Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 38,269
- 47,485
Hizi ajali za barabarani za mfululizo za mabasi zinazomaliza maisha ya watu na kuwafanya maelfu kuwa walemavu ni kama zimekuwa jambo la kawaida sasa na kuzoelekana.
Inasikitisha sana kuona Waafrika hatuyapi maisha thamini na hadhi inayostahili. Ajali mfululizo za mabasi za aina hii zinazotokea nchini kwetu zingekuwa zinatokea katika ulimwengu wa magharibi huenda zingeiondoa hata serikali madarakani kwa kura za raia au za bunge za kutokuwa na imani na serikali. Hili Bunge letu kwa nini halitimizi wajibu wake wa kuisimamia serikali katika mambo muhimu kama haya?! Ajali tatu za mabasi zinazoua makumi ya raia kwa mwaka zilitosha kuunda kamati maalumu lakini mpaka sasa bunge letu ni kama halina habari kuhusu jambo hili!
Serikali kwa sababu hamna jawabu sahihi kuhusu hizi ajali fanyeni haya kwa kuanzia wakati tunasubiri reli.
1. Ondoeni haya mabasi makubwa ya abiria 40, 50 hadi 60 kwa safari za masafa marefu. Safari za umbali unaozidi kilometa 200 zitumuike gari zinazobeba abiria wasiozidi 30 tu ili kama hata kuna ajali wafe wachache.
2. Magari ya mizigo ya masafa marefu yatembee saa kumi mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni tu.
3. Gari lolote litakaloharibika barabara kubwa(highways) lisikae barabarani zaidi ya lisaa moja. Polisi, afisa wa LATRA, Mwenyekiti wa kijiji au mtaa anapopata taarifa kuna gari limekaa barabarani zaidi ya lisaa limoja awe na mamlaka ya kuliondoa na kulitupa pembeni mbali na barabara kokote kule kwa njia yoyote ile.
4. Basi zote za abiria mwisho wa kusafiri kwa siku moja iwe ni masaa 12 tu , kama safari ni zaidi masaa 12 au KM 800 abiria wakate tiketi zaidi ya moja za mabasi tofauti.
5. Dereva mmoja wa basi za abiria endeshe gari kwa masaa 6 tu au KM 400 kwa siku.