Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,168
- 5,522
"Umati huu wa watu ambao mmekusanyika leo(Novemba 29, 2024) uwanja huu wa Kawawa ni ishara dhahiri ya kwamba sisi ndio washindi katika uchaguzi uliomalizika wa serikali za mitaa Vijiji na Vitongoji”
“Kama CCM wanaamini kuwa wao ndio washindi waje wathubutu kutujibu mkutano kama huu hapa Kawawa, sisi ndio wenye mji huu na leo tumewaonyesha mtu aliyeshindwa hawezi kuwa na furaha hii tuliyonayo, hawezi kukusanyika hapa na kufanya mkutano kama huu tunaoufanya”
Ni maneno ya Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wafuasi wa chama hicho pamoja na wananchi wa Kigoma waliojitokeza kumsikiliza jana Novemba 29, katika Uwanja wa Kawawa, uliopo Ujiji Kigoma.
PIA SOMA
- LGE2024 - Kigoma: Zitto Kabwe adai palikuwa na kua nyingi bandia kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
- LGE2024 - Kigoma: Zitto Kabwe aonya wizi wa kura, atoa rai Wananchi kuzilinda