Sikilizia Ubuyu huu wa motomoto!
Zari hana presha na Wema wala Kajala kama watu wengi wanavyodhani.. Kwa mujibu wa chanzo kutoka kwa TeamDiamond, Zari anamhofia zaidi Jackline Wolper ambae aliwahi kutoka na Diamond.
Unaweza jiuliza, iweje Wolper wakati saa hivi anatafunwa na Harmonize??? Sasa mdaku wetu amesasambua kuwa ukaribu baina ya Wolper na Diamond ni kabambe kuliko hata ukaribu wa akina Wema na Kajala kwa Chibu. Unakubali?
Chanzo kinazidi kupayuka kuwa, pamoja na Wolpa kuwa na Harmonize, ila pia yuko karibu mno na Chibu (ex wake) na hii inaweza kuwa rahisi kwa musee kuchepuka kirahisiii na bila kujua. Mashosti wa Zari wamemshauri awe makini!
Wema hayuko karibu tena na Chibu kivile na wala hawawasiliani tangu watemane.. Na hata miezi kadhaa iliyopita Zari alitonywa awe macho na Kajala kufuatia tetesi kuwa Diamond anamkunja Kinyemela..
Ila Zari, hawa mademu wawili (Wema na Kajala) wala hawamtii presha kama Wolper..
''Zari hana amani, hana imani na Wolper kabisaa na wala sio Wema au Kajala. Mashoga zake wanamwambia Wolper anaweza kuwa anaminyana na Diamond kisirisiri kwa sababu wana uhuru na hata kazi wanafanya pamoja'' kilifunguka chanzo chetu.