JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Mdau wa JamiiForums.com ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa UTI kwa wanawake. Anahoji inakuwaje sababu kubwa inayotajwa kuwa ni uchafu ipate mashiko kwa nyakati hizi, kwani wanawake wa zamani ndio walikuwa wasafi zaidi kuliko hawa wa sasa? Mdau huyu anashauri wataalam wa afya waingie upya maabara kuchunguza nini hasa chanzo halisi cha kuongezeka kwa maambukizi ya UTI. Kwake hoja ya kuwa ugonjwa huu unaweza kusababishwa na uchafu anaona kama haina mashiko. Sayansi inasemaje juu ya hoja hizi za mdau?
Habari zenu wakuu Hivi nmekua nikijiuliza sana ni hali ya hewa ndio inapelekea watu kuumwa sana sasahivi au ni nini?? Maana nmekua nikishuhudia watu wangi wakikohoa sana ambapo hali hii yakukohoa wengi wamekua wakieleza kua huwakuta sana ifikapo mida ya saa 12 jioni ambayo huwafanya hata washindwe kulala kwa kikohozi icho kikali. Je, mabadiliko ya hali ya hewa yana mchango wowote katika kusababisha magonjwa?
Leo, Machi 15, 2021 Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda wilayani Korogwe, alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salamu kutoka kwa Rais Magufuli "Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu" Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.
Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna malori (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo. Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.
Kuna madai kuwa Takukuru wameingia nyumbani kwa Kakoko leo ghafla na kumkuta na begi lenye $1,625,800 taslimu baada ya kusimamishwa kazi jana! Haijulikani hizo alizichota lini, lakini kama ni kweli inawezekana alikuwa akizichota pole pole kwa muda mrefu kidogo na huenda sasa hivi ana 'vijisenti' vingi sana huko Jersey au Switzerland kama yule mzee. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha madai haya
Hayawi Hayawi sasa yamekuwa, ilianza kama kamchezo kakuigiza kutokupeana support za kupostiana kati ya Rayvan na wasanii wenzake wawasafi lakini utetezi ukawa mwingi, Ikafuata mama yake Boss wa Rayvan kumkatia Behewa Rayvan huko Instagram yaan Mama Dangote kumunfollow Rayvan. Zikaja Event zote kubwa za wasafi Ikiwepo EP ya FOA kutopostiwa na kijana huyo Shaban Mwakyusa Almaarufu kama Rayvan na Leo hii kaamua kukata Behewa kwenye Bio yake na kuondoa Taarifa iliyokuwa ikimtambulisha kama msanii wawasafi. Inasemekana Rayvanny kaondoka Wasafi. Hii ni kweli?
Picha ambayo baadhi ya watu wanadai kuwa inamuonyesha raisi wa Urusi Vladimir Putin akitoa mafunzo kwa wapigania uhuru kusini mwa Afrika ilisambaa na kutumiwa na baadhi ya watu kuhalalisha kuwa nchi za kiafrika zinapaswa kuunga mkono Urusi katika vita vya Ukraine. Picha hiyo ilisambazwa sana mtandaoni baada ya kuchapiswa katika blogu za Zibwabwe mwishoni mwa mwaka 2018, machapisho hayo yalidai yanamuonyesha Putin katika mafunzo ya kijeshi ya Tanzania kwaajili ya harakati za kupigania uhuru katika nchi za Afrika mwaka 1973.
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia kwenye Jumatatu hii ya Pasaka , Kwamba Mheshimiwa Juma Raibu aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro , kabla ya kung'olewa hivi karibuni , ameanza kampeni kabambe ya kuondoa miundo mbinu yote aliyojitolea akiwa madarakani . Wakati wa madaraka yake alisaidia kutengeneza miundo mbinu ya maji kwenye uwanja wa Mandela uliopo Kata ya Pasua , ili kusaidia vijana wanaotumia uwanja huo , Sasa baada ya kung'olewa kwenye Umeya naye akaamua Kama Mmbwai basi iwe Mmbwai tu , kang'oa miundo mbinu yote ya maji aliyosaidia . Zipo Taarifa kwamba anapanga kung'oa mabati yote aliyosaidia kwenye mashule mbalimbali pamoja na Zahanati . Akijibu tuhuma hizo, Juma Raibu amesema: “Siwezi ondoa misaada...
Back
Top Bottom