Ahmed Arajiga kuwa refa (pilato) katika mechi ya Simba vs Yanga 5/11/2023

bakundande jr

JF-Expert Member
Oct 22, 2021
507
671
Wakati homa ya pambano la watani wa jadi ikianza kupanda kabla ya timu hizo kuvaana Jumapili ya kesho Novemba 5.Bodi ya Ligi imetaja waamuzi watakaopewa pambano hilo litakalopigwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Ahmed Arajiga ataamua dabi hiyo kama muamuzi wa kati akiwa na wasaidizi Muhamed Mkono na Kassim Mpanga na wa akiba ni Ramdhani Kayoko huku Kamishana wa mchezo ni Hosea Lugano kutoka Lindi.

Simba itaikaribisha Yanga ikiwa ni dabi yao ya pili msimu huu wa ligi baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti jijini Tanga, Simba ikibeba ngao hiyo.
Nini maoni yako kuhusu waamuzi hawa?

#FutbalPlanetUpdat

FB_IMG_1699098309585.jpg
 
Ni muda sasa kuwe na gunduzi za teknolojia za kusimamia mpira, hawq marefa ni watu wenye timu zao, mtu kama Gentamycine akiwa refa hawezi simamia sheria kwa uadilifu
Charismatica Fella anaweza akamzaba mchezaji kibao. Ni mtu wa kupanic
 
Huyo refa ni mwanachama kabisa ukoloni.This time akizingua itabidi mashabiki tumsake kitaa.
 
Wakati homa ya pambano la watani wa jadi ikianza kupanda kabla ya timu hizo kuvaana Jumapili ya kesho Novemba 5.Bodi ya Ligi imetaja waamuzi watakaopewa pambano hilo litakalopigwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Ahmed Arajiga ataamua dabi hiyo kama muamuzi wa kati akiwa na wasaidizi Muhamed Mkono na Kassim Mpanga na wa akiba ni Ramdhani Kayoko huku Kamishana wa mchezo ni Hosea Lugano kutoka Lindi.

Simba itaikaribisha Yanga ikiwa ni dabi yao ya pili msimu huu wa ligi baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti jijini Tanga, Simba ikibeba ngao hiyo.
Nini maoni yako kuhusu waamuzi hawa?

#FutbalPlanetUpdat

View attachment 2803548
Marefa wengi bongo ni wabovu lakini huyu ndiyo balaa kabisa. Tegemea vioha leo.
 
Back
Top Bottom