mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,310
- 6,544
Hotuba ya Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kwa Kamati Kuu Juu ya Hali ya Siasa Nchini Tanzania
Ndugu Mwenyekiti wa Chama Taifa,
Ndugu Makamu Wenyeviti, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar
Ndugu Katibu Mkuu
Ndugu Manaibu Makatibu Wakuu
Ndugu Wajumbe wa Kamati Kuu
Leo tunakutana kwenye Kikao Maalumu cha Kamati Kuu kujadiliana kuhusu ajenda mahususi mbili – Kupokea Taarifa ya chaguzi za kata 43 na Ushiriki wetu kwenye chaguzi ndogo za Ubunge na Madiwani. Katibu Mkuu aliona ni vema kujadili kwa mapana hali ya kisiasa ya nchi yetu hasa ukizingatia kuwa tunakutana mwishoni mwa mwaka. Hii itatupa nafasi ya kujipanga vizuri kwa mwaka 2018. Lakini pia inajulikana kuwa "hali ya nchi" (siasa na uchumi).
Tumekuwa na Kamati Kuu 4 mwaka 2017, ikiwemo mafunzo ya itikadi tuliyofanya kule Kahama, hivyo sitarudia maelezo tuliyoyatoa huko nyuma kwani ni sehemu ya kumbukumbu za chama na ninaamini Sekretarieti itaweza kuyaweka vizuri kwa mtiririko wake kama kumbukumbu za rasmi za chama na nyaraka rejea kwa ajili ya maamuzi mbele ya safari.
Hivyo tutatazama matukio ya kuanzia mwezi Oktoba tangu kikao chetu cha mwisho cha Kamati Kuu na kuyachambua kisha kutoa mwelekeo wa Chama, kukwepa mawimbi hayo na kusonga mbele katika harakati za kuimarisha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi nchini. Pia tutatazama maeneo machache kuhusu hali ya uchumi wetu hususan usimamizi wa Fedha za Umma na miswada inayotarajiwa kupelekwa bungeni kutungiwa sheria.
Hali ya Siasa Ndani na Nje ya Chama Chetu
Kati ya Mwezi Oktoba na sasa kumekuwa na mtikisiko kwenye mfumo wetu wa Demokrasia kwa kushuhudia wimbi kubwa la wanachama wa vyama vya upinzani wakijiunga na chama tawala. Tumeshuhudia wabunge waliochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 wakiachia majimbo yao na kujiunga na chama tawala (pia mbunge mmoja kutoka chama tawala na kujiunga na chama cha upinzani).
Kabla ya hapo madiwani waliachia nafasi zao na kubadili vyama kwenda chama tawala. Chama chetu kimepoteza wanachama waandamizi kadhaa wakiwemo wenzetu tuliowahi kuwa nao kwenye Kamati Kuu hii. Miongoni mwao ni Profesa Kitila Mkumbo, Anna Mghwira, Albert Msando, Samson Mwigamba na Edna Sunga.
Msando, Kitila na Mghwira walikoma kuwa wajumbe wa Kamati Kuu katika vipindi tofauti kabla ya kuhama kwao. Edna na Mwigamba walihama wakiwa ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama chetu. Kiukweli hili limeleta taharuki kwenye chama chetu na kwenye nchi yetu kwa ujumla. Watu mbalimbali wanahoji nini kinaendelea kwenye siasa za Tanzania?
Ninawashukuru sana wajumbe wa Kamati Kuu kwa utulivu wa hali ya juu katika kipindi hiki. Utulivu umeonyesha ukomavu wetu wa kisiasa licha ya mawimbi haya tunayopita. Pamoja na kwamba wenzetu walioamua kutuacha na kujiunga na vyama vingine wanaendelea kutushambulia kwa namna moja au nyengine, sisi tuendelee kuwa watulivu na kutazama mbele namna ya kujenga chama chetu.
Takribani watu wote wanaoondoka kutoka vyama vya upinzani kwenda chama tawala wanasema wanaunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Tawala katika uendeshaji wa nchi yetu. Hii sababu haitoshi kueleza maamuzi yao, hususan kwa wale wanaotoka chama chetu cha ACT Wazalendo. Naomba niwakumbushe kuwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama kilichoketi Jeshi la Wokovu Aprili 2016 tuliazimia masuala ambayo chama chetu kinaweza kuunga mkono Serikali au chama kingine na masuala ambayo kamwe hatuwezi kuunga mkono.
Naomba Kunukuu; "Chama chetu cha ACT Wazalendo ni lazima kiendelee kuunga mkono juhudi zozote za kuondoa ufisadi nchini kwetu. Hata hivyo Chama chetu ni lazima kiendelee kukosoa Serikali pale ambapo tunapoona mambo hayaendi sawa. Tusiogope kuikosoa Serikali kwa hoja, kwani kukosoa Serikali ni tukio muhimu sana la kizalendo. Narudia tusiogope kukosoa Serikali kila inapobidi". Mwisho wa kunukuu.
Hili pamoja na mambo mengine yalikuwa maazimio ya Halmashauri Kuu ya mwisho ya chama chetu. Hivyo wanachama wa chama chetu wanaohama chama eti kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais hawana sababu kwani wangeweza kuunga mkono wakiwa ndani ya chama. Mimi kama Kiongozi wenu wa Chama nimefanya hivyo mara kadhaa, kusifia pale ninapoona panafaa na kukosoa pale ninapoona hapafai. Ni dhahiri kuwa wenzetu wana sababu zaidi ya kumwunga mkono Rais, kuna ambao sababu ni vyeo walivyopewa, na wengine ahadi za vyeo watakavyopewa.
Lakini ni lazima tujiulize maswali magumu sisi wenyewe na kuzungumza tukitazamana machoni, je hakuna sababu za ndani sisi wenyewe zinazokimbiza wanachama wetu? Kama zipo ni zipi? Je ni sababu ambazo tunaweza kurekebisha na kukiimarisha chama? Kama ni sababu zilizo nje ya uwezo wetu tunafanya nini ili kuzikabili? Je bado sisi tunaamini katika misingi ya Chama kwa mujibu wa Azimio la Tabora? Tulikuwa kundi tu tulioumizwa na vyama tulivyokuwamo na tukaamua kuunda chama kupoza hasira zetu tu na sasa hasira zimeisha hakuna sababu ya chama kuwapo?
Katika baadhi ya Waanzilishi wa Chama, wawili wamerudi CCM. Hii hairutubishi hoja kuwa Chama chetu kilikuwa mradi tu wa CCM na sasa mradi hauna maana tena na hivyo CCM inavunja mradi wake? Hili la mwisho mtaweza kusema mbona CHADEMA na CUF wanakwenda CCM, labda mradi huo ulihusisha baadhi ya wanachama wa vyama vingine vya upinzani. Lakini kwanini watu hawatoki TLP, UDP, NRA nk na kujiunga na CCM? Haya maswali ni lazima tuyajibu kwa ukweli wa mioyo yetu ili kuweza kujisahihisha kama tuna makosa yetu wenyewe.
Mimi binafsi, ndugu Wajumbe, kwa hakika ya moyo wangu ninaamini katika misingi ya Chama hiki. Niliacha ubunge miezi 9 kabla ya muda wangu kwisha kwa sababu ya kuamini katika 'Muvumenti' hii tuliyoizindua tarehe Machi 29, 2015. Wenzangu wawili tulioanzisha nao Chama hiki walikuwa hawaamini kuwa hatimaye nitajiunga na chama.
Nakumbuka Katibu Mkuu wetu wa kwanza alikuwa na wasiwasi kuwa nitawageuka na sitaondoka CHADEMA. Hii ni kwa sababu mara zote nilikuwa nawauliza wenzangu kama kweli tunaamini katika 'Muvumenti' hii na wao wakidhani sitaki kujiunga na Chama. Nyaraka ya kwanza Chama hiki kuzalisha ni misingi 10 ya Chama, na 'Statement of Objectives (Dibaji) ya Chama ni ya kimapinduzi kweli kweli. Ninaomba kuinukuu Dibaji hiyo kwa msisitizo unaostahili;
"KWA KUWA tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, ufisadi, uzembe na uvivu;
NA KWA KUWA tumeamua kuhakikisha kuwa maliasili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na kuleta maendeleo sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa;
NA KWA KUWA tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na kwa kuzingatia misingi ya haki kwa watu wake wote;
NA KWA KUWA tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili
kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Mwafrika na kujenga bara lenye sauti yenye nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa ulimwenguni;
NA KWA KUWA tumeamua kupigania demokrasia, umoja, utu, uadilifu,
uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa;
NA KWA KUWA kwa nia moja tumeamua kujenga Chama chenye kufuata misingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic Socialism ), na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) ikiwemo Azimio la Arusha; na
NA KWA wajibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na
utamaduni wa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania;
HIVYO BASI; Sisi Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha
Wazalendo (ACT Wazalendo) uliofanyika Dar es salaam leo tarehe 28 Machi 2015, tumepitisha KATIBA MPYA ya Chama chetu itakayojulikana kama KATIBA YA ACT Wazalendo YA MWAKA 2015”. Mwisho wa kunukuu.
Wenzetu hawakuwa wanaamini katika maneno haya? Kwa Dibaji ya kimapinduzi namna hii (mimi huwa nikiisoma nasisimka mwili), unawezaje kuhama chama kama hiki na kusema unaunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa chama kingine ambaye ametokea kuwa Rais wa nchi. Je tuliobakia tunaamini katika maneno haya mazito yanayoapiza, "kulinda utamaduni wa vyama vingi"? Huu sio wakati wa kulishana yamini kwenye misingi ya 'Muvumenti' yetu? Tuendelee tu na maneno 'tunawatakia kila la kheri' wenzetu wanapotuacha?
Ndugu Wajumbe,
Kwenye Halmashauri Kuu ya mwisho ya chama nilizungumza namna tunapaswa kufanya siasa tofauti kulingana na wakati wa sasa? Nilisema "Ni lazima tuwe innovative (wabunifu) katika Siasa. Tusifanye siasa za kila siku". Hili ni jambo la kujiuliza na kujihoji ni kwa namna gani tunafanya siasa tofauti. Inawezekana wenzetu wanaona tunafanya siasa zile zile za miaka yote na hivyo wameamua kutafuta aina mpya ya siasa.
Leo nitawapa mfano wa wanasiasa wenzetu wa upinzani katika nchi ya Venezuela, ambapo Rais Mjamaa mwenzetu, ndugu Nico Maduro, kamaradi, amezuia vyama kushiriki uchaguzi. Wakati wa Rais Chavez vyama vya upinzani na wanasiasa wa upinzani walikuwa wanabanwa kweli na Serikali. Hii tunayofanyiwa na Magufuli ya watu kufungwa na kuachiwa, kupigwa, kuzuia mikutano, kukamata watu wanaomkosoa kwenye mitandao ni cha mtoto.
Mwandishi William Dobson aliandika kitabu mwaka 2012 kiitwacho 'Dictator’s Learning curve: Inside the global battle for democracy'. Katika kitabu hiki alimhoji Meya mmoja wa chama cha upinzani katika mji mmoja masikini kabisa kuhusu siasa tofauti. Meya Carlos Ocariz wa Mji wa Petare alimshinda mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Rais Chavez. Rais Chavez akaamua kukata fedha kwenda kwenye mji huo, akaondoa magari ya takataka na kukata maji.
Meya Ocariz anasema, "sikuanza kulalama na kupiga kelele. NIliamua kufanya tofauti na kutekeleza masuala ya maendeleo yaliyo ndani ya uwezo wangu kwenye mji wangu. Kuhakikisha watu wangu wanapata maji nilitumia magari ya Mji kusambaza maji kwenye nyumba za watu. Nilizuia matumizi makubwa ya ofisi na kupeleka fedha kuzoa taka na kuanza kuwalipa wazazi ili wapeleke watoto shuleni".
Meya Ocariz akaendelea; "Upinzani tunalalamika lalamika tangu mwaka 2000, tunapata nini? Badala yake tuwaonyeshe wananchi tofauti ya siasa zetu na za Kamaradi Chavez. Tutatue matatizo ya watu".
Kwa kimombo anasema; "we must offer true political alternatives to Chavez, solving problems and not just complaining about how we are treated in the system that almost everyone agrees is unfair".
Ndugu wajumbe, sisi tuna maeneo tunaongoza, ama Vijiji, Kata au Manispaa. Sisi pia tumekuwa tukisema kuwa tunataka kufanya siasa tofauti. Je inawezekana tumeshindwa kufanya hivi ndio maana baadhi ya wenzetu wanaondoka na kutuhama? Ninatoa rai kuwa tujitafakari kwa kina sababu za ndani za mawimbi haya ya kisiasa na tupate majawabu ya namna ya kusonga mbele.
Hali ya Uchumi wa Nchi
Ndugu Wajumbe,
Mtakumbuka kuwa mara ya mwisho tulipokutana tulichambua Hali ya Uchumi wa nchi yetu na kuonyesha kuwa uchumi wa nchi yetu ulikuwa unasinyaa na kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kufuatia uchambuzi wetu, mimi Kiongozi wa Chama, Mwenyekiti wa Chama na Katibu Mkuu tulihojiwa na kitengo cha makosa ya kifedha kwa makosa ya sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mitandao. Polisi bado wanaendelea na uchunguzi wao. Walichukua kompyuta za ofisi na simu yangu ya mkononi kwa ajili ya uchunguzi wao.
Juzi, Disemba 13, 2017 Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeitaka Serikali itazame upya vyanzo vyake vya takwimu za uchumi ili kupata picha halisi ya Hali ya uchumi wa Taifa letu. IMF wamethibitisha kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania unashuka, kutokana na viashiria vingine vya uchumi, na kwamba takwimu za Serikali ni lazima zitazamwe upya. Tunatarajia kuwa Jeshi la Polisi litaachana na kesi wanayotarajia kuifungua dhidi yetu, na kutuacha vyama vya siasa kuendelea na uchambuzi wa shughuli za Serikali kwa uhuru.
Jambo moja muhimu ambalo watu wa IMF wameiambia Serikali ni suala la kuheshimu Bajeti. Mtakumbuka tulieleza katika kikao kilichopita kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza tabia ya kutumia fedha za Mashirika ya Umma bila kufuata taratibu za sheria. Kwa mfano mapema katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali ilipewa gawio la shilingi bilioni 300 na Benki Kuu ya Tanzania kutokana na faida ya benki hiyo mwaka 2015/16 ( tazama uk 67 wa Taarifa ya Benki Kuu Bank of Tanzania: Publications and Statistics EconomicAndOperationsAnnualReports/BOT%20ANNUAL%20REPORT%202015-16.pdf ).
Serikali haikutoa Taarifa juu ya gawio hili popote kwenye Taarifa za Fedha, mapato haya hayakupelekwa Bungeni kugawiwa kwa mujibu wa sheria na Rais aliamua kutumia fedha hizi kulipia Mkandarasi wa Ujenzi wa Airport ya Chato na madeni ya ndege za Bombardier na Boeing bila kufuata taratibu za sheria za fedha na bila CAG kuidhinisha kwa mujibu wa Katiba.
Utaratibu unataka fedha kuingia kwenye Mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kisha kuidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ndipo Serikali kuanza kutumia. Shilingi bilioni 300 kutumika na Serikali bila kushirikisha Bunge na kufuata sheria za nchi ni kusigina Katiba na kudharau Taasisi za Uwajibikaji za nchi yetu.
Ninashauri Kamati Kuu ya Chama itoe Azimio kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalumu wa fedha hizi na kutoa Taarifa kwa Bunge na Bunge liwachukulie hatua kali Maafisa wote wa Serikali waliokiuka sheria bila kujali vyeo vyao. Jambo hili likiachwa litaleta matatizo makubwa huko mbeleni. Tunao mfano wa nchi ya Msumbiji namna ilivyopata matatizo kutokana na matumizi ya fedha za umma bila kupata idhini ya bunge na kinyume na bajeti.
Nafasi ya Chama chetu juu ya Miswada inayokwenda Bungeni mwaka 2018
Ndugu Wajumbe,
Moja ya ajenda kubwa ya Chama chetu ni Hifadhi ya jamii. Chama chetu kinataka haki ya hifadhi ya jamii kwa kila raia ili kuwa na Taifa ambalo raia wake wote wana bima ya afya na uhakika wa pensheni uzeeni. Katika ilani ya Uchaguzi ya Chama chetu tuliahidi mabadiliko makubwa ya mfumo wa hifadhi ya jamii ikiwemo kuunganisha mifuko iliyopo na kubakia na mifuko 3 tu (miwili mifuko ya pensheni na 1 mfuko wa Taifa wa bima ya afya).
Serikali imeamua kutekeleza wazo letu hilo na tayari muswada wa sheria ya hifadhi ya jamii umewasilishwa bungeni kwa ajili ya kuanza kufanyiwa kazi na kuunda mifuko miwili tu. Tunapongeza hatua hii ya Serikali kuchukua mawazo yetu na kuyafanyia kazi. Hata hivyo muswada unaopendekezwa bungeni una matatizo makubwa ambayo yanaweza kusababisha wazee wetu 120,000 kukosa kabisa pensheni, hasa watakaoanza kustaafu mwaka huu na waliokwishastaafu tangu mwaka 1999.
Jambo hili ni la kihistoria kidogo, nitaeleza. Serikali mwaka 1999 iliunda Mfuko wa PSPF kwa ajili ya watumishi wa umma. Kabla ya mwaka 1999 Watumishi wa Umma walikuwa hawachangii pensheni zao bali walikuwa wanalipwa pensheni kutoka Hazina moja kwa moja kupitia bajeti za Serikali za kila mwaka. Hii ndio sababu wastaafu wetu nchini wanapokea pensheni ndogo sana ya shilingi 50,000 tu kwa mwezi.
Serikali ya Rais Mkapa iliamua kuunda Mfuko wa Pensheni ili kuboresha pensheni za watumishi wa umma. Hata hivyo, Serikali ilitakiwa kulipa michango ya wafanyakazi wote walioajira kabla ya mwaka 1999 (pre 1999). Serikali ya Rais Mkapa ilikubali deni lakini haikulipa. Serikali ya Rais Kikwete ilifanya uhakiki wa Deni na kukubali kulipa lakini haikulipa. Serikali ya Rais Magufuli imeamua kutolipa kabisa kisheria. Taarifa ni kuwa Serikali imeamua kuachana na madeni haya, na hivyo wastaafu 120,000 wa Tanzania wako hatarini kutolipwa pensheni kabisa, mara tu baada ya muswada huu mpya kupita na kuwa sheria.
Vile vile muswada wa sheria hii unabadilisha kanuni ya mafao, na hivyo kuathiri Walimu wetu wote nchi nzima ambapo pensheni zao zitakatwa kwa 50%. Jambo hilo litakuwa na athari kubwa mno kwa walimu nchini.
Niiombe Kamati Kuu iazimie kuwa Chama chetu kianze kazi ya kuhamasisha makundi ya vyama vya Wafanyakazi nchi, kuungana na kusimama pamoja kupinga Mswada wa Sheria hii, hasa ulivyo sasa. Kwa kuanzia ni muhimu kuzungumza na Chama cha Walimu Tanzania, maana wao ndio waathirika wakubwa wa sheria hii. Lengo likiwa ni mswada huu usiende Bungeni ili iboreshwe na kulinda maslahi ya wazee wetu wastaafu.
Chama pia kiitishe mijadala wa wazi kwa mfumo wa makongamano ili kujadili sheria mpya ya pensheni na kujiunga na vyama vya wafanyakazi kuboresha muswada ili kutunga sheria inayohakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na haki ya Hifadhi ya jamii. Kamati zetu za Sera na Utafiti, pamoja na Sheria na Katiba zitakuwa na wajibu mkubwa sana wa kusaidia uandikwaji upya wa sheria hii. Tuwe mstari wa mbele kwenye jambo hili.
Muswada mwengine ni muswada wa Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa nchini, miongoni mwa miswada mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini, muswada ambao ukiachwa kama ulivyo na ukawa sheria basi utafuta siasa za vyama vingi nchini.
Maana ni muswada unaompa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini mamlaka ya Udhibiti na Uendeshaji wa Vyama na kupoka mamlaka hayo kwa Vyama vyenyewe kupitia wanachama. Hata zuio haramu la mikutano ya hadhara nchini limewekwa kisheria katika mswada huo. Tunao wajibu wa kuviunganisha vyama vyote vya siasa vya Upinzani nchini, kupinga muswada huu.
Miswada hii miwili, ya Pensheni ya Vyama vya Siasa inahalalisha Siasa zetu za Uchumi na Haki za Raia. Mswada wa Pensheni utaharibu maisha ya Watanzania wenzetu 120,000 pamoja na wategemezi wao, utaua kabisa uchumi wao. Na mswada wa vyama vya siasa utapoka kabisa mamlaka na haki za raia katika siasa zetu za vyama vingi. Chama chetu kina wajibu mkubwa kwenye masuala haya.
Hitimisho:
Ndugu Wajumbe,
Sikuzungumzia kabisa masuala ya Uchaguzi pamoja na ukiukwaji wa haki kwenye chaguzi hizi za marudio katika kata 43 nchini kwa sababu hiyo ni ajenda ya Sekretarieti katika kikao hiki. Naamini tutaijadili vyema baada ya kupokea taarifa yao, taarifa yangu ililenga mjadala wa jumla kuhusu hali ya siasa na uchumi wa nchi yetu (Hali ya Nchi).
Naomba kuwasilisha waraka wangu huu, na naamini tutaujadili kwa kina. Nawatakia Kikao chema cha Kamati Kuu na Maazimio yenye maslahi ya wananchi wetu walio wengi, pamoja na kuhakikisha Chama chetu kinavuka mawimbi haya na kuwa chama bora kabisa.
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Disemba 16, 2017
Dar es salaam