpaka tunduma dereva alikuwa smart sana na sikumbuki kama tulikutana na trafiki pamoja na kwamba gari zinakimbia kuliko Tanzania kwa sababu barabara zao hazina konakona sana wala mabonde lakini unakuwa na amani kabisa

Nilivyokuja kupanda rungwe safari ilikuwa mbovu sana sana ni kama tu dereva ni mvuta bangi fulani kuchukuliwa huko kawekwa pale atupeleke safari ilikuwa ngumu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza

Kiongozi;
MAMBO YAMEBADILIKA sio kama enzi ya Mrema
1. Sikuhizi tuna barabara nzuri
2. Mabasi yamekuwa ya kisasa haswa (Yanachoo, yana camera, yana visibiti mwendo nk nk)
3. Uelewa umeongezeka kwa madereva na Abiria kujua wajibu wao (watu wengi wamesoma),
4. Vitu vingi kwa sasa ni Digital badala ya kutegemea traffic , mtu anaweza kufuatilia basi akiwa nyumbani/ofisini masaa 24
5. Usalama umeimarika sana hata kule maeneo ambayo Ilibidi kutemebea na askari enzi za Mrema
6. Watu wengi wame elimika (wanahitaji kufanya kazi) badala ya kushindwa kutwa kwenye mabasi (ni matumizi mabaya ya nguvu kazi)
 
Augustino Mrema alifuta safari za usiku ilikuwa ni kutokana na sababu za kiusalama, mabasi yalikuwa yanavamiwa na majambazi, kutekwa na abiria wote kuvuliwa nguo zote walizovaa mwilini na kisha abiria kubaki uchi wa mnyama. Nguo zote za abiria pamoja na mizigo yao yote ilikuwa inaporwa na majambazi na kutokomea nayo kusikojulikana.
Ilikuwa ni kwa sababu ya ajali!!! Narudia tena: ilikuwa ni kwa sababu ya ajali.
 
Mimi nalia na taa za booster sijui TBS, Polisi na Mamlaka zingine wapo wapi. Unakutana na mtu kawasha full light booster aisee anakupiga mwanga hadi gari ya nyuma nayo anaona full light.

Hizi ndio tatizo hasa ajali za usiku, zile taa ukutane nazo ghafla lazima uhame kidogo au sana, na kama umekunywa mtungi chenchi unaeza rudisha kabisa.

No biashara ila madereva wengi wa kitanzania hawajui matumizi ya full light. Mahali kuna taa za bara barani bado mjinga mmoja amewasha full light tena za booster.
 
Kiongozi;
MAMBO YAMEBADILIKA sio kama enzi ya Mrema
1. Sikuhizi tuna barabara nzuri
2. Mabasi yamekuwa ya kisasa haswa (Yanachoo, yana camera, yana visibiti mwendo nk nk)
3. Uelewa umeongezeka kwa madereva na Abiria kujua wajibu wao (watu wengi wamesoma),
4. Vitu vingi kwa sasa ni Digital badala ya kutegemea traffic , mtu anaweza kufuatilia basi akiwa nyumbani/ofisini masaa 24
5. Usalama umeimarika sana hata kule maeneo ambayo Ilibidi kutemebea na askari enzi za Mrema
6. Watu wengi wame elimika (wanahitaji kufanya kazi) badala ya kushindwa kutwa kwenye mabasi (ni matumizi mabaya ya nguvu kazi)
Barabara nzuri? Naona hujui maana ya barabara nzuri. Tena siku hizi ndiyo imekuwa hatari zaidi kwa sababu kwa vile barabara nyingi zina lami, madereva wanakimbia sana. Na hapa ndipo tunapokuja kwenye kiini cha tatizo: barabara ni nyembamba na zina kona nyingi. Matokeo yake ni magari kugongana au kupinduka.
 
Kwa hiyo tubaki na uzamani kwa upuuzi wetu wa kutowadhibiti abiria(askari barabarani na wasafiri)?Tutashangaa tumeachwa mbali sana.Tujirekebishe wakati tunatoa na kupokea huduma.
 
Siku hao wanaopewa za kubrashi wakiacha na kufanya kazi walizopewa naapa madereva wangenyooka

Ila tatizo hata mlevi anaachiwa kisa katoa buku 2
Halafu wanachukua chochote kama ombaomba
Yale maandamano mngekuwa mnaandamana kwa mambo kama haya
 
Mimi nalia na taa za booster sijui TBS, Polisi na Mamlaka zingine wapo wapi. Unakutana na mtu kawasha full light booster aisee anakupiga mwanga hadi gari ya nyuma nayo anaona full light.

Hizi ndio tatizo hasa ajali za usiku, zile taa ukutane nazo ghafla lazima uhame kidogo au sana, na kama umekunywa mtungi chenchi unaeza rudisha kabisa.

No biashara ila madereva wengi wa kitanzania hawajui matumizi ya full light. Mahali kuna taa za bara barani bado mjinga mmoja amewasha full light tena za booster.
Tanzania watu wenye sifa ya kuitwa madereva ni wachache sana. Hii ni kwa sababu namna watu wanavyofundishwa kuendesha magari ni kama utani. Mtu anamfundisha rafiki yake siku mbili, siku ya tatu anamwachia gari aendeshe mwenyewe. Halafu sasa wabongo walivyo wabishi na wajuaji. Kila mtu ni mjuaji wa kuendesha wakati wengi hawajui sheria.
 
Back
Top Bottom