Katika hali isiyo ya kawaida vijana wanaosadikika kutoka vyama vya upinzani wamempa wakati mgumu mbunge wa jimbo la Bagamoyo , Dkt.Shukuru Kawambwa kwa kumuuliza maswali ya kebehi na kuudhi alipokuwa anafanya ziara jimboni kwake Bagamoyo mwezi wa Januari 2017.
Muuliza swali mmoja katika swali lake alimtaka mbunge aoneshe kwa juhudi zake amejenga vyumba vingapi vya madarasa huku akimtuhumu mheshimiwa Mbunge kujawa na màneno badala ya utendaji.Amemuuliza PhD yake imewasaidia nini wananchi wa jimboni mwake.
Muuliza swali mwingine amegusia swala la wazee kufyekeshwa barabara huku wakilipwa 2300 kwa siku kiwango ambacho ni kidogo bila ya mbunge kuchukuà hàtua.
Katika maelezo ya awali mbunge ameelezea jitihada zake binafsi katika kuleta maendeleo Bagamoyo.Amegusia mafanikio yake katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, usambazaji wa umeme vijijini, mchakato wa
ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na uwezeshaji wa makundi maalumu, ujenzi wa viwanda na mambo mengine.
Mwanzo wa mkutano alisifia mwitikio wa wananchi kuwa wengi , aliahidi kabla ya kuondoka kutembelea mradi wa ujenzi wa madarasa katika eneo alilohutubia adhma yake hii ilivurugwa na vijana hao waliyemuuliza maswali korofi, kwani alitumia muda mwingi mpaka giza kuingia kujibu maswali yao na kusahau kutembelea madarasa hayo.Mkutano huo wa wazi uwanjani uliisha zaidi ya saa moja jioni.
Mwisho wa mkutano vijana hao wahuni baadhi yao walikunywa viroba walimzomea mbunge wakati akiondoka.
Hii ni dharau ya hali ya juu kwa mwakilishi huyu halali wa wananchi wa Bagamoyo.Vitendo hivi vinamvunja moyo wa kuwatumikia wananchi.