Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,247
- 26,149
Katika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.
Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.
Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM
Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.
Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:
1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja
2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.