Barua ya wazi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Nsema

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
273
467
Mh.Waziri Mkuu awali ya yote nakupa pongezi na shukrani Kwa kulipambania taifa letu kwenye pilika za kuleta maendeleo. Mungu azidi kukupa nguvu na uwezo wa kuendelea kulipambania taifa letu Ili lisonge mbele.

Mh. Waziri mkuu nakuja kwako naleta Malalamiko yangu Kwa niaba ya wenzangu tuliokuwa tunafanya kazi ya Uthamini kwaajili ya wananchi kupisha maeneo Yao kwenye hifadhi ya Ruaha bonde la Ihefu.

Mh.Waziri Mkuu tulikuwa watalaam wapatao 183 wanaojumuisha Maafisa maendeleo, Wathamini, Maafisa Mipango miji, Wapima,Madereva,na Maafisa salama wa raia (Police) ambao walishiriki kufanya hii kazi.

MH.Waziri mkuu zoezi hili la Uthamini lilisitishwa mnamo tarehe 02/11/2023 huku watalaam wakiwa wanadai Posho zao za takribani miezi 3 na zaidi ukizingatia mara ya mwisho kulipwa ilikuwa tarehe 01/07/2023.

Waziri mkuu tangu zoezi la Uthamini lisitishwe Hadi Leo hakuna Posho yoyote tumelipwa ambapo takribani miezi 6 imepita.Kama watalaam tumefatilia ngazi nyingi kupata ufumbuzi wa madai yetu lakini hatujapata majibu yoyote.

Kwa niaba ya Wenzangu tunakuomba Waziri mkuu ingilia Kati tusaidie tupate stahiki zetu kwasababu wakati tunafanya hii kazi yenye manufaa Kwa nchi yetu tulikopa sehemu mbalimbali Ili tuweze kujikimu ukizingatia Posho ilikuwa hailipwi mara Kwa mara na kupelekea kuwa na madeni ambayo hatujui tutayalipaje,na pia hatujui uchakataji wa malipo yetu ulifikia wapi? MH. Waziri Mkuu tunaomba tusaidie katika wewe tunaamini jibu tutapata.

Mwisho Nakutakia Ujenzi mwema wa Taifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kazi ziendelee.
 
Back
Top Bottom