Membe S K
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 1,389
- 1,243
ZIELEWE KAZI YA USALAMA WA TAIFA (TISS) NA MIPAKA YAKE
Leo tuongelee TISS au USHUSHU au UNYOKA au IDARA au KITENGO. Kwasababu uelewa mdogo kwa idara hii na kazi zake miongoni mwa wananchi unafanya watu wengi wakose amani wanapokuwa na watu wanaowahisi ni mashushushu, na wakati mwingine watapeliwe na wajanja wanaojifanya watu wa idara.
IDARA YA USALAMA WA TAIFA
Idara ya usalama ni idara maalum chini ya ofisi ya rais. Naam, yaani ukiongelea ushushushu unaongelea idara kubwa ndani ya ikulu yenye mkurugenzi mkuu (Director General of Intelligence Services (DGIS)) na wakurugezi kadhaa wa vitengo mbalimbali (directorates directors) ambao nchi nyingine wanaitwa chiefs, mfano chief wa operesheni au chief wa wafanyakazi na mafunzo. Kutegemea na namna idara ilivyojipanga kunakuwa na ofisi za idara hii wilayani na mikoani.
HISTORIA FUPI YA USALAMA WA TAIFA
Kwenye nchi mbalimbali idara za usalama zilianza kwa kasi nyakati za vita baridi (Cold War) kati ya nchi za Soviet na NATO. Nchi za NATO na washabiki wake wakihofia mashushu wa Soviet kupandikizwa nchini kwao na kushawishi watu kudai sera za kikomunist huku nchi za Soviet na washirika wake zikihofia mashushu wa nchi za NATO na washirika wake kuingia na kushawishi watu wadai siasa za kibepari. Hivyo kama umenifuata vizuri hapa utajuwa kwamba idara ya usalama lengo lake la awali lilikuwa kulinda usalama wa dola dhidi ya adui wa nje na ndani.
KAZI ZA IDARA NA MIPAKA YAKE
Sasa vita baridi vimeisha tatizo nini? Matizo yanayohatarisha usalama wa taifa bado yapo tena mapya na makubwa tu: serikali kupinduliwa, ugaidi, mauaji ya kimbari ya kisiasa (genocide), ukiukwaji wa mikataba ya umoja wa mataifa kama vile madawa ya kulevya, silaha za maangamizi nk. Kwakuwa haya yote yanaweza kutekelezwa na watu wenye maarifa ya juu, akili kubwa, fedha na vitendea kazi vizuri; idara za usalama zinahitaji mfumo imara wa kukusanya taarifa au viashiria kila siku ya Mungu ili kuvichakata, kuvitafsiri, kutunza, na kutolea maamuzi kwa wakati. Mfumo huu hapa Tz tumeuremba kwa jina la kimombo: Tanzania Intelligence and Security Service (TISS), nchi nyingine zinaita Secret Services, nyingine Internal Security and Intelligence nk.
Kwa mantiki hiyo TISS imepewa majukumu makubwa matatu. Mosi, kukusanya taarifa za kintelijensia zihusuzo usalamawa taifa, kuzichakata, kuzitafsiri, kuzitunza, kushauri, na kuziwashirisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi. Pili, kumtaarifu rais juu ya uwapo wa viashiria vya uhujumu, uwapo wa mashushu wa nje ya nchi ndani ya Tz au vibaraka wa wavunjifu wa amani na usalama ndani ya Tz na hivyo kupata baraka ya rais kuweka ufuatiliaji wa mambo hayo kwa wakati. Tatu, kushirikiana na wizara na taasisi nyingine za serikali nchini katika kazi zote zihusuzo idara na pia kushirikiana na idara za inchi nyingine kadri ipasavyo katika kutekeleza majukumu yake. Nne, kumhoji mtu au kikundi chochote cha watu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wizara husika.
MPANGO KAZI WA IDARA KWA KAWAIDA NA WAHUSIKA
Kwa kawaida kila siku ya kazi na siku za tukio maalum saa nne Asubuhi usalama wa taifa chini ya DGIS na mchambuzi wa taarifa zakiintelijensia (national intelligence analyst) inafanya mkutano unaoitwa DEBRIEFING kwa mkuu wa nchi. Kwenye mkutano huu mkuu wa nchi anapewa taarifa zote mpya zenye viashiria chanya (credible threats) na taarifa za ufuatiliaji unaoendelea pamoja na changamoto. Baada ya kupata taarifa kinachofuata ni uchambuzi wa taarifa, kutoa maazimio, kumshauri rais na kuomba ridhaa yake katika kutekelezaji.
Utaalamu wa ofisi ya usalama upo kichwani mwa mtu niliyemtaja hapo juu: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Wala sio DGIS kama wengi tunavyodhani, DGIS ni bosi tu anayeongoza ofisi na ndio maana akiteuliwa anatangazwa mchana kweupe, na wala haitaji kwenda kusoma huko SCOTLAND YARD tulikozoea kusikia wanakwenda kusomea ushushushu. Nimeona watu wakihoji kwanini ma DGIS wanateuliwa na kutenguliwa hadi kufikia 4 tangu mama Samia ashike madaraka. Niwatoe hofu kwamba tunayetakiwa kushangaa akitenguliwa ni mtu ambaye hatuwezi kumjua kwa urahisi: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Mtu huyu akiteuliwa umma haujui wala akitenguliwa haujui. Lakini huyo ndio mtu anayetakiwa awe maili million kadhaa kabla ya wabaya wanaoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Mara nyingi anafanyakazi kwa kushirikiana na watu kadhaa.
MIPAKA NA MIIKO YA WATU WA USALAMA WA TAIFA
Pigia mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUFANYAKAZI YA KUSIMAMIA SHERIA KAMA ILIVYO KWA POLISI. Pigia tena mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUMFUATILIA MTU KWASABABU MTU HUYO ANAJIHUSISHA NA MAANDAMANO YA KIKATIBA AU ANASHIRIKI AU KURATIBU MALALAMIKO DHIDI YA SERIKALI KWA NJIA ZINAZOFUATA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI.
Mfanyakazi wa TISS ana miiko mitatu mikubwa anayotakiwa kuizingatia awapo kazini. (i) kutotangaza kazi yake kwa njia yeyote isipokuwa kwa wanafamilia wakaribu tu. Mkurugenzi mkuu peke yake ndio anayetambulika tangu siku anaapishwa; (ii) kutunza siri za kazi zake zote. Yaani mlaji/mtumiaji wa taarifa za shushu ni rais na idara ya usalama tu, sio umma; (iii) kutotangaza chanzo au vyanzo vya taarifa au kumtaja raia aliyesaidia kupata taarifa za kintelijensia.
MASWALI NA MAJIBU
Nadhani baada ya kusoma bandiko hili utajiuliza TAKUKURU NI USALAMA WA TAIFA? ASKARI KANZU NI USALAMA WA TAIFA? Je wale vijana wanaokesha Best Bite, Break point, Kinondoni Biafara na Mlimani city bila kuwa na kazi maalum nao ni usalama wa taifa? Je wale tunaokunywa nao kisha wakalewa na kujitangaza watu wa idara nao ni usalama? Kama wanajitaganza USALAMA HUU KWELI UPO SALAMA?
Niseme kwa kunong'ona..!! Kimsingi kila wizara, kila shirika, kila kampuni kubwa, kila mkoa, kila wilaya, na kila kwenye shughuli kubwa ya kiuchumi tegemea kwa 90% uwapo wa watu wa usalama. Sasa wapo watu wa usalama wa ngazi mbalimbali; wapo wakudumu kwenye vituo vyao, wapo wafuatiliaji wa tukio/mtu, wapo wasaidizi walioajiriwa kwa kazi maalum ambao yawezekana wala hawajui wanafanyakazi ya idara na wapo wanaofanya ushushushu kwa mujibu wa kazi zao, mfano aliyekuwa kwenye kikosi cha usalama wa kiongozi wa juu Dar akipangiwa kazi nyingine Mufindi ujuwe amehama nyani na msitu wake.
Yote kwa yote huwezi kumjuwa mtu wa usalama aliyeiva kwenye kazi yake na anayefuata kanuni ya kazi yake. Unaweza kuhisi tu. Mtu wa usalama akijitagaza mtilie shaka hapo hapo kwasababu tayari anauweka usalama wa taifa kwenye hatari na yeye mwenyewe pia. Huyo anaweza kuwa MWEHU wa usalama wake mwenyewe. Muhimu usimwogope kama wewe ni raia mwema maana yeye analinda dola, na yeye sio polisi.
SEMA NIMESEMA
Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda
Lindi Tanzania
Tel: +255689463664
email: smembe426@gmail.com