Zuku ni kampuni ya hovyo kuwahi kutokea, nimewachukia mno hawa jamaa washenzi sana!

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,642
3,483
Usishangae wala usitahamaki maana kwa ujinga walio nao hapo sijawatukana kabisa. Nimewaita washenzi hapo ili kupunguza ukali wa maneno tu lakini nilitamani nitumie maneno zaidi ya hilo kabisa

Hawa watu king'amuzi kimezingua nikawapigia kuwauliza nijue tatizo ni nini. Sasa kwa maswali aliyouliza juu ya ninachoona huku kulingana na maelekezo yake na majibu niliyotoa, mhudumu akajiridhisha kwamba king'amuzi kimekufa.

Akaniambia kuwa nilipie kifurushi cha juu kisha nipige simu nitumiwe king'amuzi kingine. Nikalipa chap na kupiga simu, wakasema kwa njia za kawaida itachukua wastani wa wiki mbili kupokea king'amuzi changu na kama nitahitaji haraka basi niwatajie basi la kwetu wakala wao hapo mjini atanipigia ili anitumie lakini nauli juu yangu

Niliwaambia kwamba mimi nipo tayari kwa njia yoyote tu ilimradi nipate hicho king'amuzi. Ebwana tangu mwaka jana hiyo hadi leo hii sijapata king'amuzi. Simu nikipiga huduma kwa wateja wanatoa majibu yao wanayoyajua wao na kwa yule wakala wao napata majibu mengine anayoyajua yeye

Huko kote nilishapuuza kabisa nikaamua kufanya kama nimesahau vile ila sasa kilichoniudhi ni hiki cha kunipigia na kuniambia ving'amuzi viliisha stoo ila sasa vipo nitume nauli; nikawaambia situmi nauli ila kuna mtu hapo mpeni nikawaunganisha na mtu pale Dar wamkabidhi. Wakamzungusha wee na mwishowe akaambulia patupu. Hilo pia baadae nikaona labda niwachukulie udhuru nipotezee tu

Sasa kubwa kuliko ni juzi nikawaambia anakuja mtu ofisini kwenu kufuata huo mzigo wakasema atupigie kabla hajatoka ili asije kuchoma mafuta ya bure. Jamaa akawapigia akataja details nilizompa na wakamwambia njoo hakuna tatizo. Kufika jamaa ananipigia anasema hebu ongea nao hapa maana siwaelewi, kidada kinaniambia mbona stoo hakuna ving'amuzi nikakiwakia kwamba nyinyi si mmemwambia aje!

Kuona hivyo wakaamua kutumia kitu inaitwa KUMTOKA. wakanidai eti nitaje namba ya akaunti nikitaja ya king'amuzi akaikataa nikataja hizo tarakimu 6 walizonipaga nikalipia bado wanazikataa eti siyo hiyo. Nikamwambia yule jamaa aondoke aachane nao wababaishaji hawa

Nimejitahidi kupunguza maelezo lakini bado naona paragraphs zinakuwa nyingi basi acha tu niishie hapa ila ZUKU NAWACHUKIA kinoma... halafu nimeona wameanza kujipendekeza na meseji zao sasa sijui za nini wakati king'amuzi kipo kwao

Kampuni zingine hizi njaa tu!
 
pesa ngumu kiseng***Kwa watz mambo ya delivery bado sana, huduma mbovu, ulichoagiza na unacholetewa tofauti kwa ubora,,,ama utapeliwe kabisa ! Pole Masta
 
Biashara ya visimbuzi kwasasa imeshakuwa ngumu baada ya AzamTV kuteka Soko lote la Bongo

Kwahiyo Kampuni nyingi zinajiendesha Kwa uzoefu tu

Ndiyo maana Marehemu Mzee Mengi aliposoma alama za nyakati, akaamua kutoendelea na biashara ya ving'amuzi vyake vya DidiTek 🙌
 
Zuku Kuna channel gani za maana!?huenda Kuna uhondo tunamisi kung'ang'ana na Azam tv na "haya ni maajabu"
 
Back
Top Bottom