Hakuna kifaa chochote kilichoungua lakini dili zangu zimeharibika sababu ya kukosa umeme, naanzia wapi kiwashtaki TANESCO?

Black Opal

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
201
263
Wakuu kichwa cha habari nadhani kinajieleza vya kutosha.

Hakuna uharibifu wowote nilioupata upande wa vifaa kutoka na "Hitilafu" hii ya umeme lakini dili zangu zinaharibika sababu ya hitilafu hiyo.

Kazi nyingi zinategemea umeme, unapata dili fresh, unapokea advance na kazi inabidi ikamilike ndani siku mbili halafu kama hivi unakatiwa umeme masaa saba sasa, kazi imeharibika, ugali wako ndio unakuwa rehani hivyo.

Je, kwa hali kama hii nawezaje kuwashtaki TANESCO ?

UKizingatia anayetaka kushtaki hana uwezo wa kulipia Mwanasheria, naamini wapo watu wengi mambo yanaharika kama mimi wanaishia kurusha laana za dunia TANESCO wakati tunaweza kudili nao Kisheria.

Wakuu naomba mwongozo wenu.
 
Back
Top Bottom