Hizi ndio sababu kwanini ni rahisi kwenda mbinguni kuliko motoni

Umeongea Vizuri Ila hujaonyesha Ushahidi wa Kwe da Mbinguni ulioandikwa kwenye biblia zaidi ya maneno yako mwenyewe..
Kwa mujibu wa Ufunuo kiti cha Enzi kitashuka na Mbingu mpya kwahyo kusema kuhusu Kiti cha enzi ni mbinguni bado kuna Ualakini
Ushahidi nilionyesha kwa ufafanuzi wa 1 thesalonike 4. Huo hujauzungumzia kabisa. Hata Yesu mwenyewe ni ushahidi anakwenda kuandaa mahali ili aje atuchukue yeye alipo na sisi tuwepo. Hilo zoezi ni utangulizi wa kiti cha enzi kushuka.

Kama Mungu anashuka kutoka mbingini na watu kuja sehemu mpya aliyoiandaa akae na hao watu. Hujiulizi hao watu huko mbingini wamefikaje. Mchakato wa hao watu kufika huko ndio ninausisitiza na kupigia debe. Ndio maana nasisitiza umejenga msimamo kwenye vipisi vya taarifa sio picha yote.
 
Naomba nijibu maswali yangu haya matatu kwa wewe unavyoelewa mbinguni kuna nini sababu hio mbingu (kutokana na watu wanavyoelezea huenda ikawa kama Motoni kwa wengine)

  • Mbinguni kuna nini na watu wanafanya nini ?
  • Iwapo mimi wadau wangu wote niliokuwa ninaelewana nao duniani pamoja na ndugu zangu ambao tunakula nao bata wakiwa motoni wanachomwa na mimi nikajiunga na nyie mbao hata huku hatuelewani na naona tunazinguana, nitakuwaje na furaha ?
  • Nyie mtakuwa watu wa aina gani mnakula bata wakati wengine huko wanahangaika na mateso na nyie mnasherekea maisha yenu yote, huo si ni kama u-sadist ? Binafsi labda nibadilike na niwe robot lakini siwezi kuwa na furaha wakati wengine wana matatizo...
Mbinguni kuna vitu ambavyo macho hajawahi kuviona, wala masikiò kusikia. Mambo ambayo Mungu ameandaa kama zawadi kwa watoto wake.
Biblia imeyaeleza kwa lugha hafifu maana mengine hayaelezeki kwa lugha za duniani.

Kuhudu kuumia wenzako kuungua motoni. Kitu cha kwanza zoezi hilo litatanguliwa na hukumu ya haki ambayo kila mtu atakili na kukubali maamuzi aliyochagua. Ndio maana ya sentensi kila goti litapigwa na kukiri hukumu yako ni ya haki.

Hakuna mtu atakayeenda motoni kwa unconscious decision hata kama sasa tunajitoa fahamu. Ataingia kwa hiyari yake na kupenda na hata wewe utaonyeshwa na kudhihirishiwa kuwa jamaa amependa bata la motoni zaidi ya hilo la mbinguni. Hata yeye hatalalamimika.

Ndio maana watu wote watakaoongia mbinguni kabla ya shamlashamla kuanza watashirikishwa docs za hukumu ua malaika na watu wenzao na kukiri kabisa hukumu hiyo ni ya haki na ya kweli na Mungu amekuwa muungwana kuheshimu kabisa maamuzi ya wajomba kula kibiriti na kupotea kabisa. Bata likifunguliwa hakuta kuwa na muda wa majutoa au malalamiko.
 
Unaiita Takataka sehemu ambayo inakuhifadhi, unaposema Dunia ni takataka naomba unijibu swali hili kati ya Dunia na watu nani amepewa hukumu ya kufa ?

Hata kwenye dini mnazoamini hakuna sehemu inayoonyesha dunia imewahi kwenda kinyume na Aliyeiumba ila waishio humo ndo huenda kinyume na Sheria za Muumba, wa kuitwa takataka ni watu na sio Dunia,

Muumba anaipenda Dunia hawezi kuitupa wala kuiangamiza kama mnavyodanganyana makanisani na misikitini,.... Moja ya kiumbe kitiifu sana kwa Muumba basi ni Dunia.

Na kwa kkuonyesha kwamba Dunia ni kiumbe pendwa sana hata ukisoma katka hayo maandiko mnayoamini yanaonyesha kabsa baada ya maasi kuzidi ndani ya Dunia......Muumba aliangamiza wanyama,wadudu na wanadamu wengi sana kwa Gharika,

Swali la kujiuliza unafikiri kwann Dunia haikuadhibiwa ila viumbe viishivyo humo ndo vikaadhibiwa ? Kama Muumba angeiona Dunia imekosea asingeshndwa kuwahamisha kidogo wakina nuhu wakaishi hata Kwenye Jua au sayari nyngnezo alafu aiangamize Dunia kisha aiumbe mpya.

Ukishindwa kuelewa huo mfano wa Mwisho basi.
Sio mimi ni aleiumba ndio anasema hivyo. Tunaishi kwenye version chakavu kabisa ya dunia.

Isaya 24:20
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.

Mwanadamu ndiye mfalme wa hii dunia. Alichokifanya pale eden. Ni regime change. Alimkabidhi ibirisi ufalme wa hii dunia. Na kazi ya ibirisi ni kuiba, kuua na kuharibu. Ndio maana anaandaa silaha na mavumbuzi ambayo matokeo yake ni uharibifu wa dunia na vyote vilivyomo. Kimsingi ni muuaji.

Ukiwa umempokea Yesu unafanyika kuwa raia mpya wa serikali ya Mungu. Hivyo duniani panabaki kama mahala pa mpito kwako ukitazamia mahala bora kabisa siku xijazo ambazo serikali yako ambayo sio danganyifu imeandaa.

Sasa unapokuwa mtoto wa ufalme au serikali hii unaanza kuwa na attributes za mbingunimbinguni. Na hii ndio itakupa msukumo wa kuboresha maeneo yako ya mpito sio ili pawe bora milele bali pakuhifadhi wakati unasubiri kitu bora zaidi.

Mungu sio mchafu, na mcha Mungu kuwa mchafu au kuishi pachafu no dhambi na ni uwakilisho mbaya wa ufalme wako. Hivyo utasafisha mazing8ra yako kama Yesu alivyoagiza wanafunzi kusafisha mabaki ya mikate na kuyaweka kwenye vikapu ili lile pori libaki safi.
 
Mbinguni kuna vitu ambavyo macho hajawahi kuviona, wala masikiò kusikia. Mambo ambayo Mungu ameandaa kama zawadi kwa watoto wake.
Biblia imeyaeleza kwa lugha hafifu maana mengine hayaelezeki kwa lugha za duniani.
Kwahio hatujui.., sababu ukisema furaha isiyo kifani (je furaha inafanana kwa kila mtu) unless tuseme ni kama vile mtu anapotumia kilevi (drugs) yaani zile chemicals zinamfanya awe na furaha no matter nini kinamzunguka....
Kuhudu kuumia wenzako kuungua motoni. Kitu cha kwanza zoezi hilo litatanguliwa na hukumu ya haki ambayo kila mtu atakili na kukubali maamuzi aliyochagua. Ndio maana ya sentensi kila goti litapigwa na kukiri hukumu yako ni ya haki.
Haijalishi kama mtu atakiri au vipi ndio maana hata wale wabakaji na majangari kule mahakamani bado wana ndugu wanaowatembelea na kuwaonea huruma..., Sasa kama mimi nakula bata na mke wangu kipenzi na watoto wote wanachomwa moto mimi kuendelea na furaha lazima ubinadamu wangu (huruma na upendo) utakuwa umeondoka na nimekuwa kama roboti
Hakuna mtu atakayeenda motoni kwa unconscious decision hata kama sasa tunajitoa fahamu. Ataingia kwa hiyari yake na kupenda na hata wewe utaonyeshwa na kudhihirishiwa kuwa jamaa amependa bata la motoni zaidi ya hilo la mbinguni. Hata yeye hatalalamimika.
Mimi tuseme nimekwenda mbinguni na wadau wangu wote marafiki zangu wapo motoni kwahio company yangu ipo motoni ila mbinguni kuna wadau kama nyie ambao hata huku kitaa zilikuwa haziivi (uoni hapo ni vigumu kuniambia takuwa nina furaha)
Ndio maana watu wote watakaoongia mbinguni kabla ya shamlashamla kuanza watashirikishwa docs za hukumu ua malaika na watu wenzao na kukiri kabisa hukumu hiyo ni ya haki na ya kweli na Mungu amekuwa muungwana kuheshimu kabisa maamuzi ya wajomba kula kibiriti na kupotea kabisa. Bata likifunguliwa hakuta kuwa na muda wa majutoa au malalamiko.
Siongelei kulalamika au Haki naongelea uhalisia binafsi siwezi nikala bata wala kufurahia kama kuna wadau wangu wanahangaika..., Kwangu mimi raha ni kula na wenzangu..., Kwahio if that is the case ninaomba Wasabato Imani yao iwe ya kweli kwamba wakosaji tusiamshwe tulale usingizi wa maisha sababu ni heri kulala kuliko kuwa macho kushuhudia watu wanahangaika na kupata shida za hatari
 
Kwahio hatujui.., sababu ukisema furaha isiyo kifani (je furaha inafanana kwa kila mtu) unless tuseme ni kama vile mtu anapotumia kilevi (drugs) yaani zile chemicals zinamfanya awe na furaha no matter nini kinamzunguka....

Haijalishi kama mtu atakiri au vipi ndio maana hata wale wabakaji na majangari kule mahakamani bado wana ndugu wanaowatembelea na kuwaonea huruma..., Sasa kama mimi nakula bata na mke wangu kipenzi na watoto wote wanachomwa moto mimi kuendelea na furaha lazima ubinadamu wangu (huruma na upendo) utakuwa umeondoka na nimekuwa kama roboti

Mimi tuseme nimekwenda mbinguni na wadau wangu wote marafiki zangu wapo motoni kwahio company yangu ipo motoni ila mbinguni kuna wadau kama nyie ambao hata huku kitaa zilikuwa haziivi (uoni hapo ni vigumu kuniambia takuwa nina furaha)

Siongelei kulalamika au Haki naongelea uhalisia binafsi siwezi nikala bata wala kufurahia kama kuna wadau wangu wanahangaika..., Kwangu mimi raha ni kula na wenzangu..., Kwahio if that is the case ninaomba Wasabato Imani yao iwe ya kweli kwamba wakosaji tusiamshwe tulale usingizi wa maisha sababu ni heri kulala kuliko kuwa macho kushuhudia watu wanahangaika na kupata shida za hatari
1: Furaha mtu anayoipata kwa cocaine, au punyeto au chochote nje ya hii ya Mungu ni furaha feki tena yenye lifespan fupi sana. Ni sawa na utamu mtu anaoupata akila kitu chenye ladha feki kama pipi. Baada ya kula anapata kiu kubwa ya furaha kuliko kabla hajapata hiyo.

Muasisi wa mambo feki ni ibirisi. Moja jambo ambalo Mungu atakufanyia katika mabadiliko hayo ni kukuokoa na vitu feki ambavyo ulivipenda kwa kutokujua kwa sababu ya shambulizi la mtazamo sahihi juu ya mambo yenye kuleta faida za milele.

2: Mahusiano ya mtu aliyefanikiwa kiroho ni yale ambayo attachment kubwa kuliko zote ni ile ya yeye na Mungu. Siku Mungu anamuumba adam, hakukuwa na rafiki, mjomba, mama, mke, mtoto, na wala jirani. Alikuwa peke yake.

Mahusiano yako na Mungu kiasi kwamba uwepo au kutokuewepo kwa washaji zako hayaathiriki ndio kiwango cha juu cha kujitambua kwa mwanadamu.

Mungu kwa kujua hilo la watu ambao bado wanabaki na makovu ya wapenzi wao waliopotea, atafuta kila ambacho kitaleta simanzi mbinguni maana hakuna huzuni huko. Kila utakachopoteza utakipata mara billioni ikiwemo mke marafiki na watoto tena kwa utoshelezefu ambao uko nje ya upeo wa kibinadamu.

Ufunuo wa Yohana 21:4
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Ufunuo wa Yohana 21:5
Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
 
Mkuu una mtazamo wa kimungu ambao ata viongozi wa dini hawana.
Lengo la Mungu watu wote waende mbinguni
.
Upeo wa uelewa wa kiongozi wa dini unategemea kiwango chake cha kumuelewa Mungu sio taratibu za kiriturujia za kidini. Ndio maana Yesu mtoto muumini kabisa wa miaka 12 aliwaoutsmart magwiji ya viongozi wa kidini.

Tunapaswa ķutafuta uhusiano wa juu na Mungu hii ndio muhimu sio kutafuta kutally uhusiano wetu au uelewa wetu na Mungu na uelewa wa kiongozi wa dini.
Ndio maana kunawaumini wanauwezo mkubwa wa nguvu za Mungu huku sisi viongozi wa dini tuna uwezo mkubwa wa nguvu za giza bila kujali kama tunakauli za kimungumungu mbele za watu.

Ni hayo tu.
 
Sijui kama nitakuwa sahihi..

Kwa upande wangu, Huwa naamini hakuna moto. Sababu ni hizi;

Nikiangalia jinsi maisha ya ulimwengu yalivyo. Kuna watu wanaoishi maisha ya dhiki sana hapa ulimwenguni na wapo wanaoishi kifalme sana. Kuna watu tangu wanazaliwa Hadi wanakufa ni watu wa kuandamwa na magonjwa tu na wapo ambao ni nadra. Kuna watu wanazaliwa na ulemavu na wanateseka nao Hadi mwisho na wengine kinyume chake.

Kwa kuzingatia haya, naamini kabisa hakuna moto Kwa sababu, ikiwa Kuna mtu anaishi kifalme na ni mtenda dhambi, na yupo mwenye dhiki kuu, fukara pia mtenda dhambi, tukisema suala la kuingia wote motoni naona hakuna usawa hapo na tunajua Mungu wetu ni mwenye haki. Kuna mmoja mzani wake hautokuwa na balance. Fukara atakuwa kateseka mara mbili, hakuna sehemu atayafurahia maisha. Dunia ni kapata mateso na bado anaenda kukutana na adhabu ilhali tajiri kafurahia Dunia ni na kuteseka baadae.

Sijui kama naeleweka????

NAleta hoja ya pili...
Biblia inaonesha watu wenye dhambi wakifa wanaenda kuzimu roho zao zinakuwa kwenye mateso wakisubiri siku za mwisho kwenye moto wa jehanam wenye mateso ya milele
Mhubiri 9:10
 
1: Furaha mtu anayoipata kwa cocaine, au punyeto au chochote nje ya hii ya Mungu ni furaha feki tena yenye lifespan fupi sana. Ni sawa na utamu mtu anaoupata akila kitu chenye ladha feki kama pipi. Baada ya kula anapata kiu kubwa ya furaha kuliko kabla hajapata hiyo.

Muasisi wa mambo feki ni ibirisi. Moja jambo ambalo Mungu atakufanyia katika mabadiliko hayo ni kukuokoa na vitu feki ambavyo ulivipenda kwa kutokujua kwa sababu ya shambulizi la mtazamo sahihi juu ya mambo yenye kuleta faida za milele.
Kwahio furaha yangu ya kuona hakuna watu wanaopata shida / matatizo nayo ni feki..., Na mimi kuwa nakula Bata mbinguni wakati wengine wanapata shida na mimi kutokujali hio ndio Real ? Feki ni nini na Real ni nini ? kama ufeki unapimwa kwa muda ambao furaha unabakia nayo basi mtu ukiridhika na kuwa na peace of mind huwezi kuita ni feki
2: Mahusiano ya mtu aliyefanikiwa kiroho ni yale ambayo attachment kubwa kuliko zote ni ile ya yeye na Mungu. Siku Mungu anamuumba adam, hakukuwa na rafiki, mjomba, mama, mke, mtoto, na wala jirani. Alikuwa peke yake.
Siwezi Kujifanya nampenda sana ambaye sipo nae hapa kuliko hata ambao ninao hapa kila siku..., kwangu mimi huo ni unafiki...
Mahusiano yako na Mungu kiasi kwamba uwepo au kutokuewepo kwa washaji zako hayaathiriki ndio kiwango cha juu cha kujitambua kwa mwanadamu.

Mungu kwa kujua hilo la watu ambao bado wanabaki na makovu ya wapenzi wao waliopotea, atafuta kila ambacho kitaleta simanzi mbinguni maana hakuna huzuni huko. Kila utakachopoteza utakipata mara billioni ikiwemo mke marafiki na watoto tena kwa utoshelezefu ambao uko nje ya upeo wa kibinadamu.
Kile kimoja kinachopotea kwangu mimi ni bora na cha muhimu kuliko hata vitu bilioni kadhaa vilivyopo.., Nadhani hata kwenye ile hadithi ya Mwanampotevu (The Prodigal Son) tuliona hilo jambo...

Kwahio binafsi wadau wangu ninaokunywa nao kilauri kila siku kwa kutokuwa nao huko popote kwenye Bata siwezi kuwa na furaha unless huyo wa kipindi hicho atakuwa tofauti na mimi wa sasa (na kama nikiwa tofauti basi takuwa Fake)
 
Hahahaha na wewe mkubwa hivyo unaamini hizo hadith 😝😝😝
1715595654907.png
... mbinguni kuzuri!
 
Sijui kama nitakuwa sahihi..

Kwa upande wangu, Huwa naamini hakuna moto. Sababu ni hizi;

Nikiangalia jinsi maisha ya ulimwengu yalivyo. Kuna watu wanaoishi maisha ya dhiki sana hapa ulimwenguni na wapo wanaoishi kifalme sana. Kuna watu tangu wanazaliwa Hadi wanakufa ni watu wa kuandamwa na magonjwa tu na wapo ambao ni nadra. Kuna watu wanazaliwa na ulemavu na wanateseka nao Hadi mwisho na wengine kinyume chake.

Kwa kuzingatia haya, naamini kabisa hakuna moto Kwa sababu, ikiwa Kuna mtu anaishi kifalme na ni mtenda dhambi, na yupo mwenye dhiki kuu, fukara pia mtenda dhambi, tukisema suala la kuingia wote motoni naona hakuna usawa hapo na tunajua Mungu wetu ni mwenye haki. Kuna mmoja mzani wake hautokuwa na balance. Fukara atakuwa kateseka mara mbili, hakuna sehemu atayafurahia maisha. Dunia ni kapata mateso na bado anaenda kukutana na adhabu ilhali tajiri kafurahia Dunia ni na kuteseka baadae.

Sijui kama naeleweka????

NAleta hoja ya pili...
... kwa jinsi maisha ya Duniani yalivyo mafupi na yaliyojaa mashaka kwa masikini, matajiri, wenye afya na watesekao kwa magonjwa, MOTO WA MILELE HAUNA MIZANIA KWA YEYOTE!
 
1: Mungu ananguvu kuliko shetani.

2: Mungu ametoa kila kitu cha lazima mtu yeyote atakaye kwenda aende. Hakuna alichobakiza.

3: Neema ya Mungu ina nguvu kuliko nguvu ya dhambi

4: Kwa Mungu unaweza kuwa muovu miaka yako yote ilq sekunde moja tu kama mwizi msalabani ukasema Unikumbuke katika ufalme wako tayari tiketi ikiwa umemaanisha.

5: Biblia inaonyesha watakeondea mbinguni ni wengi kama mchanga wa bahari. Yaani hawahesabiki. Hata wewe ukitaka unaenda.

Ni hayo tu.
Hakuna mahali pagumu kwenda kama Mbinguni. Kila mwaka ni watu wawili watatu tu wanafanikiwa kati ya mamilioni wanaokufa!
 
Il
Maana yangu inaanzia kwenye kuamini yasiyoonekana na kugusika. Mambo halisi ambayo kwa sasa yanaonekana kama ni upumbavu ujinga na ushamba. Ila sisi wengine tumshategua huo mtego wa dhihaka kwa mambo hayo kitambo saana. Uhalisia wa tukio la kwenda mbingini ni moyo wa uwepo wangu na uhai wangu. Sitenganishwi ha hiki mkuu
a ukumbuke wewe ni Balozi wa serikali ya Mbinguni, na upo hapa duniani ili kufanya lile kusudio ambalo Mungu amekupa...

So Mbinguni na yaliyomo ni mali yetu sote, ila wengine ndio hivyo tena tunaingia mkenge wa kuaminishwa ya duniani ambayo yanatupeleka kwenye kuwa kuni huko kuzimu..

Suala la kumjua Mungu, kumtumikia, ni wajibu wetu, ila kufanya kazi ya Baba aliyotutuma ni la lazima.

Sasa utajuaje kusudio lako kwa Mungu hapa duniani?

Hilo ni swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kulijua na kulikamilisha.

NB: Wapo ambao wanatimiza makusudi ya Mungu pasipo hata kujua..na Muda wako ukifika tuu, done.
 
Back
Top Bottom