JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,726
Unapoweka switch on kwenye gari lako ni vizuri ukahakikisha angalau taa hizi zifuatazo zinawaka kwenye dashboard ya gari lako. Taa hizo ni
1. Check engine
2. Oil pressure
3. Airbag
4. Coolant temperature
5. Battery
6. Automatic Transmission Temperature (Kama ipo)
7. ABS
In fact, Ni vizuri kuhakukikisha kila taa iliyopo kwenye dashboard inawaka kwa sababu kila taa pale ina umuhimu wake. Sina uhakika kama kuna gari ukiweka switch on taa zote za dashboard huwa zinawaka ila angalau hizo nilizozitaja hapo juu nina uhakika huwa zinawaka kwa magari yaliyo mengi.
Kwa maaana kama haziwaki basi kuna mambo mawili yanaweza kuwa yametokea.
Jambo la kwanza taa inaweza kuungua au sakiti inayocontrol hiyo taa inaweza kuwa ina shida(hasa kukatika kwa waya). Japo mara nyingi kama kitaa hakiwaki na dashboard yako haijawahi chezewa na mafundi, basi shida huwa ni taa za dashboard kuungua. Kama taa zikiungua zinaweza badilishwa au mtu itamlazimu tu akatafute dashboard nyingine.
Jambo la pili, kuna mafundi huwa wanang'oa hivyo vitaa au kuviziba ili visiwe vinawaka kwa sababu ambazo wanaona zitawapa pesa. Mfano, Kama siku 10 zilizopita nilifungua Dashboard ya passo moja baada ga kukuta taa ya check engine haiwaki. Nilichokikuta ni kwamba taa ilikuwa inawaka ila ilizibwa tu na gundi nyeusi(inaonekana huyo fundi alipewa kazi ya kuzima taa ya check engine badala yake akaamua kuizima tu isionekane machoni pa watu ila iendelee kuwaka ndani kwa ndani na akapiga hela yake). Kwa hiyo tulitoa gundi na taa ikawa inawaka.
Kama taa hizo haziwaki kwa sababu yoyote ile, maana yake ni kwamba likitokea tatizo lolote kwenye gari lako hutojua mpaka Gari lako likuzimie au ligome kutembea kabisa au upate ajali(kwa case ya warning light za usalama).
Ni vitu vidogo lakini vina umuhimu mkubwa.
MWISHO.