Zitto Kabwe Mwenyekiti wako hamjui Corbyn!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Wakati Zito Kabwe akiwa nchini Uingereza kukutana na Wazungu na kupiga selfie kutuma kwenye mitandao ili tuzione Picha hizo, huku site Mwenyekiti wa Chama chake cha ACT amejiunga na CCM, hii inaonyesha wazi kwamba moja kati ya matatizo makubwa ya hawa wanaoitwa Upinzani Tanzania kama chadema, ACt &Co. ni kwamba wako out of touch na Watanzania na ndiyo maana hawafiki popote, na kila siku tunaendelea kuwakataa!


CHAMA Cha CCM Mkoa wa Kigoma kimevuna jumla ya Wanachama wapya 868 kutoka vyama mbalimbali vya siasa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Venasi Busunzu wa wilaya ya Kakonko na Mwenyekiti wa CUF Kilembwe Omari mgombea udiwani kata ya Sinuka wamekabidhiwa kadi ya chama hicho jana, katika hitimisho ya sherehe za madhimisho ya kutimiza miaka 40 ya CCM.

Akihitimisha sherehe hizo jana zilizo fanyika Kimkoa Katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza Mwenyekiti wa CCM kigoma Amani Kabourou , alisema katika maazimisho waliyafanya Mkoa mzima katika Wilaya zote walipatikana wanachama wapya 726 na kutoka vyama vya upinzani ni wanachama 146 ambao walikabidhiwa kadi katika sherehe za maazimisho zilizo fanyika jana katika Kijiji cha Mwakizega kata ya Mwakizega Wilaya ya Uvinza.

Alisema wanachama hao Waliamua kurudi katika Chama hicho kutokana na Shughuli kubwa zinazo fanywa na chama hicho , ambapo mpaka sasa kuna Maendeleo Makubwa yaliyo fanyika katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha uongozi wa serikali unaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Kabourou alisema Kwa sasa Viongozi wa chama hicho wameweka mikakati wa kukisafisha chama hicho kwa kuondoa viongozi wote wasio na sifa wanaokichafua sana na kuifanya CCM kuwa mpya na Serikali mpya kutokana na Misingi iliyo wekwa na waanzirishi wa Chama hicho.

Akizungumzia hatua hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Bususnzu alisema amegundua mapungufu makubwa katika chama cha awali hali ,iliyomshawishi kujiunga na ccm ni pamoja na viongozi kuhamasisha misuguano kwa jamii ,ili nchi isitawalike lakini kwa awamu ya serikali ya wamu ya tano ya John Magufuli ni kigezo cha upinzani kukubali uwajibikaji wake wenye tija kwa wananchi.

Akizungumzia hilo Kilembwe Omari alisema amerudi kundini akiwa na wananchama 34 kutoka chama cha ACT wazalendo ,akidai amerudi kwa baba na mama yake akiwa na wenzake hao,sababu aminiye na kubatizwa ameokoka na anatumaini atakuwa mumini mzuri wa chama hicho.

Akiongezea hilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF,wilaya ya Kakonko Amana Ramadhani alisema anapokea kadi kwa hiari japokuwa amekulia katika upinzani akiwa mwenyekiti wa kina mama kwa miaka 15 wa chama cha CUF,kwa sababu ya sera zake akijua kitawakomboa wananchi,kumbe kipo kwa ajili ya kupata ruzuku ya serikali.

Alisema tangu mwaka 1990 wapo wanachama wawili hali inayokwamisha jitihada za kuleta maendeleo ,awali aliamini ujio wa UKAWA ni kuimarisha vyama lakini kilichotokea ni ubaguzi wa udini na kugombea maslai binafsi na si wananchi,hivyo hana budi kujiunga na ccm ili kutimiza ndoto za kuinua uchumi .

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emanuel Maganga alisema kwa awamu ya tano ya serikali ya leo,imetatua kero mbalimbali za wananchi,hususani katika sekta ya elimu kigoma imepiga hatua 2015/16 wilaya ya kakonko ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha pili na kidato cha sita kigoma ilishika nafasi ya kwanza kitaifa.


CCM wakiwa site wanapiga kazi!






Hapa CCM wakiwa na Wananchi kula keki!


Huku site ushapoteza Mtu muhimu, Mwenyekiti wa ACT amejiunga na CCM!


Huyo Mzungu hapigi kura Tanzania!
 
Pole sana mleta mada. Mada yako ni dhaifu sana, ndio maana haina wachangiaji. Ningekuwa moderator ningeifutilia mbali. Yaani mleta mada bado unatuletea siasa za maigizo? Pole sana.
 
Wewe wacha kutaka kuigeza JF kuwa kama TBCCM au kijarida cha Uhuru
Upuuzi huu mpelee Ayub Rioba
 
Hao hawajapata ajali na kufia Mbali?

Maana wamekiuka Agizo la Mungu Mtu
 
Be positive mr.
Unaanza kupoteza mvuto hapa Jf na thread zako za wapinzani kila siku.. Kuna mambo mengi yakuzungumziwa na yenye manufaa ktk jamii hii ya kitanzania.
Mfano hii thread yako ina mchango gani kwa taifa hili? Ukimkosoa au kumtukana zitto inatusadia nn ss watanzania? HIZI NDIZO SIASA ZA MAJITAKA AMBAZO ZINAENDA KUFA
*Ajira zimesimamishwa
*Uhakiki usiosha
*Madawa ya kulevya
*n.k
Hata siku moja sijaona thread yako ya maana zaid ya kudili na wapinzani tu kila siku. Hii inatupa picha kuwa ndivyo mlivyo mpo kwa ajili ya kukipigania chama siyo watanzania.
Ukiona ulivyochokwa angalia VIEWS NA REPLIES. UNATIA HURUMA.
TUNAHITAJI MAMBO MENGI YAFANYIKE KWA AJILI YA MAENDELEO YA WATANZANIA KM VILE AJIRA, MIKOPO,MAMBO YA AFYA, KILIMO, ELIMU N.K NA JITIHADA ZILICHUKULIWA.
*Hapo ndipo utofauti mkubwa sana unapoonekana kati ya chama cha ssm na wapinzani. SISIEM WANAHANGAIKA KILA SIKU KUIMAIRISHA CHAMA CHAO NA WAPINZANI WENGI WANAHANGAIKA KWA AJILI YA KUTETEA MAENDELEO YA WATANZANIA.
SIKU MLIPOSIMAMISHA AJIRA ZA WATOTO MASKINI NDIYO NIKAJUA SISIEM NI CHAMA DHALIMU SANA HATA ILE MIEZ MIWILI YA mungu WENU NAYO MPAKA LEO HAIJATIMIA SBB NI ZAMU YA KULA MAKADA
"Hakuna nchi yyte dunian isiyotoa ajira na hakuna nchi yyte dunia inayoajiri watu wote''
*Akili za kushikiwa na kukaririshwa kuwa ukilalamika ww ni mpinzani au mpiga dili.
Ww endelea kuhangaika na wapinzani wakt kuna mambo mengi ya kuzungumzia. Ndiyo maana nashangaa miaka yote 54+ bado watoto wanakaa chini KUMBE WATU WAPO BUSY NA UPINZANI
 

Chachu Ombara, leo nimekuweka kwenye kundi la watanzania wazalendo tunaoishi kwa uhalisia na sio bendera fuata upepo..
 

CCM chama cha majizi hata kama wapinzani wataamia wote CCM ntapigia kura jiwe sio kwamba sipigi napiga kutoichagua CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…