peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,940
Unguja, Serikali ya Zanzibar imekabidhiwa rasmi takwimu (data) za utafutaji wa mafuta na gesi kutoka Serikali ya Tanzania. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo Jumatano Agosti 10, 2022 Ikulu ya Zanzibar kwa kutiliana saini kati ya Waziri wa Nishati wa Tanzania, January Makamba na Waziri wa uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Zanzibar, Suleiman Masoud Makame.
Awali takwimu hizo zilikuwa zikihifadhiwa na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (Pura), ambapo sasa imekabidhi takwimu hizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA). Hatua hiyo inatoa fursa kwa sasa Zanzazibar kuanza kujisimamia katika suala hilo na kuliondoa kwenye Muungano.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema kuna kila dalili inayoonyesha Zanzibar ina rasilimali ya kutosha ya mafuta na gesi. “Mungu atatuwezesha Zanzibar sasa ianze kuchimba mafuta na gesi, kila dalili zipo za kuwa na rasirimali ya kutosha kilichobaki ni kukamilisha kutoka hapa kwenda hatua nyingine. Hizi data nyingi zipo katika hatua ya 2D tunatakiwa twende hatua ya pili ya 3D na ya tatu ni kuanza kuchimba.”
Dk Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji katika sekta hiyo ili kuendelee kufanya utafiti na kuchimba rasilimali hiyo itakayoleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa Zanzibar. Amesema iwapo Zanzibar ikifanikiwa kupata mafuta na gesi asilia, uchumi utabadilika kwa kiasi kikubwa na tayari kitalu cha Zanzibar-Pemba wameshapata takwimu za awali zinazoonyesha kuwa na kiasi cha trilioni 3.8 za gesi asilia.
Naye, Waziri Makamba amesema takwimu hizo ni muhimu katika mnyororo wa utafiti na utafutaji mafuta na gesi. Amesema vitalu vilivyokabidhiwa ni vitano; kitalu namba tisa, 10, 11, 12 na kitalu cha Zanzibar-Pemba. Amesema tangu miaka ya 1950 zilipoanza shughuli za utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi, data zimekusanywa katika maeneo ya baharini na nchi kavu zinazohusisha mitetemo ya 2D kiasi cha kilometa za mraba 139,000 na data za mitetemo za 3D kilometa za mraba 32,094 na data za miamba kutoka kwenye visima 96 vilivyochimbwa na kuchorongwa.
Kwa upande wake, Makame amesema licha ya utafutaji wa mafuta na gesi kuanza kipindi kirefu, kwa Zanzibar ilikuwa ni nadharia ila kwa kukabidhiwa takwimu hizo sasa wanaanza kazi hiyo kwa vitendo. “Wawekezaji walikuwa wakija na kuondoka kwasababu ya kukosa data hizi, sasa zitakuwa kichocheo cha utafutaji wa kukuza uchumi wa Zanzibara,” amesema.
Chanzo: Mwananchi