Zengwe: CHADEMA isipojiangalia Itaanguka Baada ya 2025

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
263
429
Umewahi kujiuliza kwanini vyama vya siasa hupoteza mvuto au kufa kabisa na vinaibuka vyama vingine ambavyo huchukua nafasi hiyo na kuwa na nguvu ambayo haukuwahi kufikiwa?

Yawezekana sio mara nyingi jambo kama hili kutokea katika uwanja wa siasa ya vyama vingi duaniani lakini inawezekana kabisa vyama kufa au kupoteza mvuto kwa raia wa taifa husika.

Kwa kutambua hilo ndio maana vyama ambavyo vipo madarakani katika utawala wa mataifa mbalimbali hujitutumua kwa kila hali ili kulipinda visianguke nafasi yake ikachukuliwa na vyama vingine vya upinzani.

Wakati mwingine vyama tawala hutumia kinyume nguvu ya dola kama vile jeshi, mahakama na bunge ili viendelee kubakia madarakani haijalishi vina sera nzuri au mbaya juu ya maendeleo ya watu na nchi husika.

Kwa upande wa vyama vya upinzani duniani kote Suala la kujilinda visianguke ni gumu sana kutokana na changamoto mbalimbali ambazo huvikabili, changamoto hizi hutokana na vyama vyenyewe na kuingiliwa na vyama tawala.

Vyama vya upinzani kuwa na sera nzuri tu haitoshi ili kulinda uhai wake bali kuna mambo kadhaa vinapaswa kufanya ili viendelee kudumu katika uimara na kutimiza adhma ya kuongoza serikali kwa kusilhinda uchaguzi.

Jambo moja likikosekana katika mkakati wa vyama vya upinzani ni vigumu kustawi bali vinaweza kufa visipo shituka na kuweka sawa mambo kabla hayajaharibika.

Ukizingatia hayo yote hivi karibuni hapa nchini mara kadhaa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo "Chadema", kupitia viongozi wake kumekuwa kikisiaitiza msimamo wake wa kutoshiriki chaguzi zote za viongozi katika serikali kwa sababu mbalimbali ikiwemo madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Chadema wanatumia Uchaguzi Mkuu wa 2020 kama kielelezo cha udhaifu wa katiba ya nchi ilivyo sasa ili kudai mabadiliko ya katiba yatakayo ondoa udhaifu na kufanya haki katika mambo mbalimbali ikiwemo kupunguza mamlaka ya Rais, kukomesha rushwa, kujenga serikali mpya ya muungano na mengine mengi kama ilivyo ainishwa kwenye rasimu ya Warioba ya 2014.

Hoja inayokaziwa zaidi kwa Chadema ni udhaifu wa tume iliyopo kuwa haiwezi kuleta ushindani wa Kidemokrasia kwakuwa haipatikani kwa njia iliyo huru kwa sababu viongozi wakuu wa tume pamoja na wajumbe wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwanachama cha siasa.

Chadema hukoleza msimamo wao kuwa kitendo cha uchaguzi wa serikali za mitaa kusimamiwa na watendaji wa halmashauri na serikali za mitaa hauwezi kuwa huru kwa kuwa hupokea maagizo kutoka kwa waajiri wao hivyo huharibu uchaguzi.

Msimamo wa Chadema ni kutoshiriki uchaguzi wowote unaohusu serikali mpaka pale katiba mpya na tume huru ya uchaguzi itakapopatikana.

Ingawaje mchakato wa katiba mpya na tume huru hauelezeki moja kwa moja bado Chadema wameshikiria msimamo.

Hivi karibuni Rais wa Tanzania Samia Suluhu aliteua kikosi kazi ambacho kimekusanya maoni juu ya mabadiliko ya katiba na tayari kikosi kazi kimekabidhi ripoti lakini ni vigumu kuelewa kuwa katiba mpya itapatikana lini.

Si hivyo tu Viongozi wakuu wa Chadema mara kadhaa wamekutana na Rais Samia ili kufanya maridhiano juu ya mambo mbalimbali nchini lakini bado mkutono wao haujatoa majibu kwa wananchi nini hatma yake.

Wakati sintofahamu hiyo ikiendelea unaweza kujiuliza je Chadema wasiposhiriki uchaguzi wowote hata uchaguzi mkuu wa 2025 watapata nini?.

Pili utajiuliza Kuwa Chadema imepima maono ya chama tawala CCM kuhusu madai ya katiba mpya, kwamba CCM inaguswa au haiguswi?.

Kwa maana kama CCM haiguswi na katiba mpya basi itaishawishi serikali isiitishe mabadiliko ya katiba wala kutekeleza madai yoyote ya Chadema ili uwe mtego kwa Chadema kutoshiriki uchaguzi wa 2025 na CCM ishinde kirahisi sana.

Pia Unaweza kujiuliza Chadema wasiposhiriki uchaguzi watamnufaisha nani chama chao au Chama tawala na vyama vingine ambavyo vitajikusanyia viti vya ubunge pasipo kutolewa chasho na chama kikuu cha upinzani?.

Mwisho wa kujiuliza utafunga mjadala kwa kuangalia madhara ya kutoshiriki uchaguzi kwa Chadema, je chama bado kitaendelea kuwa imara pasipo kuwa na uwakilishi serikali au kitaanguka na nafasi yake kuchukuliwa na chama kingine.

Ni kweli katiba mpya ni muhimu lakini pia njia ya kupima uhai wa chama ni kushiriki uchaguzi ili kujua ni kwa kiasi gani sera za chama husika zimewaingia wananchi.

Ni wakati sasa kwa Chadema na vyama vingine washirika kuangalia namna bora ya kupigania katiba mpya, ikiwemo kuongeza msukumo wa harakati kisiasa na kuongeza elimu kwa umma ili kujenga uelewa wa mambo ya kisiasa.

Chadema isipo jiangalia inaweza kuingia kwenye mtego ambao utakiangusha chama na kupoteza wanachama ambao watachukuliwa na vyama vingine wakati na baada ya uchaguzi wa 2025.

Safari ya mabadiliko ya kikatiba katikati nchi nyingi duaniani sio safari rahisi, inaitaji juhudi, utayari wa kuteseka, na kupambana kwa njia yoyote Ile kwa kushirikiana na raia kwakuwa nguvu ya watawala waliopo madarakani huwa kubwa na yenye mitego mingi sana.

Peter Mwaihola ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii na kisiasa.
 
Hata CDM wakiamua kushiriki, sisi wananchi wengi tumeshalipuuza box la kura. Hakuna mtu anayejitambua atashiriki tena kwenye hizo chaguzi za kishenzi. Ni vyema tukaangalia njia nyingine hasa ya machafuko, au kutengeneza mazingira ya kupindua nchi, kuliko kwenda kupoteza muda kwenye box la kura lisiloheshimika.
 
Mkuu Peter Mwaihola huwezi shiriki chaguzi eti kisa kupima uelewa wa sera, hujui Kila mkishindwa ndio morale ya wapiga kura inashuka?

Ni kheri usishiriki kuliko uhalalishe mchakato ambao sio halali. Kingine Chadema isiposhiriki itawapa leverage kubwa zaidi kwenye kudai katiba mpya maana wata risk positions na ruzuku Ili kupambania katiba hii itaonyesha seriousness hasa kwa serikali na wananchi.

Sio mara ya kwanza hata Odinga alisusa uchaguzi wa 2017 na amepata kura nyingi 2022 kuliko 2017, same to Arusha Chadema ilisusa kiti Cha umeya 2011 ila ikaja kuzoa almost kata zote 2015. So sio mara ya kwanza kwa chama kususia uchaguzi ikiona haki haijatendeka but trust me mara zote imerudi ikiwa imara zaidi ya chaguzi zilizopita. Kwa udhaifu huu wa Samia na CCM hata Chadema isipopiga kampeni inakura nyingi sana za hasira hiyo 2030 if at all watasusa 2025!!
 
Kuna vitu vingi vya kugain kwa CDM kuliko kupoteza endapo hawatashiriki uchaguzi

1. Upotevu wa fedha
2. Kupoteza maisha
3. Kupoteza muda nk

Naunga mkono CDM kutoshiriki uchaguzi endapo mazingira ya uchaguzi hayatakuwa sawa. Dogo wewe ni shahidi hapo mwakaleli 2020 hakukuwa na uchaguzi bali uporaji wananchi walimkataa huyo MCCM lkn matokeo yalilazimishwa je kuna faida gani kushiriki uchaguzi huo?

CDM isiposhiriki ni alert kwa jumuiya za kimataifa kuona kipi kipo tanzania huenda ht kupewa kibano cha kutopewa misaada.
 
Naibu katibu mkuu ameshasema bila katiba mpya chadema haitashiriki na uchaguzi wenyewe hautafanyika.Nakuomba embu tujadilie uwezekano wa chadema kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kama upo.

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Uwezo wa wananchi hawa waoga kuzuia siuoni, labda yafanyike mashambulio ya kigaidi kwenye vituo vya kura, na hasa nyakati za kampeni. Bila mashambulio ya kigaidi kwenye mikutano ya kampeni sioni chaguzi kutofanyika. Sana sana CDM wasiposhiriki uchaguzi utakuwa na wapiga kura wachache sana.
 
Back
Top Bottom