Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,662
- 8,787
Zitto Kabwe amesema mwaka 2012 alipata changamoto chama chake cha wakati huo cha CHADEMA akidai ilikuwa juhudi ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Zitto amesema kulikuwa na makubaliano baada ya kugombea uchaguzi wa nyuma yake kwamba amuachie kijiti Freeman Mbowe na atampokea miaka mitano ijayo na badala yake miaka miwili kabla aliondolewa nyazifa zote za uongozi Chadema na wapo katika kundi lao walisema waende CCM.
Zitto Kabwe amesema Jakaya Kikwete alimuita na kumwambia ana machaguo mawili kwa kuwa alikuwa anachipukia kwenye siasa, kwanza kujiunga na chama tawala cha CCM na endapo angefanya hivyo angempa uwaziri wa fedha siku inayofata.
Rais mstaafu Kikwete alimpa angalizo Zitto Kabwe kwamba kwa maono yake CCM haitakuwepo madarakani muda mrefu ilhali Zitto bado kijana mdogo na kumshauri kutafuta jukwaa lingine lakini sio la chama tawala.
Zitto amesema kwenye hicho kikao mmoja wa waliokuwepo ni rafiki yake Deo Fulikunjombe naye akamshauri asiende CCM.