Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Siku nyingine usilipe pesa kubwa kama hiyo kwa agent bila ku verify vipimo mwenyewe.

Mimi walinikadiria 1.8mil nikafunga safari kwenda dsm tukapima na tape measure nikiwa naona kumbe watu wao wa china waliover estimate! Badala ya 1.8mil nikalipa 1.3mil! Nika save laki5 nzima!
Jomba mimi kabla ya kununua kitu chochote lazima nijue vipimo vya package. Yaani kabla Silent Ocean hawajanipa bei tayari ninakuwa na makadirio yangu binafsi. Na mara nyingi huwa wako chini zaidi. Ila nashukuru kwa ushauri
 
Bado kuna vijiji vingi wanafanya hivyo
Na wengi hawajajua bado ila ina hela sana.

Ili kuona matunda yake Kodi na nyumba huko huko Kijijini kwaajili ya kufanya store za nafaka unazopota Kwa Wakulima

Baada ya miezi 2/3 unakuta una Tani za kutosha za mazao
 
Jomba mimi kabla ya kununua kitu chochote lazima nijue vipimo vya package. Yaani kabla Silent Ocean hawajanipa bei tayari ninakuwa na makadirio yangu binafsi. Na mara nyingi huwa wako chini zaidi. Ila nashukuru kwa ushauri

Nakubaliana na wewe ila kilichonikuta ni hiki..

Kiwandani walinipa vipimo vya mzigo na silent ocean wakanipa vyao, nikajiuliza why hawa jamaa vipimo vyao vimeachana sana na sio kawaida! Maana mara zote huwa nakuga either wako sawa au wanapishana kidogo sana!

Baada ya kuona hivyo ndio ikabidi niende dsm mwenyewe ku verify kwa tape measure! Ningelipa kichwa kichwa hamna rangi ningeacha ona!

Pia kujua kiasi makadirio binafsi ni rahisi ni unachukua cbm ulizopewa na supplier wako then unazidisha na rate ya agent!
 
Nakubaliana na wewe ila kilichonikuta ni hiki..

Kiwandani walinipa vipimo vya mzigo na silent ocean wakanipa vyao, nikajiuliza why hawa jamaa vipimo vyao vimeachana sana na sio kawaida! Maana mara zote huwa nakuga either wako sawa au wanapishana kidogo sana!

Baada ya kuona hivyo ndio ikabidi niende dsm mwenyewe ku verify! Ningelipa kichwa kichwa hamna rangi ningeacha ona!

Pia kujua kiasi makadirio binafsi ni rahisi ni unachukua cbm ulizopewa na supplier wako then unazidisha na rate ya agent!
Kweli mkuu. Kujua vipimo ni muhimu sana. Watu wengi ni wavivu kusoma specifications za mzigo au hata kumuuliza muuzaji
 
Na wengi hawajajua bado ila ina hela sana.

Ili kuona matunda yake Kodi na nyumba huko huko Kijijini kwaajili ya kufanya store za nafaka unazopota Kwa Wakulima

Baada ya miezi 2/3 unakuta una Tani za kutosha za mazao
Ni nzuri ila na wewe unatakiwa uwe na hela za mahitaji yako mengine. Ni biashara inayohitaji subira
 
Nje ya mada..

Hivi kumbe hutu tudada dada natotuonaga tunauza maduka ya simu full kuringa ringa na kuongea kwa nyodo, kujidai tu slay queen, kumbe tunalipwa laki tu kwa mwezi..?🙄
Unashangaa hao mkuu? Bar maid mwenyewe anaringa na kila mwisho wa mwezi anakatwa mpaka hela ya glass aliyovunja anabaki na 20k tu. Ground pagumu sana
 
TRA wana njia 2 za kukadiria kodi. Kwanza ni mtu anayetunza kumbukumbu/hesabu pili ni mtu asiyetunza.

Sasa jamaa inaonekana hatunzi so wanamkadiria kutokana na uzoefu wao TRA.

Angekua anatunza hesabu zake angelipa kodi ndogo sana!
Inaonekana anatunza ndio maana ana rekodi za.kila kitu ila.hajui kuwa alichokadiriwa si sahihi..
 
Bongo ukiamua kufanya biashara watu wanahisi kama ushafanikiwa,kuanzia serikali mpaka watu wa kawaida watadhani wewe ni tajiri,kodi za ajabu ajabu zitakuandama,ushuru,mara fire,mara service levy,..mara omba omba nao waje,mara chuma ulete,mara wanawake wajitegeshe mimba ili uwape hela ya mtoto kila mwisho wa mwezi..yaani ni shida tupu.
 
Biashara hizi ndogo ndogo zenye mtaji wa chini ya 10M kusavaivu ndani miaka mitatu ni ngumu sana mwaka jana nami nilifunga duka baadaya ya kutoona faida kutokana na gharama kubwa ya uendeshaji kwa mfano
1. Tra 250,000
2. Leseni jiji 200,000(phones and accessories)
3. Kodi jengo (150,000*12)=1,800,000
4. Umeme (10,000*12)=120,000
5. Afu kuna hawa jamaa wa fire niliwakataa
6. Posho ya mfanyakazi (100,000*12)=1,200,000
7.ulinzi (10,000*12) =120,000
8. Usafi na mengineyo=100,000
9. Service levy( hapa niligoma kabsa kutoa) wakatisha kufunga biashara wakanipa control number kwa lazima ila sikulipa

Kwa gharama Hizi kutoboa ni ngumu sana aisee bora niendelee kuajiliwa ila biashara ni big no kabsa
Kweli kabisa,,
 
Nmekumbuka mbali, kipindi nafanya biashara TRA walipiga kufuli goli langu,, dogo anapiga "boss jamaa wamepiga kufuli huku" nikamchek mwamba mmoja tukatimba kwa yule mzee mkuda,, kumbe wanajuana,, hiyo ndio pona yangu,, nikapewa na funguo nikaenda fungua maisha yakaendelea, ile biashara ilidumu miaka 4, nikaifunga,,
 
Back
Top Bottom