Zijue simu zitakazofungiwa tar 16/6

Senator jr

JF-Expert Member
Apr 3, 2016
367
496
Habari wakuu..
Leo sina Habari njema sana but very Important..
Mamlaka ya Mawasiliano
nchini imetoa tamko la
kufungia simu zote feki ifikapo
tarehe 16, Juni. Je, simu yako
ni miongoni mwa simu
zitakazofungiwa ifikapo mwezi
wa sita?
Utatambua vipi kama simu yako ni feki?
Utaweza kutambua kama simu yako ni feki kwa kuangalia
IMEI namba ambacho ni kifupi cha International Mobile
Equipment Identity. Kila simu ina IMEI namba kama
utambulisho wa simu husika, hivyo simu isiyokuwa na
IMEI namba ni sawa na mtu asiye na jina au gari lisilo na
namba ya usajili.
Ili kuweza kujua IMEI namba ya simu yako kuna
njia kuu mbili
Ya kwanza ni kwa kubonyeza *#06# katika simu
yako, hapo simu yako itakuonyesha tarakimu
kadhaa katika kioo chako, usihofu hizo ndio IMEI
namba za simu yako.
Ya pili ni kufungua mfuniko wa nyuma wa simu
yako alafu toa betri, chini ya eneo linapokaa
betri utaweza kuona IMEI namba za simu yako.
Kama simu yako ni ya laini mbili katika njia
utakayotumia kama ilivyoelekezwa hapo juu
utaona IMEI namba mbili tofauti.
Mara nyingi IMEI namba huwa na tarakimu 15

Njia ya Pili
Kwa kutumia kompyuta au simu yako tembelea
tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano kwa kugonga
hapa, utapelekwa katika ukurasa wenye fomu ya
kujaza IMEI namba za simu yako.
Ingiza IMEI namba za simu yako alafu alafu
bonyeza kitufe kilichoandikwa Verify My Device
Utaletewa maelezo yanayohusiana na simu yako,
angalia kwa makini kama maelezo hayo
yanafanana na ya simu yako, kama yanafanana
basi simu yako ipo safi na haitahusika na kifungo
cha Juni 16.

..JE UTATAMBUAJE SIMU FEKI KWA KUIANGALIA...



Hizi ni simu zinazotengenezwa na viwanda bubu hasa hasa
nyingi zinaingia kutoka nchini Uchina. Simu hizi saa
nyingine zinaiga muonekano ata wa makampuni makubwa
yanayofahamika duniani kwa sifa za ubora, mfano za
Samsung au Apple – lakini mnunuaji akizichunguza vizuri
anakuta ni feki.
Ukiacha simu zingine zinazokuja na majina yasiyoelewa
simu nyingi feki huwa zinaiga hadi muonekano wa matoleo
maarufu ya simu za iPhone na Samsung
Wakuu ni muda wa final decision..
Ni jambo litakalokuumiza sana endapo simu yako itafungiwa ikiwa mkononi kwako.
FANYA MAAMUZI MAPEMA
BADILIKA..
cc
Hope of Jf
Senator Jr
 


Ahsante! TECNO BOOM J8, bilashaka itasalimika kutokana na kibano kinachokuja cha mwezi June kutoka TCRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…