Korea Kaskazini yajaribu mfumo wa droni za kimkakati za chini ya maji

HERY HERNHO

Member
Mar 4, 2022
70
314
20230408_06_1240738_L.jpg

  • Korea Kaskazini imesema wiki hii imefanya jaribio lingine la droni ya mashambulizi ya chini ya maji yenye uwezo wa nyuklia.
Tahariri ya leo Jumamosi ya gazeti la chama tawala cha Wafanyakazi imesema taasisi ya taifa ya utafiti wa sayansi ya ulinzi ilifanya jaribio hilo kwa siku nne hadi jana Ijumaa.
Ripoti hiyo ilisema droni ya chini ya maji ijulikanayo kama “Haeil-2” ilifika kwenye eneo la majaribio Jumanne wiki hii kwenye mwambao wa jimbo la Hamgyong Kusini, lililopo mashariki mwa nchi hiyo.
Ilisema droni hiyo ilitumia takribani saa 71 kusafiri umbali wa kilomita 1,000 ambazo si halisi kabla ya kufika eneo lengwa lililoigiziwa na kulipua kwa usahihi silaha ya jaribio.
Hii ni mara ya pili Korea Kaskazini kutangaza jaribio la silaha yake mpya, inayoitwa Haeil ikiwa na maana ya “tsunami” kwa lugha ya Kikorea. Nchi hiyo ilisema iliijaribu silaha hiyo mara ya kwanza mwezi uliopita, na kudai inaweza kusababisha “tsunami yenye dutu za mionzi hatari” inayoweza kuharibu meli na bandari za adui.
 
Back
Top Bottom