Kilimanjaro: Madereva wa mabasi na Costa watishia kugoma kutokana na ubovu wa Stendi ya Bomang'ombe

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,850
15,279
Madereva wa mabasi ya mikoani pamoja na Costa hasa zile zinazofanya safari zake Moshi - Arusha wametishia kugoma kwa kile kinachodaiwa ni miundombinu mibovu iliyopo Stendi ya Bomang'ombe hasa barabara.

Barabara ya eneo hili lililopo Hai Wilayani Kilimanjaro limetawaliwa na mashimo mengi na makubwa yaliyopo ndani ya Stendi hiyo ambayo yamekuwa yakisababisha uharibifu mkubwa wa magari yao.

Ukifika kituoni hapo na kuona hali ambavyo sio nzuri unaweza kukubaliana na hicho wanachotaka kukifanya kwa kuwa wapo baadhi ambao wanakwepa hali hiyo na kuamua kushusha abiria nje ya kituo, ikitokea wameonekana na Maafisa wa Polisi fainai yake ni shilingi laki mbili.

Hoja iliyopo mezani ni kuwa ushuru unaolipwa kila siku ni Shilingi 1,000 kila gari inapoingia kituoni hapo na ni lazima uingie lakini fedha hazionekani zinapoelekea, hakuna maendeleo yoyote yanayopatikana.

Kama mamlaka ambazo zinapokea fedh kila siku hazitafanya maamuzi na Askari nao wakiendelea kupiga mabao yao ya Laki Mbili, tunapoelekea ni kushuhudia mgomo.
WhatsApp Image 2024-04-05 at 10.06.42_596873e4.jpg

WhatsApp Image 2024-04-05 at 10.07.08_0bb30f92.jpg

WhatsApp Image 2024-04-05 at 10.05.56_5554981a.jpg


Pia soma:
 
Ile stand ya Bomang'ombe kwa miaka nenda rudi haibadiliki na haiendelezwi sijui sababu ni nini na wanapokea ushuru kila siku kila baada ya dakika kadhaa

Ni kama ile stand iliyopo pale njia panda ya himo kama unaelekea Mwanga na Same, wanachukua ushuru kila siku kwa miaka zaidi ya 10 sasa lakini hakuna kilichofanyika

Halmashauri zishughulikiwe
 
Ile stand ya Bomang'ombe kwa miaka nenda rudi haibadiliki na haiendelezwi sijui sababu ni nini na wanapokea ushuru kila siku kila baada ya dakika kadhaa

Ni kama ile stand iliyopo pale njia panda ya himo kama unaelekea Mwanga na Same, wanachukua ushuru kila siku kwa miaka zaidi ya 10 sasa lakini hakuna kilichofanyika

Halmashauri zishughulikiwe
Jamani naomba ieleweke standing ya himo na bomang'ombe hazistahili kuitwa stendi tafuteni jina lingine sio kuita standing za mabasi
 
Back
Top Bottom