Kwa uzalendo wa hali ya juu na kuthamini vya kwetu, ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu wakichafua mazingira kwa kutupa taka hovyo, hasa kandokando ya mito inayoingiza maji katika Ziwa Rukwa.
Katika maeneo kama Makongolosi kwenye Mto Makongoso, Kipoka na mingine, imekuwa kawaida kukuta malundo ya taka katikati ya mto au kwenye kingo za mito, huku mamlaka husika zikiwa kimya.
Cha kushangaza zaidi, watu wanaotupa taka hizo wanajulikana, lakini hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa dhidi yao. Ikiwa hali hii itaendelea, Ziwa Rukwa litafunikwa na taka, na tutaathirika kwa kupoteza mazao na faida nyingi zinazotokana na ziwa hili muhimu.
Watanzania, ni wakati wa kuthamini rasilimali zetu. Kuna mataifa yanayohangaika hata kupata dimbwi dogo la maji kwa ajili ya ufugaji wa viumbe hai, lakini sisi tunaharibu rasilimali tulizopewa.
NEMC na serikali kwa ujumla, chukueni hatua stahiki kuzuia uharibifu huu. Tuliokoe Ziwa Rukwa