Kuelekea 2025 Ziara ya Balozi Nchimbi yafyeka ACT, CUF na CHADEMA Kusini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
951
620
Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, inayoendelea katika mikoa ya Kusini, akianzia Mtwara na sasa yuko Lindi, imewahamisha viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema walioamua kujiunga CCM leo, wakisindikizwa na mamia ya wanachama waliorejesha kadi zao za vyama vya zamani kwa kasi kubwa kwenye mkutano wa hadhara.

Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mpilipili, Lindi mjini, ukiwa ni mwendelezo wa ziara ya Balozi Nchimbi, amewapokea viongozi hao waandamizi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mchinga Ndugu Hamidu Bobali akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Wanawake wa ACT Wazalendo Lindi Mjini Bi. Hawa Kipara, Meneja Kampeni wa Wabunge ACT Wazalendo Lindi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF Lindi Issa Sapanga, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mchinga, Mwenyekiti wa Wanawake Chadema Lindi Mjini pamoja na Wanachama 250 wa ACT Wazalendo.

Wakati akikabidhi kadi yake ya ACT na kujiunga CCM, Ndugu Bobali amesema;

“Nimeishi miaka 20 nje ya CCM ambako niliaminiwa sana katika ngazi tofauti ndani ya CUF na ACT Wazalendo hadi kuwa Waziri Kivuli wa Maji lakini nikiri niliyokuwa yanapigania Jemedari Samia ameyafanya kwa nguvu kubwa hivyo sina jinsi isipokuwa kujiunga CCM na kumuunga mkono. Kule upande wa pili tulikokuwa ametupiga kwenye mshono, hakuna tena agenda. Sasa hakuna kingine zaidi ya kazi nzuri za Dkt Samiana wenzangu hawa sasa tupo tayari kumsaidia.”

Naye Balozi Nchimbi akiwapokea wanachama hao wa vyama mbalimbali wakiongozwa na ACT Wazalendo amesema “karibuni huku wanachama wote ni sawa na mtapata ushirikiano mkubwa sana kuanzia sasa na kikubwa mmesema mmerudi sababu ya mambo makubwa yaliyofanywa na Dkt Samia nawapongeza kwa kuliona hilo mapema sasa tukaifanye Lindi ya kijani.”

🗓️ 30 Julai, 2024.
📍 Lindi Viwanja vya Mpilipili.

IMG-20240730-WA0555.jpg
IMG-20240730-WA0556.jpg
IMG-20240730-WA0557.jpg
IMG-20240730-WA0558.jpg
IMG-20240730-WA0559.jpg
IMG-20240730-WA0560.jpg
IMG-20240730-WA0561.jpg
IMG-20240730-WA0562.jpg
 
ZIARA YA BALOZI NCHIMBI YAFYEKA ACT, CUF NA CHADEMA KUSINI.

Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, inayoendelea katika mikoa ya Kusini, akianzia Mtwara na sasa yuko Lindi, imewahamisha viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo...
Kadi za Sasa hv ni za kidigital unazikusanyaje kirahisi hivyo acheni sanaa. Imani ya mtu siyo vikaratasi. Siasa hizo zimepitwa na wakati. Msigwa karudisha kadi lini?
 
ZIARA YA BALOZI NCHIMBI YAFYEKA ACT, CUF NA CHADEMA KUSINI.

Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, inayoendelea katika mikoa ya Kusini, akianzia Mtwara na sasa yuko Lindi, imewahamisha viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo...
Chadema hatuna card za namna hiyo wanajiongopea wenyewe
 
Wangekuwa wanaccm ndio wamerudisha hizo kadi, ungesema hayooo?
Siasa za kudanganya watu fulani karudisha kadi za zamani, mlipokuwa mnawahadaa wananchi Sasa hv watu wa leo siyo wa mwaka 47. Pia ni makosa Kwa nn asirudishe alikoitoa? Kwani unaowarudishia ni kadi yao? Halafu wanaopeleka wapi! Wanapenda kuigawa au kuichoma au kubandika ukutani
 
CCM bado wapo 1990
 
Wangekuwa wanaccm ndio wamerudisha hizo kadi, ungesema hayooo?
CHADEMA ilishatoka huko, ukivutiwa nayo ni unajiandikisha kidigitali na unapata kadi yako..maisha yanasonga.Mambo ya kurejesha/ kupeleka kadi hayana mantiki, zaidi mwanachadema akijisikia kusherehesha upande mwingine, anapeleka zile za zamani maana tunazo bado.Hata ya kwangu ya zamani nilimpa mtu akajiorodhesha kuirejesha Geita kwenye mkutano wa Upendo Peneza, akakunja buku dasi yake kiroho safiii,maisha yasonge.
 
Kwahyo siku izi hampokei wanachama wapya kwenye majukwaa yenu ya siasa kwa wanaorudisha kadi za ccm?
 
Back
Top Bottom