Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,500
- 3,698
Kupitia kurasa wake wa Twitter, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo amepinga maneno ya Dkt. Wilbroad Slaa akidai kuwa Sheria ya Ukaguzi wa Fedha (2009), inaeleza baada ya CAG kukabidhi ripoti kwa Rais na Bungeni, hatakiwi kuichambua kiundani hadharani
Zitto amesema “Dkt. Slaa hasemi kweli kuhusu mjadala wa ripoti ya CAG. Ripoti ya CAG ikishawekwa mezani Bungeni inakuwa nyaraka ya umma. Mtu yeyote ana Haki ya kuijadili. Wajibu wa Serikali ni kujibu hoja za Ukaguzi kwa mujibu wa Sheria. Mjadala umekuwepo Siku zote. Dkt. Slaa anakosea sana
Dkt. Slaa alipokuwa anazungumza kuhusu kashfa ya EPA alisubiri PAC? Report ya Ernst&Young aliyoitumia ilikuwa imepita PAC? Mwaka 2012 akiwa SG wa Chama aliidhinisha Wabunge kutia saini hoja ya kutokuwa na imani ya Waziri Mkuu kufuatia ripoti ya CAG. Ilikuwa imepita PAC?
CAG kasema TANROADS walifanya manunuzi ya mtambo wa kuzalisha Sukari kinyume na Sheria na Kiwanda kimechelewa Miaka 3 sasa. Dola 50.3M zimehojiwa. Unasubiri PAC wafanye nini hapa? Lini mjadala ulizuia PAC kufanya kazi yake? ( nimekuwa Mkt wa POAC/PAC) kwa Miaka 8 ).
CAG kasema kuwa Mkandarasi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga alijipatia Fedha TZS 65 Bilioni kinyume na Mkataba kwa kutoa kazi aliyopewa kwa Kampuni nyengine (subcontract) kinyume na mkataba wake na TPA. Unasubiri PAC ndio tujadili? Huyu Mkandarasi alipaswa kuwa ameshtakiwa
CAG kasema TZS 196 Bilioni za Wananchi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinazozunguka Bwawa la Umeme la Nyerere hazijatolewa, haijulikani zipo wapi na Mkandarasi kalipwa Fedha zake.Unasubiri PAC ujadili hili?Yeye Slaa Enzi zake Slaa kweli angesubiri na Fedha za Wananchi kupotea?
CAG kasema kuwa Mkandarasi wa kujenga vihenge/maghala ya chakula kalipwa Fedha na kasepa kaacha Mradi, Nchi haina maeneo ya kuhifadhi chakula tangu mwaka 2017. Yeye Slaa angesubiri PAC ili kujadili jambo hili linalohusu uhai wa Watanzania ?
Ripoti ya CAG ikishaingizwa Bungeni ni MALI YA UMMA. Lazima ijadiliwe na umma. Tumekuwa tukifanya hivyo Siku zote tangu ripoti zianze kutoka kwa umma kisheria Mwaka 2008 baada ya Sheria ya Ukaguzi wa umma kutungwa. Wajibu wa PAC ni kupata majibu ya Hoja za Ukaguzi. BASI”
SEHEMU YA NUKUU YA ALICHOSEMA DKT. SLAA
"Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu"
Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.
Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG"