Dkt. Sule: Kutumia Majini kupata Mali si dhambi/ haramu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,691
12,051
Screenshot_2024-05-14-23-13-48-364_com.twitter.android~2.jpg

Akifanyiwa mahojiano na kituo cha Habari cha Global TV Dkt Sule ameeleza masuala mbalimbali yanayohusu kupata mali kwa kutumia majini. Akifafanua kwa imani yake kuwa kupata mali kwa Majini si haramu Sule anasema:

Kupata mali kwa njia ya majini ambao sio wachafu sio haramu, nitasema na nitaendelea kusemawala siogopi. Wapo Majini ambao wanamiliki mali, inategemea pia mali hizo unazitumia wapi. Ukitumia mali hizo kwa njia yaFreemason unaoza upande moja hiyo ni haramu.

Kama unatumia dua mali na riziki zinafunguka, mali inapatikana wale waliokusahau wanakukumbuka, unaletewa mipango ya biashara inakuja, unatiki moja zinakuja kumi, hizo ntafanya mpaka naondoka duniani, siachi sababu simshirikishi Mungu , mimi natafuta riziki za halali

Ingekuwa naiba ingekuwa skendo Sule mwizi lakini nafanya dua. Namfanyia dua mtu ya kwake yanafunguka ananiletea hela, napata mali hiyo kwangu sio shida.


 
Hizi imani ni utata mtupu, heri akina LIKUD na Mshana Jr walioamua kubaki na mizimu ya babu zao
Mizimu kila mtu anayo, tunachotofautiana ni unamizimu ya aina gani? Ipo mizimu ya kimasikini, mizimu ya maradhi, mizimu ya kuvuruga mahusiano mizimu ya utambuzi , mizimu ya kichawi , mizimu ya utajiri n.k

Hao ulio wataja wana mizimu ya utambuzi mizimu ya kiganga kwenye watu elfu 30 unaweza kupata wawili au watatu tu.
 
Hawa watu ni waganga wa kienyeji wanawashika masikio waislamu wanaopenda short cut na wasio na maarifa wala utambuzi juu ya dini yao, habari za kuabudu na kuomba msaada majini ni katika madhambi yanayomtoa mtu kwenye uislamu.

Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia malaika: "Hivi hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi"? watasema: "Tunakutakasa kukutakasa, wewe ndiye kipenzi chetu kinyume na wao, bali wao walikuwa wakiwaabudu majini, wengi wao wakiwaamini hao".

Qur'an 34:40-41

Huu ndio uislamu wa sawasawa unamtaka mtu kufanya kazi na kutafuta rizki ya halali, na si kutumia ushirikina wala kafara na matambiko na kuwanyenyekea majini kupata mali, nimeona hapo juu watu wengi wameutukana uislamu kwasababu ya neno la mtu mmoja asiyejua hata uislamu ni nini.

Wakuu kuweni na uvumilivu sisi ndo tumeshakuwa waislamu na tutabaki hivyo mpaka siku ya kufa kwetu kwa idhini ya allah, punguzeni chuki na muache matusi yasiyo na maana, uislamu uko mbali na kuabudu na kuwataka msaada mashetani.
 
Back
Top Bottom