Zitto Kabwe: Mwanasiasa atayenufaika na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)

affinitytz

JF-Expert Member
Feb 10, 2020
215
1,001
Habari ya ACT Wazalendo kukubali kuwa sehemu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekuwa za kuwashtua wafuatiliaji wengi wa masuala ya kisiasa.

Wengi Wanajiuliza je ACT Wazalendo imekubali dhuluma zilizotokea wakati wa uchaguzi?

Licha ya Addo Shaibu kutanabaisha umma kuwa majadiliano yalikuwa makali sana na kwamba chama kimefikia uamuzi mgumu. Ukweli ni upi?

Ukweli ni kwamba kujiunga kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa ni wazo la Zitto Zuberi Kabwe.

Kwa chama kichanga cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Zuberi Kabwe anajua kuacha chama kiwe bila uwakilishi kwa miaka mitano ni kukiua chama.

Zitto anafahamu faida za uwakilishi wa ACT Wazalendo katika serikali ya umoja wa kitaifa na katika bunge la jamhuri.

Zitto ameona fursa ya kukuza chama.

Kutoka chama kilichopata kiti kimoja cha Ubunge mpaka kuwa sehemu ya Serikali ya Mapinduzi na wabunge watatu.

Huu ni ushindi kwa Zitto.

Kwa sasa ACT Wazalendo inazidiwa na CHADEMA tu katika njia kuelekea kuwa chama kikuu cha Upinzani Tanzania..

Kushiriki kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar itawapatia mtaji wa rasilimali na muda wa kukuza chama.

Hongera Zitto, kwa mara nyingine tena umeweza kuweka mbele maslahi yako ya kuwa na chama kikubwa cha upinzani nchini.
 
Sasa kama alijua kuwa ina faida kwake kwanini aliwahadaa wazanzibar kuwa hawautambui uchaguzi huo?
Kwanini acheze na akili za wazanzibar wasio na hatia?

Ni heri angekubari toka mwanzo kuliko alivyojidai kuwa ana "msimamo" kumbe tapeli tu kama matapeli wengine😑
 
Siasa si uadui kama CDM wanavyofanya dhidi ya CCM
CDM haifanyi siasa kuwa uadui, CCM kwa kushirikiana na Polisi, Tiss na vyombo vingine ndo wanafanya siasa kuwa uadui,

Ina maana Lissu alipopigwa risas ilikuwa ni kumfanya kuwa rafik?

Ben Saanae kupotezwa ni kufanya urafik?

Wanasiasa wa upinzani/ chadema kutekwa ni kuwafanya marafiki?

Mbowe na wenzake na viongozi wengine wa chadema ngazi tofauti kupewa kesi na wengine kufungwa ni kuwafanya marafiki?

Mbowe kufilisiwa na wanachama wengine pia ni kuwafanya marafiki
 
Ukweli ni kwamba kujiunga kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa ni wazo la Zitto Zuberi Kabwe.
Acha uwongo. Zitto na mwenzake Lissu wamekuwa wapinzani wakubwa wa wazo hilo. Wameshinikiza kwa nguvu zao zote wabunge wao wasuse kwenda bungeni kwani watakuwa wanahalalisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020 ambao kwao wanauona ulikuwa haramu na wamewakabidhi akina Robert Amstedam kuushughulikia kimataifa!

Chadema wameingia kwenye mkenge kwa kufuata dhana hiyo ya kijinga ya akina Zitto na Lissu. Wamewafukuza wabunge wao wa viti maalum na yule mmoja wa jimbo yuko kando. Wanasubiri neema ya ushindi kutoka kwa Robert Amsterdam ya kurudiwa uchaguzi mkuu hivi karibuni kwa shinikizo la kimataifa.

Mzee Maalim Seif kwa uzoefu alio nao kakataa katakata upumbafu huo wa kuamini kwamba akina Amsterdam wana uwezo wa kufanya uchaguzi mkuu utarudiwa. Hivyo wazo la ACT kujiunga kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ni la Maalim Seif Sharif. Zitto Kabwe hana mamlaka tena huko kwenye ACT ya Zanzibar. Huko mwenye mamlaka ni Mzee Seif ambaye ndiye mwenyekiti wa chama na ni makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Zitto mamlaka yake yanaishia kwetu Tanganyika ambako amepoteza kila kitu including Membe! Kuna uwezekano naye akakimbilia huko aliko rafiki yake Lissu. Time will tell.
 
Zito alaumiwe Kama ameingia SUK bila makubaliano yoyote maana akumbuke Kuna chaguzi ndogo, Ila pia ameenda kubana nafasi za wachumia tumbo sasa hivi watakuwa wanaumwa kweli kweli, Sasa Kila chama kijijenge chenyewe kisitegemee nguvu ya kuungana.
 
Back
Top Bottom