Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,118
- 62,845
ZOMBIE NA VAMPIRE NI JAMBO HALISI, SIO MAIGIZO KAMA WENGI MUONAVYO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Bila Shaka wengi wetu tumewahi kuziona filamu za Mazombi na Vampire, na ambao hamajwahi kuziona basi mnaweza kuzitafuta Baada ya kusoma andiko hili.
Kuna watu huniuliza na kuniona Mbona Huyu Robert ni kijana mdogo lakini anaakili nyingi( Kwa muono na mtazamo wao) amewezaje kuwa hivyo alivyo. Kwa ufupi nipo hivi Kwa sababu zifuatazo;
1. Napenda kuangalia wanyama na tabia zao Kwa sababu Tabia za hao wanyama naziona katika Maisha ya wanadamu.
2. Nilipenda na kuishi na Wazee, Bibi na Babu. Hii iliniongezea maarifa na ufahamu Kabla sijawa mtu mzima.
3. Napenda kuwafuatilia Watoto(Akili na tabia zao) Hii hunifanya niishi Kwa Imani na kutokuweka vitu moyoni.
4. Napenda kusoma na kuandika. Hii huijenga Akili na ufahamu wangu.
5. Napenda kuangalia Filamu Hasa Filamu zinazotisha kama Mazombi na Vampire Kwa sababu ule ndio uhalisia WA Maisha ya Mwanadamu. Pia napenda kuangalia katuni.
Lakini Kwa Leo nipo kwaajili ya kuelezea uhalisia WA Mazombi na Vampire katika Maisha yetu ya kila Siku.
Concept ya filamu za Mazombi na Vampire ni halisi tofauti na wengi wanavyoichukulia. Ile sio simulizi na filamu za kubuni. Matukio ya kweli yanayoelezewa Kwa Akili kubwa ambayo Watu wenye upeo mkubwa huelewa.
Watu wazima na Vijana wote mnaotafuta Maisha katika filamu za kutazama basi nawasihi mtazame filamu za Mazombi na Vampire.
Iko Hivi;
(Mkanda wa Filamu ya Maisha yako unaanza kuonyeshwa katika Luninga. Watazamaji tupo lakini pia ni sehemu ya watazamaji wa filamu za wengine ingawaje kuna muda mnaingilia. Muongoza na mtunzi wa filamu hamumjui na hamjawahi kumuona lakini mnaamini naye ni sehemu ya Watazamaji na muongoza filamu) Filamu inaanza;
"Unazaliwa ukiwa hujui ulikotoka, hujijui wewe ni nani, na huwajui waliokupokea, na hujui ulipo. Upo Uchi na haujui upo uchi. Ni mtoto mchanga"
(Filamu inaonyesha waliokupokea wanafurahia na kukupakata Kwa upendo, lakini ugeni wa Mazingira na Wahusika hao(wazazi au walezi) unakutisha. Unalia nao wanahangaika kukubembeleza)
" Welcome to the World New Angel. Sisi ni Wazazi wako, usiogope. Sisi ni jamii ya binadamu kama wewe. Usiogope. Labda hi ni harsh reality ya Maisha yetu, tumboni ilikuwa Kwa muda tuu, Huko ulifanyiwa kila kitu na Kupata dezo. Haya vaa kiguo hiki"
(Unavalishwa, matambara labda ni kanga au vitenge, kisha unabembelezwa Kwa nyimbo)
" Kila kitu haukielewi, yote kwako ni mapya. Lugha Mpya, Watu wapya, Dunia Mpya, kila kitu kwako ni kipya. Akili yako Jambo la Kwanza kulisajili ni Woga na hofu Kutokana na ugeni uliokuwa nao. Hofu! Hofu! Hofu ya uhalisia"
Taikon unazungumzia mambo gani siku ya leo. Kwa nini huwezi kufupisha? Unakuwa kama sio Msomi!
Nisikie, Maisha hayanaga kifupi, ukweli haunaga kifupi. Uhalisia ni mchakato unaohitaji muda.
" Umekua umeshaanza kuyazoea mazingira, wale walioandaliwa kukuleta utakaowaita wazazi na wale walioandaliwa kukulea utakaowaita Walezi wameshakutoa hofu yote, na wanakufundisha kujitegemea, naam jitegemee, jiweze, ujifanyie mambo yako mwenyewe pasipo kutegemea MTU mwingine ikiwemo wao wenyewe. Unakua Kwa kujiamini Kwa sababu unaamini kila uambiwacho na unaamini Yule aliyekuleta Duniani Mama na Baba ndiye Mkubwa na anauwezo kuliko Wahusika wengine"
Filamu inaacha kuonyesha matukio yako inakuonyesha ukiwa umekaa kwani bado hujaweza kusimama wala kutembea, unasinzia lakini Hali hiyo huijui, unaiogopa unahisi Jambo Baya usilolijua hasa ukiwa unafumba macho, unaanza kulia. Mama au Mlezi anakuja anakubeba ati unausingizi, "kumbe huu ndio usingizi" Mama anaimba ili ulale;
" Lala mwanangu, lala mikononi mwangu,
Safari Hii tangu, ukiwa tumboni mwangu,
Lala kitoto changu, wewe uliye lango langu
Utimize ndoto zangu, upaapo katika wingu"
Papo hapo filamu inaonyesha angani kwenye mawingu na nyotanyota nyingi. Kisha kunakuwa na Giza na Sauti ya wadudu wa Usiku.
Filamu inaendelea
" Baadaye hofu iliyoondolewa inarudishwa tena, unaambiwa Ile Dunia uliyoambiwa usiogope, sio Ile. Unaambiwa Dunia ina Watu wabaya na Wema. Lakini wewe wanakuambia uchague kuwa MTU Mbaya. Wanakuambia, ukae mbali na Watu wabaya Kwa sababu wao ni Watu wala Watu. Chakula Chao ni nyama za binadamu wenzao, kinywaji Chao ni Damu za Watu wenzao. Huteka ndoto za wenzao na kuzichukua na kuzifanya zao, huiba Maoni ya wenzao na kuwaua"
" Wanakuambia waepuke hao Watu wabaya, usikae karibu Yao, wala wasikukaribie Kwa sababu mate Yao yanasumu, wakikung'ata watakuambukiza ubaya wao. Nawe unakuwa Mbaya kama wao. Wanataka uwe Mbaya kama wao na kama hutaki wanakugeuza chakula chao"
Bado hujamuelewa Taikon? Sijakuelewa Bwana!
" Niliona haya kwenye filamu, binadamu akila nyama za wanadamu wenzake, tena huwakimbiza Kwa hamu isiyo na nidhamu, huwarukia na kuwang'ata" Akili yako itakuambia. Wazazi wako watakuambia, hiyo uliyoiona sio filamu, hayo ndio Maisha halisi.
Msikilize Taikon,
Binadamu wabaya ambao ni kama Mazombi na Vampire hawataki kuona unakuwa na Maisha mazuri, wao wanataka aidha wakukule au ufanane kama wao.
Kuna Watu Kwa vile wao wameshindwa katika Jambo Fulani, basi wanataka na wewe ushindwe, watakukimbiza na kukufanyia kila Aina ya hila na njama wakung'ate ili wakuambukize Kushindwa kwao, huo ndio uzombi na u-vampire.
Mazombi na Vampire wamejaa Pale Kariakoo, hapo ofisini unapofanyia kazi, makanisani, misikitini, Mashuleni, hospitalini, Huko mabarabarani. Huko kote yapo Mazombi na Vampire. Wanataka wakung'ate usifanikiwe, uwe Zombi kama wao.
Huenda pia na wewe ni Zombi na vampire mnyonya damu na Maisha ya wanadamu wenzako. Hutaki kuona wenzako wanaofanikiwa na kuwa Maisha mazuri. Unataka uwang'ate ili wawe Zombi kama wewe.
Hiyo ndio Concept ya Filamu za Mazombi na Vampire ambapo sio picha za kubuni Bali ni uhalisia WA Maisha.
Zingatia Mazombi hayawezi kupona Kwa sababu uzombi unaishi ndani Yao. MTU akishang'atwa na Zombi hubaki kuwa Zombi miaka yote.
Dawa kuu ya Zombi ni aidha kukaa naye mbali au kulikatilia MBALI.
Taikon Leo sina la ziada, Leo sitaki maswali wala majibu. Nilichokikusudia nimeifanya.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam