Zingekuwepo bado jamii(species) nyingine za binadamu zaidi ya kwetu ya Homo Sapiens dunia ingekuaje wakati huu?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
46,625
66,816
Kulingana na evolution inasemekana kulikuwepo na jamii(species) zaidi ya tisa za binadamu ambapo kufikia miaka elfu arobaini iliyopita nane zilitoweka kwa sababu mbalimbali na hatimaye ikabaki moja tu iliyo survive ambayo ni ya kwetu ya Homo Sapiens,

Sasa wangekuwepo akina Homo Neanderthals , Homo Erectus, Denisovans n.k dunia si ingekuwa ya moto sana maana kama hii specie moja tu ya kwetu ya Homo Sapiens mtifuano wake ni mkubwa hivi yenyewe kwa yenyewe vipi zingekuwepo species nyingine 8!
 
Mi nilivokua najua evolution maana yake from simple to complex

Yaani alitoka kuwa homo eructus aka develop na kuwa sapiens...

Au wali exist kwa pamoja .?
Kulingana na evolution Kutoka level moja ya simplicity kwenda nyingine complex viumbe waliojitokeza katika hiyo level walikuwa mbalimbali, wengi na walitofautiana kiasi fulani.
Wansayansi wamegawanyika kuhusu Homo Erectus, wapo wenye mtazamo alikuwa ancestor wa binadamu, wengine wana mtazamo ilikuwa specie tofauti inayojitegemea.
 
Aaah sawa sawa lakini vipi ishu ya survive for fittest.... ?
 
Ndio sisi Homo Sapiens tume survive mpaka sasa kati ya species zaidi ya 9 ambao walikuwa ndugu zetu wa karibu.
Ila evolution ya huyu mwamba kama ina shida hvi...

Japo ni nje ya mada mkuu.
Unavozani hiyo gradual change bado inaendelea kwetu au..?
 
Evolution bado inaendelea kulingana na mazingira, mfano kuishi milimani kwa muda mrefu kwa baadhi ya jamii za watu kunafanya mfumo wa upumuaji kuwa tofauti na wengine. Kuna baadhi ya watu hawaoti meno ya magego tena, uwezo wa baadhi ya jamii mbalimbali za watu kupambana na magonjwa unazidi kuongezeka na kuna muda itafikia watakuwa resistance kabisa kwa magonjwa mengi, ubongo wa binadamu unazidi kupungua ukubwa wake, binadamu anazidi kuishi miaka mingi zaidi n.k
 
Hiyo ya watu wa milimani kubadilika kwa mfumo wao wa upumuaji ni temporary change au permanent change...??

Isije ikawa ni isssue ya adaptation tuu kwa kipindi wapo kule juu..
 
Kulingana na evolution inasemekana kulikuwepo na jamii(species) zaidi ya tisa za binadamu ambapo kufikia miaka elfu arobaini iliyopita nane zilitoweka kwa sababu mbalimbali na hatimaye ikabaki moja tu iliyo survive ambayo ni ya kwetu ya Homo Sapiens,

Sasa wangekuwepo akina Homo Neanderthals , Homo Erectus, Denisovans n.k dunia si ingekuwa ya moto sana maana kama hii specie moja tu ya kwetu ya Homo Sapiens mtifuano wake ni mkubwa hivi yenyewe kwa yenyewe vipi zingekuwepo species nyingine 8!
Mkuu kwanza kabisa unapaswa kujua maana ya EVOLUTION

Evolution ni hatua alizopitia binadamu wakati anabadilika kutoka stage moja kwenda stage nyingine ndani ya mamilioni ya miaka.
Kwa muktadha huu maana yake ni kwamba hao wate ni kiumbe kimoja ila kilikua kinakwenda na kubadilika taratibu kwa muda mrefu kwasababu mbalimbali
Sio sahihi kudhania kwamba eti hao walikua viumbe tofauti na waliishi wakati mmoja
Kisayansi hata sisi tunao ishi sasa baada ya miaka bilioni kadhaa zama zetu zitakua zimekwisha na itakuja species nyingine kabisa

Process ya evolution inakwenda taratibu sana na inachukua mamilioni ya miaka kuja kuona tofauti, hakuna anayeweza kuishi that far to notice the deference
 
Attachments

  • CC3BD0C7-F789-4AEF-B657-ADA1E49FA848.png
    CC3BD0C7-F789-4AEF-B657-ADA1E49FA848.png
    164.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom