Zitto Kabwe yuko kimya ishu ya January Makamba

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,199
Tunayoyasikia kuhusiana na January ni kielelezo cha njia nyingine ya viongozi wa kisiasa wanavyopata hela za haramu kwa njia tofauti. leo hii mmoja tuhuma zake zimeanikwa,wapo wengi wanatembea vifua mbele kwakuwa siku zao za kuumbuka hazijafika.

Nimeingiwa na mashaka ninavyoshuhudia ukimya wa ZZK,mara zote yupo online na anakuwa wa kwanza kuzungumzia maswala ya maadili yanaposiginwa na viongozi.

Najiuliza kwanini amekuwa kimyaa kwenye hili sakata.Ajitokeze tujue msimamo wake na chama chake.Tunaamini yeye ni kijana wa kupigiwa mfano kwa maneno na vitendo.Urafiki haupo kwenye ukweli naamini.

Wakati ambapo sakata la kumchafua January Makamba likifikia ukomo baada ya muazilishi wa swala hilo kukiri kwamba hakuwa ushahidi, Zitto Kabwe ametoa za "kibabe".

Kupitia instagram Zitto ameandika " Hasira za MWANAUME mmoja zinaweza kuzuia ukuaji wako kisiasa. Lakini kumbuka SIASA ni mbio ndefu na sio mbio za vijiti kama tulivyoelezwa.

Maneno ya Zitto yanaakisi vyema juhudi za kumchafua Makamba ambazo zimekwama.

Kwa vipi?:

1. Hasira za MWANAUME mmoja kuzuia ukuaji kisiasa : Kumekuwa na juhudi za wanasiasa waovu kuzuia ndoto za Wanasiasa vijana wenye uwezo mkubwa. Jambo hili liliwahi kumkumba Zitto kwamba na sasa limejaribiwa kwa Makamba.

Wanasiasa waovu ndani na nje ya CCM wanatamani kuona Makamba anaanguka : kwanza ili kuchukua nafasi ya Uwaziri na pili ili kulipa visasi dhidi ya kile wanachoamini Makamba aliwaadhibu wapinzani katika uchaguzi mkuu (Rejea jina la KUBWA LA MAADUI ).

Haikuhitaji kuwa mnajimu ili kufahamu kwamba Makamba ni hazina kubwa kwa Taifa, na ni kati ya nguzo muhimu za CCM na hivyo kumchafua sasa itawasaidia katika chaguzi zijazo.

Mange Kimambi alikuwa anatumika kuhakikisha anazuia ukuaji wa Makamba kisiasa. Ifahamike Mange hajaanza kumchafua Makamba sasa alishaanza lakini Jambo jema ni kwamba amekuwa akishindwa kufanikiwa na jaribio la sasa ameshindwa kwa aibu zaidi.

Zitto anamaliza kwa kusema.

Maneno haya yanakuja wakati ambapo "kamaradi" Makamba anapata ushindi dhidi jaribio la kumchafua. Mange Kimambi ameshatangaza kwamba hakuwa na ushahidi kwa jambo lake, hivyo amekaa pembeni.

Muitaliano waliyedai ametapeliwa na Makamba , amejitokeza na kuueleza ulimwengu kwamba Mange ni muongo.

Amethibitisha kwamba January hakuwahi kufanya aina yoyote ya utapeli.
Mange na mabosi wake wamebaki na aibu ya karne.

Asante Zitto kwa maneno hayo ya kishujaa.

Hongera kamaradi January Makamba kwa "ushindi wa dhahiri".
 
Zitto ameshamtetea January kupitia msemaji wake wa chama Habib Mchange,rejea uzi ulioletw humu leo na Mchange.
 
Tunayoyasikia kuhusiana na January ni kielelezo cha njia nyingine ya viongozi wa kisiasa wanavyopata hela za haramu kwa njia tofauti. leo hii mmoja tuhuma zake zimeanikwa,wapo wengi wanatembea vifua mbele kwakuwa siku zao za kuumbuka hazujafika.

Nimeingiwa na mashaka ninavyoshuhudia ukimya wa ZZK,mara zote yupo online na anakuwa wa kwanza kuzungumzia maswala ya maadili yanaposiginwa na viongozi. Najiuliza
kwanini amekuwa kimyaa kwenye hili sakata.ajitokeze tujue msimamo wake na chama chake.tunaamini yeye ni kijana wa kupigiwa mfano kwa maneno na vitendo.urafiki haupo kwenye ukweli naamini.


Zitto Kabwe

"...the anger or jealousy of one man could block the advance of a political career... BUT Politics is for long distance runners, not sprinters. Victory is certain comrade"
 
Kwani lazima yeye aseme.Si wengine waseme wakitaka au kama wana hoja?
kwa political analyst kama wewe unapaswa kuelewa kuwa maswala kama hayo yanapotokea yanatoa nafasi kwa vyama vinavyochipukia kama ACT kuonyesha misimamo yao ili kukijenga zaidi chama chao kwa kujipambanua na wanachokiamini.nadhani umeshuhudia ZZK aki tweet kukiwa na hot news za kisiasa.ukizingatia kuwa vyama vyetu vya siasa vinaimarishwa zaidi na matukio kuliko sera.Hivyo naamini yeye anaumuhimu wa kuonyesha msimamo hususani ambapo rafiki yake kaguswa,ili wananchi tupime ukomavu wake wa kisiasa.
 
Zitto Kabwe

"...the anger or jealousy of one man could block the advance of a political career... BUT Politics is for long distance runners, not sprinters. Victory is certain comrade"
we need that in a layman language not parable which give diversity of interpretation. should his friend resign or retain his political position?
 
Tunayoyasikia kuhusiana na January ni kielelezo cha njia nyingine ya viongozi wa kisiasa wanavyopata hela za haramu kwa njia tofauti. leo hii mmoja tuhuma zake zimeanikwa,wapo wengi wanatembea vifua mbele kwakuwa siku zao za kuumbuka hazujafika.

Nimeingiwa na mashaka ninavyoshuhudia ukimya wa ZZK,mara zote yupo online na anakuwa wa kwanza kuzungumzia maswala ya maadili yanaposiginwa na viongozi. Najiuliza
kwanini amekuwa kimyaa kwenye hili sakata.ajitokeze tujue msimamo wake na chama chake.tunaamini yeye ni kijana wa kupigiwa mfano kwa maneno na vitendo.urafiki haupo kwenye ukweli naamini.

YEYE ANAPAMBANA NA RAIS MAGUFURI KUWA ATANGANZAJE MUSHAHARA WAKE AKAMA VILE NI JUKUMU LAKE LA KIKATIBA.
 
YEYE ANAPAMBANA NA RAIS MAGUFURI KUWA ATANGANZAJE MUSHAHARA WAKE AKAMA VILE NI JUKUMU LAKE LA KIKATIBA.
Maswala yale sio contention issue kwa sasa! tunataka adadavue hili.ili tupime ukomavu wake wa kisiasa.mengine mbona anakuwa frontrunner?!
 
Mimi mwenyewe hapa nipo kimya.

Natafakari na kuchunguza kama ni kweli au ni chuki,fitna,wivu,kijicho au roho mbaya.
 
Kiongozi Mkuu wa ACT Tanzania ameandika ujumbe kwenye fb yake,ujumbe huu unaonekana kumtia moyo January Makamba kuhusu masaibu yanayomkuta....Ikumbukwe kwamba Zito hajawahi kumsema vibaya Makamba,hata figisu zake wakati wa uchaguzi hakuzikemea.UJUMBE wake "...the anger or jealousy of one
man could block the advance of
a political career... BUT Politics is
for long distance runners, not
sprinters. Victory is certain
comrade".Zito pia aliwahi kumtaja January kama hazina kubwa kwa Taifa,namnukuu "January Makamba, ni mmoja ya
Hazina kubwa sana ndani ya
chama cha mapinduzi. Na
nadhani kama wakimuandaa
vizuri anaweza kuja kuwa Lulu
ya chama cha mapinduzi.
Muhimu ni kuhakikisha ya
kwamba anapata majukumu
ambayo yatamkomaza zaidi
kiuongozi na kuwa tayari
kuweza kufanya majukumu
makubwa zaidi katika nchi
yetu".
 
Back
Top Bottom