Zitto Kabwe: Gharama za maisha zimepanda Wananchi wanashindwa kumudu maisha ya kila siku

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
234
427
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa kufuatia ziara za Chama hicho ambazo zimefanyika kwenye maeneo mbalimbali nchini wamebaini mambo mahususi ambayo anadai kuwa yasipochukuliwa hatua yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa Taifa.​

Akihutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya ACT Wazalendo unaofanyika kwenye ukumbi ulioko kwenye Makao ya Chama hicho Magomeni Dar es Salaam leo February 12, 2024, baadhi ya mambo ambayo ameyabainisha wazi ni pamoja na migogoro ya ardhi na migogoro ya hifadhi na vijiji. Amesema kuwa kuhusu suala hilo katika ziara zao kwenye maeneo ya Kusini mwa Tanzania wamekutana na malalamiko ya wakulima dhidi ya wafugaji ambayo yamesababisha migogoro ambayo imepelekea mauaji.

Masuala mengine ni kupanda kwa gharama za maisha, ambapo Zitto amedai kuwa wananchi wanashindwa kumudu maisha ya kila siku, baadhi ya vitu ambavyo ametaja kupelekea ugumu huo ni kupanda kwa bei za vyakula, nauli za usafiri pamoja na vifaa vya ujenzi.

Zitto amesema kuwa licha ya sababu mbalimbali zinazotolewa na Serikali lakini wananchi wanachotaka kuona ni maisha yao kuwa nafuu, hivyo amesema kuwa wito wa ACT Wazalendo ni kuwa Serikali ina wajibu wa kuhakikisha wananchi wanamudu maisha yao kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutunga na kutekelezeka sera zinazohakikisha kuwa bei za bidhaa muhimu kama chakula, mavazi na usafiri haviwi mzigo mkubwa kwa wananchi.

Sambamba na masuala hayo jambo lingine ambalo amelitaja ni changamoto ya ajira kwa vijana, amesema kuwa suala hilo limekuwa mwiba mchungu kwa Taifa kwa sababu Serikali haijielekezi kisera kujenga uchumi unaozalisha ajira nyingi, bora na zenye staha.

Amesema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kupitia baraza la mawaziri kivuli, wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kuchambua sera za Serikali kwenye baadhi ya mambo na kushauri hatua mbalimbali zichukuliwe dhidi ya mambo husika, ambapo amesema baadhi mapendekezo yamekuwa yakifanyiwa kazi lakini sio katika hali ya kulizisha.

FB_IMG_1707747024412.jpg
 
IMG_4147.jpg



Mama si anaupiga mwingi? Au kaghairi?

Makonda si anapita huko kutatua shida au hamna msaada wa direct aliowapatia wananchi?

Tutaheshimiana tu uzuri wanaccm hayo hayawagusi na wana maduka yao ya punguzo la bei kwa kila wakitakacho acha wananchi wakome huenda akili ikawarejea mwakani?
 
Back
Top Bottom