Wamtaa huu
Senior Member
- Jan 21, 2011
- 168
- 55
Ilipata kutokea GTV.Haikudumu na ikafanikiwa kutapeli na kuingia mitini.Sasa ipo zuku,je nayo imeingia mitini?
Kwanza customer care mwenye namba 0689988688 ambaye anatambulishwa kwenye website yao kama mwakilishi wa zuku Tanzania alinidanganya!Kutokana kutokuwa na habari sahihi kutoka mamlaka husika(kwa wakati huo) November mwaka jana,nilimpigia huyu.Nilitaka kujua wao zuku kwa nini local tv nalipia.Huyu akaniambia kuwa kuanzia January sitalipia zaidi ya zile za ziada.
Pia nilimuuliza kwa nini local tv ni mbili tu.(Channel ten na TBC kipindi hicho).Huyu mdada alinijibu kuwa wapo kwenye mchakato wa kuongeza clouds tv,itv na eatv ambazo mpaka tarehe 1/1 mwaka huu zingekuwa tayari.
Nikahamasisha wenzangu tununue ving'amuzi(sijui visimbuzi!) vya zuku na tukanunua wengi huku nilipo.
Kimbembe kikaja pale tcra waliposema kuwa wenye vibali vya kurusha local tv bure ni startimes na ting tu mpaka muda huo.Niwazi kuwa huyu customer care alidanganya!Siwezi kuamini kuwa alikuwa hana taarifa sahihi kwa kuwa ni muhusika wa moja kwa moja na anajua hapaswi kutoa info ambazo hazijui!Utapeli wa kwanza.
Mpaka sasa wameongeza clouds tv tu,kinyume na ahadi kuwa mpaka mwaka mpya watakuwa wameongeza eatv na itv!Huu ni udanganyifu wa wazi ambao haupaswi kufumbiwa macho.Utapeli wa pili!
Ni wiki sasa hawapo hewani.Nilipiga simu namba 0762811810 akapokea mdada ambaye alionekana wala hajui kitu!Akampa simu mwenzake mkaka naye wala hakuwa na majibu ya kuridhisha.Eti network ipo low!Badae akabadilisha eti dish limetingishika kwa hiyo nisubiri yatarudi yenyewe.Yani dish lishtuke lakini nisubiri yatarudi yenyewe?Hata haiingii akilini.Nilifikiri ataniambia nirekebishe dish lakini alisisitiza nisubiri tu!Nikagundua kuna kitu kinafichwa.Utapeli!
Leo ni zaidi ya wiki tangu wakatike hewani na sasa simu hizo hazipokelewi!Yani namba za customer care hazipokelewi kama sio usanii ni kitu gani?Wanaendelea kunikata hela 750Tsh kila siku hata kwa muda wasipokuwa hewani kwa sababu zisizonihusu mimi mteja.Hii ni sawa kweli?Huu ni utapeli!
Nawatahadharisha mliokuwa na mpango wa kujiunga na hawa wasanii msijaribu.Sisi tumetapeliwa na hapa tumechanganyikiwa!Watu hawapokei simu na wala hawapo hewani!
TCRA nawaomba mmulike huu utapeli unaofanywa na hii kampuni ya zuku kwani waathirika ni sisi walalahoi.Tumejikuta tunakubali kulipa 20000Tsh bila kupenda na hata baada ya kujipiga bado wanatutapeli.Hawapo hewani kwa wiki moja na hawajali kutoa taarifa wala kuomba radhi kwa wateja wao.Wenzangu ambao mmetapeliwa tusilipie tena mpaka watakapotoa maelezo ya kutosha na namna watakavyotufidia pesa zetu(hata ukiviita vipesa!) kwa muda wote waliopotea hawa matapeli wa zuku tv.