Zipi ni faida na athari za kuwa kwenye magroup ya Whatsapp ya ukoo

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
7,856
10,377
Katika makala ya leo,
Ni vyema tukaeleweshana kwa kina faida na athari za kuwa kwenye magroup ya Whatsapp ya ukoo.

Najua wengi tumezoea kujiunga na magroup ya shule, kazini na biashara ambapo faida zake ni nyingi sana. Kwenye haya magroup unaweza kuona tangazo la kazi, unaweza kupata connection ya kazi au biashara na hata kupata wateja wa bidhaa zako.

Kwa wenye uzoefu je ni zipi faida na athari za kuwa kwenye magroup ya Whatsapp ya ukoo.
 
Mimi sipo group lolote la WhatsApp. Si Shule, Chuo, kazini au familia. Nilikataa huo ujinga...
 
Faida za Magroup ya Whatsapp ya Ukoo:

Breaking News za Ukoo: Utajua nani amevunja ndoa, nani ana harusi, na nani kafiwa kabla hata taarifa zifike kwa wazazi.

Michango,Michango na michango: Magroup haya yanasaidia kukusanya michango ya harusi, misiba, na sherehe. Lakini ukishangaa umeingizwa kwenye mchango wa kimya kimya, usikasirike.

Kudumisha Undugu : Wale ukoo wa mbali wanaokumbuka jina lako mara ya mwisho ulipokuwa chekechea, sasa wanajifanya wanakujua vizuri.

Athari za Magroup ya Whatsapp ya Ukoo:

Drama za Kisiasa: Kila mzee wa ukoo anadhani yeye ndiye msemaji wa taifa.

Usumbufu wa Michango: Ukiwa na elfu kumi tu kwenye simu, usithubutu kufungua group.

Upuuzi wa Forwarded Messages: Hapo ndipo unapogundua ukoo wako unaamini kila chain message inayosema “sambaza kwa watu 10 kupata baraka za mwaka.”

Udaku Bila Kikomo: Maisha yako yanageuka sinema, kila hatua unayochukua kuna mjadala. Ukiweka picha ya chakula tu, watasema umeanza maisha ya kifahari.
 
Sina group lolote la whatsapp kwenye simu yangu mbali ya yale ya ofisini ambayo yapo sababu ya uendashaji wa kazi wa kila siku.

Naamini siku zote kila hatua ya maisha unayovuka unapaswa kuiacha huko huko ulipotokea. Sio usahau uliokuwa nao, hapana, achana nao kimazoea unless kuna uhitaji.

Naamini magroup yote ya shule na vyuo ulivyopitia huwa hayana dhamira ya kutaka kusalimiana na kujuliana hali. Yapo pale maalum kupima mafanikio ya walio kwenye group.
Binadamu tuna kawaida ya kukadiria heshima tunayompa mtu kulingana na aidha uwezo wake kiuchuni, madaraka yake ama uhitaji wako kwake.

Ukija kwenye magroup ya ukoo, hayo ndio ya kuepuka kabisa. Daima hakuna adui mbaya kama yule mwenye nasaba na wewe. Katika hayo magroup kuna wajomba, mashangazi, binamu nk. Sio kila ndugu atafurahia maendeleo yako ikiwa yeye ama mtoto wake hana mafanikio. Na si kila ndugu atakuwa na huruma na dhiki zako.

Kupitia hayo magroup, kwanza kuna wale wa kukadiria uwezo wako wa pesa/msaada kutokana na shughuli zako, watakuomba msaada, ukisema huna utaambiwa una roho mbaya. Mwanzo wa husda ndio huo sasa.

Daima naamini, mwenye uhitaji na mimi iwe ndugu ama rafiki lazima atakuwa na njia ya kunipata lakini njia hiyo isiwe magroup ya halaiki. Na kama kuna taarifa inapaswa niipate, nitaipata tu.

Naamini sana katika upendo na umoja, ila uwe kwa mbali. Tukutane/tujuane pale panapobidi kukutana, mbali na hapo tupendane kwa mbali tu bila ya magroup.
Mwenye nia/sababu hasa ya kuwa karribu na wewe atakuwa karibu na wewe bila hata ya magroup.
 
Faida ni kuunga undugu,kujua matatizo ya kifamilia na kurahisisha namna ya kuweza kuwasiliana na kusaidiana.

Athari zake
Majungu,kusemana kunakotokana na chuki binafsi,baadhi kujiona watu muhimu zaidi kuliko wengine,kuchangishana michango ya kipumbavu,kuwabeba wavivu kwenye ukoo kwa kukimbilia kuomba msaada kwa kila kitu,kurogana.

Pima faida na hasara
 
Mkuu hapa kwenye athari unaweza kutufafanulia kwa kina
 
Kasimu kangu kangeweza ku screenshot hii comment basi ningefanya hivyo. Point nzito hapa umesema.
Sina group lolote la whatsapp kwenye simu yangu mbali ya yale ya ofisini ambayo yapo sababu ya uendashaji wa kazi wa kila siku.

Naamini siku zote kila hatua ya maisha unayovuka unapaswa kuiacha huko huko ulipotokea. Sio usahau uliokuwa nao, hapana, achana nao kimazoea unless kuna uhitaji.

Naamini magroup yote ya shule na vyuo ulivyopitia huwa hayana dhamira ya kutaka kusalimiana na kujuliana hali. Yapo pale maalum kupima mafanikio ya walio kwenye group.
Binadamu tuna kawaida ya kukadiria heshima tunayompa mtu kulingana na aidha uwezo wake kiuchuni, madaraka yake ama uhitaji wako kwake.

Ukija kwenye magroup ya ukoo, hayo ndio ya kuepuka kabisa. Daima hakuna adui mbaya kama yule mwenye nasaba na wewe. Katika hayo magroup kuna wajomba, mashangazi, binamu nk. Sio kila ndugu atafurahia maendeleo yako ikiwa yeye ama mtoto wake hana mafanikio. Na si kila ndugu atakuwa na huruma na dhiki zako.

Kupitia hayo magroup, kwanza kuna wale wa kukadiria uwezo wako wa pesa kutokana na shughuli zako, watakuomba msaada, ukisema huna utaambiwa una roho mbaya. Mwanzo wa husda ndio huo sasa.

Daima naamini, mwenye uhitaji na mimi iwe ndugu ama rafiki lazima atakuwa na njia ya kunipata lakini njia hiyo isiwe magroup ya halaiki. Na kama kuna taarifa inapaswa niipate, nitaipata tu.
 
Back
Top Bottom