The best 007
JF-Expert Member
- Oct 6, 2019
- 38,142
- 83,533
Tuliambiwa kuna maboresho makubwa ya uwanja wa Benjamin William Mkapa (BWM) Stadium, lakini kiuhalisia sijaona jipya lolote mpaka jana nilipoenda kuangalia mechi ya wananchi (timu bora Afrika Mashariki na kati kwa sasa).
Uwanja ni mchafu, vyoo vichafu, viti ni vilevile vya kizamani, kwa kifupi hakuna kilichofanyika mpaka sasa licha ya uwanja kufungwa kwa muda mrefu kwa kigezo cha kupisha ukarabati. Watanzania tunauliza shida ni nini? Yani hakuna jipya zaidi ya kuweka vibanda vya benchi la ufundi na screen za matangazo (LED) ambazo pia hazitumiki kwa sasa.
Tulitegemea kuona mpaka sasa sehemu ya kukimbia wanariadha ingekuwa ya blue lkn ni hovyo kabisa, tulitegemea kuona mazingira ya uwanja kuwa safi lakini ni hovyo kabisa, tatizo ni nini? Wakati tulitajiwa mapesa marefu ya ukarabati, je tuhesabu kuwa tumepigwa ama? Naiomba serikali kupitia msemaji mkuu na bodi ya ligi waje na majibu haraka iwezekanavyo mana tunautegemea huu uwanja katika mashindano ya afcon 2027, hii ni aibu.