The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 746
- 2,103
Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi amewasili kwa na ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, kuanzia leo Juni 10, 2021 kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Viongozi hao wawili wanatarajia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya nchi mbili, uhusiano wa kidiplomasia, matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Botswana, bishara na uchumi pamoja na namna ya kuimarisha zaidi Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Updates:
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN:
UHUSIANO WA BOTSWANA NA TANZANIA NI TANGU ENZI ZA UKOMBOZI
“Karibu sana Rais Masisi, ziara yako nchini inatoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki wa kihistoria kati ya Botswana na Tanzania, uhusiano wetu ulianza tangu enzi za harakati za ukombozi, Tanzania, Botswana na Zambia zilikuwa mstari wa mbele kwenye kupigania Uhuru”
BIASHARA KATI YA NCHI MBILI IMEONGEZEKA
“Biashara kati ya Tanzania na Botswana imeongezeka kutoka Tsh. Milioni 731 mwaka 2005 hadi Tsh. Bilioni 3.5 mwaka huu, Botswana imewekeza nchini miradi yenye thamani ya USD Milioni 231 ambayo imetoa ajira 2128 kwa Watanzania”
MLIMANI CITY NI UWEKEZAJI WA WABOTSWANA
“Miongoni mwa miradi mikubwa ambayo Botswana wamewekeza Tanzania ni mradi wa Mlimani City, wengi tunakwenda pale kununua tunakwenda na Watoto wanacheza na nini lakini ni Uwekezaji wa Wabotswana walioingia mkataba pamoja na Chuo Kikuu cha DSM”
“Nimuhakikishie Rais Masisi kwamba tutalinda mradi wa Mlimani City (ambao Mwekezaji ni Botswana pamoja na UDSM) ili mradi ule uendelee kwa muda mrefu kwasababu mbali na biashara mradi ule umekuwa kivutio kwa Watanzania wengi”
WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA BOTSWANA
“Tumekubaliana kuwahamasisha Wafanyabiashara wa Nchi zetu kuchangamkia fursa zilizopo, Botswana inasifika kwa kupiga hatua kubwa kiuchumi Afrika ambapo inaongoza kwa kuuza Madini ya Almasi Duniani ila haiongozi kwa bahati mbaya ilijipanga nasi tumejifunza mengi kwao”
KUFUFUA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO
“Tumekubaliana kufufua Tume ya pamoja ya ushirikiano ambayo ilianzishwa mwaka 2002 na kufanya mkutano wake wa mwisho mwaka 2009 tumewataka Mawaziri wetu wa Mambo ya Nje kuitisha mara moja ili kuangalia maeneo ya ushirikiano ya kiuchumi na kijamii kwa undani zaidi”
NITATEMBELEA BOTSWANA
“Kutembelea kwa Rais Masisi Tanzania na tuliyompangia kufanya, kumempa hamu na yeye anialike Mimi kwenda kwake (Botswana) na nimepokea mwaliko huo na nimemuahidi nitatembelea Botswana wakati utakaporuhusu”
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Botswana, Dkt. Mokgweetsi Masisi, Dar es Salaam
RAIS WA BOTSWANA, DKT. MOKGWEETSI ERIC KEABETSWE MASISI:
KUFUFUA TUME YA USHIRIKIANO, MAWAZIRI WAANZE KUKUTANZA NDANI YA MIEZI 3
“Tumewaelekeza mawaziri wetu wa mambo nje kuweza kufufua ile tume ya ushirikiano na waanze kukutana ndani miezi mitatu, lazima wayabainishe maeneo ya ushirikiano ambayo mimi na wewe tumeyajadili ambayo ni utalii, mifugo, ulinzi na usalama pamoja na Corona,”
NIMEKUALIKA BOTSWANA KAMA RAFIKI NA KAMA DADA YANGU
“Nataka nikwambie mheshimiwa rais, kama kuna mtu alidhani unajialika mwenyewe Botswana nataka nitamke kwamba ni mimi ninayekualika. Ninakualika kama rafiki unawakilisha Watanzania lakini pia kama dada yangu,”
Njoo ili tuweze kushirikishana uzoefu wetu kwenye sekta ya madini namna ambavyo tunachimba na namna ambavyo tunanufaika na madini,”
“Utakuja kujionea mwenyewe namna ambavyo mahusiano yetu ya kidemokrasia yametusaidia kupata maji kutoka Angola na namna ambavyo tunatumia maji hayo,”
“Botswana ipo karibu sana, unaweza kupata kifungua kinywa Dar au Dodoma na ukapata chakula cha mchana Botswana,”