Zitto Kabwe: Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye akiba ya fedha za kigeni ya Tanzania

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
4,423
10,784
USD 500m zimepungua kwenye Foreign Reserve. Kuna ' jambo ' kubwa kwenye Akiba ya Fedha za Kigeni Tanzania

Nikiwa nasoma Taarifa ya IMF ( IMF Executive Board Completes Fourth PSI for Tanzania and Concludes 2016 Article IV Consultation) kuhusu Tanzania niliona kuwa Akiba yetu ya Fedha za kigeni imeshuka ' Akiba ya kuweza kuhudumia miezi 4.1 ya bidhaa tunazoagiza kutoka nje. Taarifa hii http://www.imf.org/external/pubs/ft/scr/2016/cr16253.pdf inaonyesha kuwa Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania imeporomoka mpaka ' Akiba ya kuweza kuhudumia miezi 3.6 ya bidhaa tunazoagiza kutoka Nje'. Sikuamini ikabidi nikatazame Taarifa za Benki Kuu.

Taarifa ya Benki Kuu ya Mwezi Novemba ( BOT Monthly Economic Review ) inaonyesha kuwa Tanzania ilikuwa na Akiba ya USD 4bn ambayo inatosha kuagiza bidhaa kwa miezi 4. Hata hivyo BOT wanaonyesha kuwa ilipofika mwezi April 2016 Akiba ya Fedha za kigeni ilishuka mpaka USD 3.8bn na Mwezi Juni imeshuka mpaka USD 3.5bn.

Katika kipindi ambacho bei ya mafuta bado ipo chini na mauzo nje bado hayajashuka ilitakiwa Foreign Reserve yetu iongezeke sio kupungua.

Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania. Ama Serikali kupitia Benki Kuu inapunguza Akiba ili kuibeba Shilingi isishuke thamani au Akiba imetumika kwa matumizi ya kawaida. Serikali haina budi kutoa maelezo ya kina.

--------------
---------------
Gavana wa Benki nkuu alizugumza haya.

http://dailynews.co.tz/index.php/business/51925-foreign-reserves-are-sufficient-bot
 
Hapa Zito naona kama amechanganya kidogo, anaposema, 'Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania. Ama Serikali kupitia Benki Kuu inapunguza Akiba ili kuibeba Shilingi isishuke thamani au Akiba imetumika kwa matumizi ya kawaida. Serikali haina budi kutoa maelezo ya kina. Huwezi kupandisha thamani ya shilingi kwa kupunguza akiba ya fedha za kigeni. Utapandisha shilingi kwa kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni.
 
Zitto habari ya kushuka kwa akiba ya fedha za kigeni wala si hoja sisi tuko busy tunakamua majipu.Shehena ikishuka bandari hatuna habari kabisa watali wakipungua ndio kwanza tunahamia Dodoma Baba mwaka huu ni wetu tutaheshimiana hapa mjini.
Tuna deal na mafisadi hasa wale wahujumu uchumi wakina Lema na wenzao.
 
USD 500m zimepungua kwenye Foreign Reserve. Kuna ' jambo ' kubwa kwenye Akiba ya Fedha za Kigeni Tanzania

Nikiwa nasoma Taarifa ya IMF ( IMF Executive Board Completes Fourth PSI for Tanzania and Concludes 2016 Article IV Consultation) kuhusu Tanzania niliona kuwa Akiba yetu ya Fedha za kigeni imeshuka ' Akiba ya kuweza kuhudumia miezi 4.1 ya bidhaa tunazoagiza kutoka nje. Taarifa hii http://www.imf.org/external/pubs/ft/scr/2016/cr16253.pdf inaonyesha kuwa Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania imeporomoka mpaka ' Akiba ya kuweza kuhudumia miezi 3.6 ya bidhaa tunazoagiza kutoka Nje'. Sikuamini ikabidi nikatazame Taarifa za Benki Kuu.

Taarifa ya Benki Kuu ya Mwezi Novemba ( BOT Monthly Economic Review ) inaonyesha kuwa Tanzania ilikuwa na Akiba ya USD 4bn ambayo inatosha kuagiza bidhaa kwa miezi 4. Hata hivyo BOT wanaonyesha kuwa ilipofika mwezi April 2016 Akiba ya Fedha za kigeni ilishuka mpaka USD 3.8bn na Mwezi Juni imeshuka mpaka USD 3.5bn.

Katika kipindi ambacho bei ya mafuta bado ipo chini na mauzo nje bado hayajashuka ilitakiwa Foreign Reserve yetu iongezeke sio kupungua.

Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania. Ama Serikali kupitia Benki Kuu inapunguza Akiba ili kuibeba Shilingi isishuke thamani au Akiba imetumika kwa matumizi ya kawaida. Serikali haina budi kutoa maelezo ya kina.
Zitto ni mzito wa kufikiria, mwenendo wa exchange rate ukiwa mbaya huyohuyo zitto atasema Benki Kuu haifanyi kazi yake, sijui anadhani BoT inatengeneza dola ya Marekani!!, anadhani BOT anapouza pesa za kigeni sokoni ili ku stabilize exchange rate hua zinatoka wapi??mwaka jana tumeona mapambano ya exchange rate sokoni na tuneona sasa hali ni shwari, hajiulizi nini kimefanyika!!

Jambo lingine zitto afanye utafiti na aangalie ni kwakiasi gani misaada ya kigeni imepungua, na umuhimu wa misaada hio katika kuongeza reserves za nchi.

Zitto aache kuropoka, akidhani ana hoja za msingi kumbe hajui kusoma report za kitaalam.
 
Uzalishaji umepungua kwa kasi ya ajabu, unategemea utauza nini nje upate hizo fedha za kigeni?
Utalii nao ndo umeshapigwa pini, hata hivyo vidola vya watalii masikini na matajiri hatuvipati tena.
Serikali haina fedha, makusanyo ya kodi yanasuasua hela ya kuendesha serikali wataitoa wapi?
 
Hapa Zito naona kama amechanganya kidogo, anaposema, 'Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania. Ama Serikali kupitia Benki Kuu inapunguza Akiba ili kuibeba Shilingi isishuke thamani au Akiba imetumika kwa matumizi ya kawaida. Serikali haina budi kutoa maelezo ya kina. Huwezi kupandisha thamani ya shilingi kwa kupunguza akiba ya fedha za kigeni. Utapandisha shilingi kwa kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni.

Mkuu kwa kuongeza dola kwenye mzunguko aotomatic bei yake inashuka

ZITTO anamaanisha BOT wanaweza kuwa waliruhusu dola nyinge kwenye mzunguko ili kupunguza price,siunajua bidhaa zikiwa nyingi sokoni automatic price inashuka.
 
Kama kungekuwa na tatizo lisilo la kawaida Serikali ingetoa tamko, tusianze kuwa overly concern na mambo ambayo Serikali ina ujuzi wa ku deal nayo, sio vizuri kuwa prophet of doom masaa yote.
Yeye kasoma kuliko kina Prof. Ndulu na Mpango. Tatizo la kujifanya unajua kila kitu.
 
Hapa Zito naona kama amechanganya kidogo, anaposema, 'Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania. Ama Serikali kupitia Benki Kuu inapunguza Akiba ili kuibeba Shilingi isishuke thamani au Akiba imetumika kwa matumizi ya kawaida. Serikali haina budi kutoa maelezo ya kina. Huwezi kupandisha thamani ya shilingi kwa kupunguza akiba ya fedha za kigeni. Utapandisha shilingi kwa kuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni.
ili zikiwa zinahitajika kwa wingi izo fedha za kigeni (high demand) uweze kukidhi mahitaji husika unaposema wamezichukua ili kupandisha shillingi maana yake zikipungua (fedha) za kigeni demand/ uhitaji wake ukiwa mkubwa itasababisha watu kutoa shiling kwa wingi ili wapate forex hivyo kuporomoka kwa nguvu kwa shilingi (wakati waanunuzi nje)
 
Back
Top Bottom