abdulrahim
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 408
- 286
Habari wanajamii!
Binafsi sio shabiki wa mchezo wa miguu ila ni mdau mkubwaa wa maswala ya michezo kwakuwa mashindano ya michezo yanaleta burudani, Afya njema na kutoa ajira na kuinua vipaji kwa vijana wetu.
Nimesikitishwa saana na Barua ya M/Kiti wa mashindano ya Sports Extra Ndodo Cup ya trh 15.07.2017 ikiwajulisha wapenzi na mashabiki wa mashindano hayo kutofanyika kwenye viwanja vya Bandari Temeke.
Hili limeniuma saana, Limenikwaza saana na limenikereketa saana wallah!
Kwa kumbukumbu yangu Bw. Shafii Dauda wiki iliyopita alitoa taarifa kwamba mechi zote zitafanyika baina ya viwanja viwili kwa kuzingatia maeneo ambapo team zinatokea. Alibainisha ni kiwanja cha Kinesi( Kinondoni ) na Bandari (Temeke) ambacho ukarabati wake umekamilika na tayari kwa matumizi.
Ukaguzi wa uwanja ulikwishafanyika na walikubaliana mpaka kufikia hatua ya kujuzwa sisi wanajamii.
Taarifa ya leo imenitia mashaka saana na kunipa dhana hasi juu ya aina ya watu wanaosimama kwaajili ya wengi tulio chini.
Mimi ni mwanachama na mpenzi wa chama cha mapinduzi pia ni Mkereketwa mkuu na mpenzi we serikali ya awamu ya tano. Noamba yafuatayo yafanyike kwa haraka ili kunusuru hili;
1. Kufanyika mashindano ya Ndondo CUp uwanja wa bandari uliokarabatiwa na kuwa na hadhi yake kwasasa ni mwanga wa kuonyesha kwamba soka la mchangani limepanda thamani, hivyo wahusika wakuu wa michezo ngazi ya wilaya temeke mpaka Taifa wanahitajika kutupa majibu ya ni kwanini mashindano hayo hayatafanyika kwenye uwanja huo?
2. Binafsi zuilio hilo nalihusisha kwa karibu saana na upinzani/kupishana kwa waandaaji(Clouds media) na aliyesimamia na kutafuta wadhamini wa ukarabati wa uwanja huo ( Ndg. Paulo Makonda). Mamlaka za juu zinazosimamia michezo( Wizara ya Habari,Utamaduni na michezo) zitolee ufafanuzi zaidi juu ya hilo kwani kwenye hili kila mmoja amekamilisha wajibu wake..Mkuu wa mkoa kutafuta wadhamini wa kuukarabati uwanja ndio ni kazi yake alipaswa kulifanya hilo na waandaji pia wamefanya kwa eneo lao.
3. Kwa hali yeyote ile zuio hilo halina nia njema kwa ukuaji wa mchezo wa mpira nchini Tanzania bali ni kukwamisha na kurudisha nyuma jitihada za wanopenda kuona soka ya Bongo inanyanyuka. Hivyo Mamlaka husika zisisite kutuma wataalamu wake na kuruhusu haraka uwanja ule kutumika kwa mashindano haya pendwa mtaani.
4. Michezo ni kinga dhidi ya madawa ya kulevya. Eneo la TMK ni eneo moja wapo ndani ya mkoa wa Dar es salaam lilioathirika zaidi na madawa ya kulevya hivyo kuondoa burudani hii ni kuondoa fursa za vijana wengi kwenye eneo hilo kiasi kwamba muda ambao wangeutumia kupata burudani hiyo na wengine kuudha bidhaa zao halali wa watazamaji basi wengi watautumia kufanya yale yasiyofaha.
Mwisho Kabisa.. Serikali ni baba na Mwananchi ni mtoto, Baba hahitaji kusifiwa wakati analea mwanae ila baba husifiwa pale mwanaye anayemelea anapotoa matokeo chanya kwa jamii..
Wenu Mkereketwa!!
CEO ChailoCoffeeShop
CC; Anko @EdoKumwembe @ShafiiDauda mwakyembe