Ziara ya Rais Xi Jinping barani Ulaya inaonesha kuwa nguvu ya kidiplomasia ya China inazidi kuimarika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,085
1,094
1715221012880.png


Mwanzoni mwa mwezi Mei 2024 Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya kiserikali katika nchi tatu za Ulaya, ziara iliyomfikisha Ufaransa, Serbia na Hungary. Kimsingi ziara za Rais Xi katika nchi hizi tatu zililenga mahusiano kati China na nchi hizo, hata hivyo kilichoonekana kwenye ziara hiyo ni zaidi ya mahusiano kati ya pande mbili.



Kwa muda mrefu sasa Ufaransa imekuwa ni nchi ambayo kimsingi sera yake kuhusu China imekuwa ni ya kujitegemea zaidi na isiyo na uhasama, licha ya kuwa inafuata makubaliano ya pamoja ya Umoja wa Ulaya kuhusu mambo ya diplomasia na hata uhusiano kati ya Umoja huo na China. Kutokana na hali hii, kwa muda mrefu sasa Ufaransa imekuwa na ushirikiano wa kunufaisha. Kwenye ziara hii moja ya mambo makubwa yaliyokuwa yakitajwa ni kuhusu makubaliano kuhusu biashara ya ndege aina ya Airbus kati ya China na Ufaransa.



Kwenye ziara hii Rais Xi pia alihudhuria mkutano wa baraza la biashara kati ya China na Ufaransa, wachambuzi wengi wameona kuwa biashara ni moja ya ajenda kuu kwenye ziara yake barani Ulaya. Makubaliano mapya kadhaa yalisainiwa na mengine mengi ya zamani yamehuishwa wakati wa ziara yake. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya changamoto za kibiashara kwenye uhusiano kati ya pande mbili kwenye muktadha wa Umoja wa Ulaya, lakini changamoto hizo hazikwamishi uhusiano kati ya China na Ufaransa.



Moja kati ya mambo yaliyofuatiliwa ni kauli ya Rais Emmanuel Macron aliyemtaka Rais Xi kutumia nguvu ya ushawishi ya China kwa Russia kukomesha mgogoro wa Ukraine. Inaweza kuwa vigumu kuamini kuwa Ufaransa ikiwa ni moja ya nchi zinazoshirikiana na Marekani na nchi nyingine za Ulaya kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Russia, kumwomba Rais Xi asaidie kutatua mgogoro ambao wanauchochea, lakini ni wazi kabisa kuwa kauli ya Rais Macron inathibitisha kuwa hadhi ya kidiplomasia ya China ni kubwa



Kwa mtazamo kama huo, tovuti ya France24 ilimnukuu mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya akipongeza ziara ya Rais Xi, na kusema ameonesha uongozi, na kwamba hata viongozi wa Ulaya wanamwomba kusaidia kutatua matatizo ya Ulaya, yaani mgogoro kati ya Russia na Ukraine.



Baadhi ya vyombo vya habari pia vimetoa makala zikiangalia mbali zaidi, na kuona kuwa kwa sasa mwelekeo wa siasa za dunia umejaa sintofahamu. Kuna uwezekano kuwa hali baada ya uchaguzi wa Marekani inaweza kuingiza dunia kwenye sintofahamu kubwa zaidi na kufanya dunia ihitaji uongozi imara. Kutokana na uimara na utulivu wa China, kuna uwezekano kuwa dunia ikaihitaji zaidi China baada ya uchaguzi nchini Marekani. Kwa hiyo baadhi ya wanahabari wameichambua ziara hiyo kuwa inaendana na mwelekeo wa siasa za sasa



Pamoja na kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatumia ziara hii kutaja mvutano kuhusu biashara kati ya China na Umoja wa Ulaya kuhusu magari ya betri na hata bidhaa za kielektroniki, ukweli ni kuwa ziara ya hii imepokelewa vizuri na watu wa Ufaransa ambao watanufaika na makubaliano ya biashara, na hata wale wanaoona kuwa China ni nguzi muhimu sio tu kwa biashara duniani, bali pia kwa usalama na utulivu wa muda mrefu wa dunia.
 
Back
Top Bottom