Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,925
- 12,204
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe; Paul Makonda amesema pikipiki hizo zimetolewa kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni utekelezaji wa sehemu ya ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni ya kutoa pikipiki hamsini kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuimarisha usalama katika Jiji la Arusha hasa kwa kuzingatia ni kitovu cha Utalii hapa Nchini.
Mheshimiwa Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linaimarisha usalama maeneo yote katika Mkoa huo ili uendelee kuwa shwari, na shughuli za utalii zifanyike kwa amani na utulivu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bwana Abdulmajid Nsekela amesema suala la usalama ni jambo la muhimu hasa kipindi hiki ambacho idadi ya watalii imeongezeka mkoani humo hivyo benki hiyo ikaona ni vyema kusaidia vitendea kazi ambavyo vitarahisisha katika utendaji wa kazi.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa na benki hiyo kwa msaada huo, amebainisha kuwa pikipiki hizo zitasaidia kufanya doria katika mitaa mbalimbali ili kutimiza dhamira ya Serikali ya kuona mkoa huo unakua shwari wakati wote.
Aidha SACP Masejo ametoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu kuacha mara moja vitendo hivyo kwani Jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha Mkoa huo unakua shwari na litaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kutenda uhalifu.